Sunday, October 25, 2020

TUNAHITAJI MKAKATI IMARA KUIKWAMUA STARS

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA MARY PETER TSJ
UNAWEZA kukaa chini na kujiuliza hivi ni kweli hatuwezi kabisa? Je, hatufanyi juhudi za kutosha kuhakikisha  tunafanya vizuri. Au mazingira pengine ndio huwa kikwazo linapokuja suala la kimataifa?

Ni kweli kwamba kujikwaa si kuanguka labda kwa timu yetu ya Taifa imekuwa kawaida kushindwa katika mechi nyingi wanazocheza na kuwepo kwa siasa na visingizio vingi kuwapoza wapenzi na mashabiki wa soka ili ionekane kawaida.

Hakuna shaka kwamba kama taifa, Serikali haitoi sana kipaumbele katika michezo, jambo ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa sekta ya michezo kufanya vibaya hasa katika ngazi ya kimataifa ambako wadau wengi wa michezo hapa nchini wamekuwa na kiu kubwa ya kuona tunapiga hatua.

Mbali na kuwa na mianya ambayo imewafanya wachezaji wetu hasa wa soka wa timu ya Taifa kupata nafasi mbalimbali ya kushiriki katika  michuano, bado imekuwa ikionesha hawajaiva vilivyo ikilinganishwa na wachezaji wa timu nyingine, ndiyo sababu tunaharibu katika michezo ya kimataifa.

Taifa Stars imekuwa ikishuka katika viwango vya ubora vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), ngazi ya Afrika pia hatuko vizuri, lakini hata kwenye Ukanda wa Afrika Mashariki bado tuko nyuma sana ikilinganishwa na wenzetu.

Si kwamba Tanzania hatuwezi kufanya vizuri, tuna wachezaji wengi wenye vipaji vya hali juu sana, lakini pengine kuna tatizo ambalo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na wadau wengine wanatakiwa kulifanyia kazi kuhakikisha tunalitatua kwanza.

Tuna makocha wazuri wazawa na kwa bahati nzuri, makocha hawa wamekuwa na mafanikio makubwa katika kuibua na kukuza vipaji vya wachezaji, lakini hatuna mipango thabiti ya kuwaendeleza wachezaji hao hadi kufikia katika ngazi za kimataifa.

Japo kumekuwa na michuano mingi ya kuibua vipaji, lakini vipaji vinavyoibuka vinaishia hewani kwa kucheza katika timu za hapa nyumbani za madaraja ya chini na wanaobahatika hufika katika klabu kubwa za ligi kuu na kuishia hapo.

TFF imekuwa haina mkakati mzuri wa kuendeleza vipaji vya wachezaji wetu, ndiyo maana leo hii hatuna wachezaji wengi wanaocheza soka katika nchi zilizoendelea kisoka. Tunatamani kuwapata kina Mbwana Samatta wengine wengi lakini hatuna mbinu na njia ya kuwapata wachezaji hao au kuwafikisha wengine katika anga hizo.

Timu yetu ya taifa ina wachezaji watatu wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi, hatuwezi kulingana na mataifa mengine, Zimbabwe tuliocheza nao wao wana wachezaji wengi na kwenye timu iliyoitwa kucheza na Taifa Stars, wachezaji 19 wote wanacheza nje ya Zimbabwe na wengine watamba kabisa huko barani Ulaya.

Kwa sasa tunao Serengeti Boys ambao wanaonekana kuja vizuri, lakini wachezaji hawa wahapo kwenye mfumo wa ligi yoyote na hawawezi kuwa wazuri kwa kukaa wao kama wao wakifanya mazoezi na kucheza mechi za kirafiki pekee. Lazima TFF ifanye mbinu ya kuhakikisha wachezaji hao wanapelekwa katika Academy za soka za klabu mbalimbali Ulaya ili wakue zaidi kisoka kama kweli tunahitaji waje kutufanyia mabadiliko miaka ijayo.

Naamini TFF ina mahusiano mazuri na vyama vya soka vingine huko Ulaya na hivyo inaweza kuomba kupata nafasi kwa wachezaji hao kuunganishwa katika programu za klabu kadhaa, angalau wachezaji 10 tu wakiwa nje wakija watakuja na kitu kipya kuliko kuendelea kuwaweka pale Karume.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -