Tuesday, December 1, 2020

TUMEJIFUNZA NINI AFCON 2017?

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA ZAITUNI KIBWANA

UHONDO wa Fainali za Mataifa ya Afika za mwaka huu (Afcon 2017), ulimalizika na kuishuhudia Cameroon ikilipeleka taji hilo jijini Younde.

Cameroon iliyoongozwa na kocha wa kigeni Mbelgiji, Hugo Broos, ilipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Misri katika mchezo wake wa fainali.

Mashabiki wa soka watakubaliana na mimi kuwa ilikuwa ni moja kati ya mechi kali tangu kuanza kwa mashindano hayo mwezi uliopita.

Kilichoufanya mtanange huo kunoga zaidi ni historia ya timu hizo zinapokutana.

Historia inaonyesha kuwa fainali hiyo ilikuwa kama marudiano ya ile ya mwaka 2008 kwa mataifa hayo mawili, wakati Misri  ilipotwaa ubingwa wa Afcon.

Cameroon kushinda katika fainali ya mwaka huu ni kama kisasi kwa Misri.

Kwa matokeo hayo, Cameroon inakuwa imechukua taji hilo kwa mara ya tano huku Misri bado wakiendelea kuwa wababe wa michuano hiyo wakiwa wameliweka ndani mara saba.

Kama kawaida Tanzania hatukufuzu fainali hizo na tuliishia kuikodolea macho na kuwashangaa wachezaji wa timu za wenzetu, hata zile ambazo tungehitaji nguvu ndogo tu kuzifikia.

Tofauti na mashabiki wengi wa soka ulimwenguni kote ambao walikuwa na hamu ya kuwashangaa akina Pierre-Emerick Aubameyang, Asamoah Gyan, binafsi nilivutiwa zaidi kuzitazama Guinea Bissau na Uganda.

Ndiyo, niliamini kuna cha kujifunza kutoka kwa mataifa hayo madogo katika soka la Afrika na ulimwenguni kote. Kila nilipozitazama nchi hizo, niliamini kulikuwa na darasa kubwa kwa soka letu.

Nisingeweza kupata picha halisi ya Ramadhani Kichuya kwa kumtazama Aubameyang, lakini Jjuuko Murshid aliyekuwa na Uganda ‘The Cranes’ hakuwa na tofauti kubwa na wachezaji tulionao Taifa Stars, ikizingatiwa kuwa anacheza hapa Bongo.

Guinea Bissau ilishiriki fainali hizo kwa mara ya kwanza tangu nchi hiyo ilipopata Uhuru wao mwaka 1974 kutoka kwa Wareno.

Kwa hesabu za haraka, imewachukua miaka 43 kutimiza ndoto yao ya kucheza Afcon.

Kwa maana nyingine, wakati Tanzania inashiriki mwaka 1980, ndiyo kwanza Taifa hilo lilikuwa na miaka sita tangu lilipojiondoa kwenye utawala wa Wareno.

Kama wao wametumia miaka 43 kufika Afcon, kwanini Tanzania tushindwe ikiwa wao hawajafikisha hata miaka 40?  Naamini inawezekana tukijipanga.

Ukiachana na Guinea, wenzetu Uganda imewachukua miaka 39 kabla ya kupata nafasi ya kurudi kwenye michuano hiyo.

 

Historia inaonyesha kuwa Uganda imecheza fainali za Afcon mara sita (1962, 1968, 1974-78).

Ni kweli soka la Uganda limeizidi Tanzania  kwa kiasi hicho cha kuwatazama kupitia vituo vya runinga na mitandao wakizichakaza nyasi za Gabon?

Nini kilichosababisha Uganda kutuzidi kete kiasi hicho? Hakuna jibu zaidi ya ubabaishaji.

Wenzetu wako makini wanapokuwa wamepanga mambo yao. Huwezi kukuta mipango ya mdomoni kama iliyojaa kwenye soka la Tanzania.

Huwezi kukuta ligi ya vijana ikianzishwa kisiasa kwa lengo la kuwanyamazisha wadau wa soka na kupiga fedha za bure huku ikiwa hoi kwa ukata na ratiba isiyoeleweka.

Kufikia mafanikio ya Uganda na Guinea Bissau, unahitaji kufanya maandalizi ya maana, mfumo mzuri na wa kisasa wa uzalishaji wachezaji chipukizi, unahitaji kuwa na wachezaji wanaocheza nje na zaidi unahitaji kuwa na benchi la ufundi linaloeleweka.

Kwa bahati mbaya, katika yote hayo, Tanzania hatuna hata moja. Kocha ataingia leo na kutoka kesho, washindi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambayo ndiyo msingi wa Stars, wanapatikana kwa nguvu ya fedha na wachezaji wanaotegemewa kuiwakilisha nchi katika michuano ya kimataifa ni ‘mababu’.

Tukiri kuwa kilichozibeba Uganda na Guinea ni kuepuka mipango mingi ya kabatini.

Hebu fikiria, tayari ratiba ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za Afcon za mwaka 2019 imetoka. Lakini je, kuna mpango gani umeanza kusukwa kuhakikisha tunafika Cameroon kucheza fainali hizo? Ukiuliza utaambiwa: “Bado mapema mno, kwanza kundi letu jepesi.”

Tatizo letu ni kwamba, tunaishi kwa kukariri na tunapokuta tulichokiamini kimebadilika, basi ndipo tunachanganyikiwa.

Mbali na Uganda na Guinea Bissau ambazo mwaka huu zimetupa somo, naamini fainali za mwaka 2019 zitakuja na mataifa mapya ambayo aidha hayajawahi au ni muda mrefu umepita tangu waliposhiriki Afcon. Kwanini isiwe Tanzania? Naomba kuwasilisha.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -