Monday, November 23, 2020

TUMEMALIZA MWAKA, UBABAISHAJI TFF UKIENDELEA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ONESMO KAPINGA

MCHEZAJI wa African Lyon, Venance Ludovick, ametufungia mwaka na kutukaribisha mwaka mpya wa 2017 huku ubabaishaji ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ukiendelea kama kawa.

Usajili wa Ludovick katika klabu ya African Lyon unaonekana wa utata baada ya kubainika kwamba ana leseni ya timu mbili, yaani Mbao FC na African Lyon zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katika mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo, mchezaji huyo alipewa leseni ya kuichezea Mbao FC, lakini baada ya usajili wa dirisha dogo mchezaji huyo amehamia African Lyon lakini akiwa hajamalizana na timu yake ya zamani.

Mchezaji huyo ametufungia mwaka 2016 huku ubabaishaji wa uendeshaji wa soka ukiendelea hasa katika usajili wa wachezaji, kwani kila baada ya usajili ni lazima utasikia jambo.

Limekuwa ni jambo la kawaida kwa utawala huu wa Rais wa TFF, Jamal Malinzi, kusikia msuguano katika suala zima la usajili kwani katika ligi ya vijana kulitokea utata wa aina hii, ambapo mchezaji Christopher Paschal pia alikuwa na leseni mbili ya Panone na Kagera Sugar.

Suala la Ludovick kuonekana usajili wake una utata ni baada ya African Lyon kutoka sare ya kufungana bao 1-1 na Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, uliochezwa Desemba 23 mwaka jana, kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Matokeo hayo yaliibua mambo yaliyofichika kuhusu usajili wa mchezaji huyo, baada ya kubainika ana leseni mbili za kuchezea soka.

Tumesikia kwamba mchezaji huyo ana leseni ambayo alipewa na TFF baada ya  Mbao FC kumwombea usajili kwa ajili ya kuichezea timu yao.

Na baada ya kuitumikia Mbao FC kwa nusu msimu akiwa bado ana mkataba na klabu yake ya zamani, amepewa leseni nyingine kwa ajili ya kuitumikia African Lyon.

Udhaifu huu wa TFF wa kumruhusu mchezaji huyo kuichezea African Lyon umewafanya Yanga wakimbilie kudai pointi tatu, ingawa ofisa habari wa shirikisho hilo, Alfred Lucas, anajaribu kuficha ukweli kwamba hawajapata barua ya Yanga ya kulalamikia mchezaji huyo.

Wewe mdau wa soka unatarajia Alfred atakubali kirahisi kwamba Yanga wamewasilisha barua ya kudai pointi tatu kutokana na African Lyon kumchezesha mchezaji huyo, wakati akijua mabosi wake wamefanya madudu?

Hata kama barua hiyo atakuwa ameiona, Alfred hawezi kusema kwani atakuwa amejimaliza mwenyewe kabla  hawajalimaliza suala hilo kimya kimya.

Kwa hali inavyoonekana TFF watakuwa wanataka kulimaliza suala hilo la mchezaji kimya kimya ikijua Mbao FC hawana ubavu wa kuendelea kupaza sauti kutokana na mazingira yaliyopanda daraja msimu uliopita.

Lakini Yanga wanaweza kuzimwa hasa ukizingatia walisaidiwa katika suala la mchezaji wao, Hassan Ramadhan ‘Kessy’, waliyemsajili kimakosa kutoka Simba na wao kuwakalia kooni.

Kama unakumbuka TFF walipeleka jina la Kessy katika usajili wa Yanga kwa ajili ya michuano ya Kombe la Afrika yaliyofanyika mwaka jana, huku mtandao wa uhamisho wa kimataifa ukisomeka ni mchezaji wa Simba.

Ulikuwa ni ubabaishaji mwingine wa TFF na kama Shirikisho la Soka Afrika (CAF), wasingekuwa makini basi usajili wa Kessy ungekamilika kama huo wa mchezaji wa Mbao ambaye inaelezwa ana leseni ya kuzitumikia klabu mbili.

Sakata la Kessy limemalizika baada ya kigogo wa TFF kukutana na Simba katika chakula cha mchana, kilichoendelea katika mazungumzo yao.

Kama suala la Kessy lilimalizwa kwa njia hii, unataka kuniambia watashindwa hilo la mchezaji wa Mbao? Mazingira yatatengenezwa na usajili wa mchezaji huyo kuonekana ni halali kuitumikia African Lyon.

Mzee wa Kupasua anauliza kwamba, ina maana Sekretiati ya TFF ilikuwa haina kumbukumbu ya mchezaji Ludovick kuwa alikuwa na leseni ya kuichezea Mbao?

Na baada ya kusajiliwa na African Lyon katika dirisha dogo walijiridhishwa na vielelezo vilivyowasilishwa na klabu hiyo kuwa ni mchezaji huru kama anavyodai Katibu Mkuu wa Lyon, Ernest Brown?

Tutaona Jumatatu ijayo

MZEE WA KUPASUA, kapssmo@gmail.com O716985381

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -