Wednesday, August 12, 2020

TUNA KILA SABABU YA KUIFUATILIA AFCON 2017

Must Read

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi...

LIBREVILLE, Gabon

PAZIA la michuano ya AFCON kwa mwaka 2017 litafunguliwa leo kwa wenyeji Gabon kuvaana na Guinea-Bissau kwenye mchezo wa kwanza wa Kundi A.

Tayari kila mmoja amekuwa akiongea la kwake kuhusu mataifa 16 yatakayoumana kuwania taji hilo kubwa kwa upande wa soka barani Afrika.

Makala haya yamekuletea dondoo baadhi kuelekea kwenye fainali hizo zinazotarajiwa kuwa kali na za kusisimua.

Wenyeji

Awali mashindano haya yalipangwa kufanyika Libya kabla CAF hawajafanya maamuzi ya kubadilisha na kuwapa Gabon mwaka 2014, baada ya kuwa na wasiwasi na usalama wa raia juu ya machafuko yaliyokuwa yakiendelea nchini humo.

Mabadiliko haya yakawafanya Gabon kuandaa fainali hizi kwa mara ya pili, baada ya awali waliposhirikiana na Equatorial Guinea mwaka 2012.

Viwanja vinne tu ndivyo vitakavyotumika kwa michezo yote huku ule wa Stade de l’Amitie wenye uwezo wa kuchukua watu 40,000, ukiandaliwa kwa ajili ya mchezo wa fainali.

Wanaopewa nafasi

Mara zote imekuwa ngumu kutabiri ni nani atabeba kombe la Afrika na hii ni kutokana na upinzani mkubwa wa mataifa yanayoshiriki.

Kwenye fainali nne za mwisho, tuliona mataifa manne tofauti yakibeba taji hili, wakiwamo Zambia walioshtua wengi miaka mitano iliyopita walipoibuka mabingwa.

Lakini kwa mwaka huu ziko baadhi ya timu ambazo zinapewa nafasi kubwa kubeba taji la Afrika, kwanini na ni timu zipi hizo? Majibu yako chini.

Ivory Coast

Wanaingia Gabon kama mabingwa watetezi na wanapewa nafasi kubwa kutetea tena taji la Afrika.

Uwapo wa nyota kama Willfried Bony anayekipiga katika klabu ya Stoke City, beki kisiki wa Manchester United, Eric Bailly na winga hatari wa Crystal Palace, Willfried Zaha unawapa viburi mashabiki wa taifa hilo kuona wana kila sababu ya kubeba taji hilo.

Senegal

Mara ya mwisho kuonyesha umwamba wao katika soka ni mwaka 2002 kwenye Kombe la Dunia.

Lakini kizazi hiki kipya katika kikosi cha taifa cha Senegal kimewafanya wengi kuamini kuwa huu unaweza kuwa mwaka wao wa kurudi kwa kishindo kwenye ramani ya soka.

Wana Sadio Mane wa Liverpool na Idrissa Gueye wa Everton katika kikosi chao na wana kila sababu ya kutunishiana misuli na miamba mingine ya soka la Afrika.

Algeria

Licha ya kufuzu mara mbili mfululizo kucheza Kombe la Dunia, Algeria hawajafanikiwa kubeba taji la Afrika tangu mwaka 1990.

Lakini uwapo wa nyota wa mabingwa wa England, Leicester City na mchezaji bora wa Afrika, Riyadh Mahrez, unawapa kiburi mashabiki wa Algeria kuamini kuwa huu ni mwaka wao wa kumaliza ukame huo.

Mahrez akishirikiana na nyota anayekipiga naye katika klabu ya Leicester, Islam Slimani, wanatazamia kuongoza safu ya ushambuliaji ya timu hiyo na kubeba taji kwenye ardhi ya Gabon.

Ghana

Licha ya kuwa timu tishio barani Afrika lakini bado Ghana hawajafanikiwa kubeba medali ya Afcon tangu mwaka 1982.

Mwaka huu wanaongozwa na kocha wa zamani wa Chelsea, Avram Grant na wanatajwa kuwa kikosi chenye wachezaji wengi wanaocheza soka nje ya Bara la Afrika.

Ndugu wawili, Andre na Jordan Ayew na straika mkongwe Asamoah Gyan ndio wanaotabiriwa kuliongoza taifa hilo kubeba taji la Afcon mwaka huu.

Usiwabeze na hawa

Pamoja na miamba hiyo minne kupewa nafasi kubwa ya kubeba taji, ziko timu tatu ambazo zinapewa nafasi kubwa ya kushangaza wengi na kubeba taji.

Misri (wakiwa na rekodi ya kutwaa kombe hili mara 7), Gabon (wenyeji wa mcihuano wakiwa na straika hatari barani Ulaya kwenye kikosi chao, Pierre-Emerick Aubameyang) na mwisho ni Cameroon (wanaokuja mashindano na kikosi chenye sura tofauti na zilizozoeleka na wengi).

Wanaopewa nafasi ya kung’aa

  1. Pierre-Emerick Aubameyang, Gabon

Macho ya wenyeji wa michuano hii, Gabon yatakuwa kwa straika wao Pierre Aubameyang, anayekipiga katika klabu ya Borrusia Dortmund inayoshiriki Bundesliga nchini Ujerumani.

Kwa zaidi ya misimu mitatu sasa, Aubameyang amekuwa katika kiwango cha juu sana hivyo kuwapa imani mashabiki wa Gabon ya kubeba taji la Afrika mwaka huu.

Mzaliwa huyu wa Ufaransa aliyechukua uraia wa Gabon, alikuwamo kwenye orodha ya wachezaji wanaoongea tuzo ya mchezaji bora Afrika na mwaka huu tayari ametajwa kwenye listi ya wachezaji 10 bora zaidi duniani.

Aubameyang anasifika zaidi kwa kasi yake, ufungaji na uwezo mkubwa wa kucheza nafasi zote katika idara ya ushambuliaji.

Gabon watayahitaji sana mabao yake na bila shaka Aubameyang binafsi atakuwa na ndoto za kuwa mchezaji bora wa michuano hii, hivyo lazima afunge na awe kwenye kiwango cha juu sana.

2.Riyad Mahrez, Algeria

Kila shabiki wa soka atakuwa na shauku ya kuona ubora wa Riyad Mahrez, mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2016.

Staa huyu wa Algeria alikuwa na msimu bora sana alipoiongoza klabu yake ya Leicester kubeba taji la kwanza la Premier League na la kihistoria kwao nchini England.

Mahrez alifunga mabao 17 msimu uliopita na kubeba tuzo ya mchezaji bora wa kulipwa nchini England, Mwafrika wa kwanza kutwaa tuzo hiyo.

Yupo kwenye kikosi cha Algeria na wengi wanatamani kuona akitakata zaidi kwenye michuano hii mikubwa kwa Bara la Afrika.

  1. Sadio Mane, Senegal

Mane (24) ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza ghali Afrika baada ya Liverpool kulipa kiasi cha pauni mil 34 wakimsajili kutoka Southampton.

Msimu wake wa kwanza akiwa Anfield, amefanikiwa kufunga na kuasisti mabao mengi na kuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Liverpool kinachofukuzia ubingwa wa EPL msimu huu.

Kasi, uwezo wa kufunga na kuasisti unamfanya Mane awe mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Senegal kilichopania kurejesha nguvu yao katika michuano ya Afrika.

  1. Mohamad Salah, Misri

Winga huyu wa AS Roma amekuwa kwenye kikosi cha Misri tangu mwaka 2011, pia alishiriki kwenye fainali za Kombe la Dunia U-20 na Olympic mwaka 2012 akiwa na jezi ya taifa hilo.

Alibeba taji la kwanza la Uswisi msimu wake wa kwanza akiwa na FC Basel na alibeba tuzo ya mchezaji kinda wa Afrika mwaka 2012 kabla mwaka 2013 kubeba tuzo ya mchezaji bora wa Uswisi.

Ni mchezaji hatari kwa kasi yake na anatabiriwa kufanya makubwa kwenye michuano hii akiwa na miamba hiyo mikubwa ya soka barani Afrika.

  1. Adre Ayew, Ghana

Mara zote Ghana huwa hawana bahati ya kupata mastraika wengi, lakini safari hii wataingia Gabon wakiwa na jina la Adre Ayew kwenye vichwa vyao.

Ayewe anayekipiga katika klabu ya West Ham, ni miongoni mwa wachezaji nyota katika kikosi cha Black Stars kwenye miaka ya hivi karibuni.

Ni mzuri kwa kumiliki mpira, kasi na mahiri wa kufunga mipira ya vichwa. Bila shaka wapenzi wa soka watakuwa na shauku ya kutaka kuuona ubora wa Ayew katika ardhi ya Gabon.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa timu hiyo kuwa atajituma na...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi katika klabu ya Simba kwa...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -