Friday, November 27, 2020

TUMSAIDIE MALINZI MAANDALIZI FAINALI ZA U-17 MWAKA 2019

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

TANZANIA inatarajiwa kuwa mwenyeji wa fainali za vijana wenye umri chini ya miaka 17 (U-17) za Afrika zitakazofanyika hapa nchini mwaka 2019.

Nafasi hiyo ya kuandaa fainali hizo, imepatikana baada ya jitihada zilizofanywa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi pamoja na viongozi wenzake, ikiwa ni sehemu ya kuamsha msisimko wa mchezo wa soka nchini ambao kwa siku za hivi karibuni umeonekana kudorora kutokana na sababu mbalimbali.

Japo wapo wanaodhani Tanzania haikuwa na sababu ya kuandaa michuano hiyo kwa wakati huu ambao soka la nchi yetu limeporomoka kiasi cha kutisha, lakini ukweli unabaki pale pale kuwa hiyo ni hatua kubwa mno kuelekea kile wapenzi wa soka hapa nchini wanakiota, yaani timu zetu kufanya kweli kwenye michuano ya kimataifa kama si wachezaji wetu kutamba Ulaya.

Tayari TFF imeanza maandalizi ya timu yetu yenye wachezaji wenye umri chini ya miaka 14 (U-14) iliyopo chini ya kocha Oscar Milambo ambayo hadi mwaka 2019, wachezaji wake watakuwa wamefikisha umri wa miaka 17 hivyo kuwa na sifa ya kukipiga katika fainali hizo.

Ukiachana na TFF, kuna wadau kadha wa kadha ambao wameonekana kuguswa na fainali hizo kwa kuona ni vipi wanaungana na shirikisho hilo la soka nchini kuhakikisha ifikapo 2019, tunakuwa na timu kabambe ya kuwatoa kimasomaso Watanzania.

Miongoni mwa wadau hao ni Kampuni ya New Habari (2006) ambayo kwa kushirikiana na Kanali Iddi Kipingu (mstaafu), hivi karibuni waliandaa mpango wa kusaka vipaji vya soka kwa wanafunzi waliomaliza darasa la saba mwaka jana ili kupata udhamini wa masomo Lord Baden Powell Memorial High School iliyopo Bagamoyo, mkoani Pwani.

Baada ya mchakato uliofanyika kwa miezi mitatu, hatimaye watoto 20 wenye vipaji vya soka vya hali ya juu, lakini walio na umri chini ya miaka 14, walipatikana na kupata udhamini huo wa masomo kwa miaka minne ambapo watakuwa wakipata muda wa kupewa mafunzo ya soka na makocha wanaotambulika na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na lile la Kimataifa (Fifa).

Japo watoto wengi waliojitokeza katika mpango huo kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini walikuwa na vipaji vya hali ya juu, waratibu waliamua kuwachukua wale wenye umri chini ya miaka 14 ambao hadi kufikia mwaka 2019 watakuwa na umri wa miaka 17 hivyo kutoa nafasi kwa kocha wa timu ya Taifa ya umri huo kuwa na uwanja mpana wa kuchagua kikosi chake badala ya kutegemea wale wanaolelewa na TFF pekee.

BINGWA tunaamini iwapo kutajitokeza wadau zaidi na kufanya kama yale yaliyofanywa na New Habari kwa ushirikiano na Kanali Kipingu na shule yake ya Lord Baden, ni wazi kuwa uenyeji wetu wa fainali hizo za vijana unaweza kuwa wa mafanikio makubwa kwa timu yetu kubeba kombe.

Kila mmoja wetu ni vema akafahamu kuwa huu ni wakati mwafaka wa kila Mtanzania kutoa mchango wake katika maandalizi ya fainali hizo za vijana, iwe ni kwa upande wa kuandaa timu au maandalizi mengineyo.

Mwisho wa siku, kila mmoja ashiriki katika maandalizi ya fainali hizo tukiwa kama wenyeji ili kama ni kuboronga, basi kusiwapo na Mtanzania yeyote wa kumnyooshea kidole Malinzi na TFF yake, bali kila mmoja wetu awajibike na matokeo hayo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -