Friday, December 4, 2020

TUNALAANI KITENDO KILICHOFANYWA NA WAKALA WA TRA

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

JUZI Wakala wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), alikamata gari lililokuwa limewabeba wawakilishi wetu, vijana wa Serengeti Boys waliokuwa wakienda Ikulu kwa mwaliko wa Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.

Kukamatwa kwa gari lao kulifanya wachezaji hao kushushwa njiani na kutafutiwa usafiri mwingine wa kuwafikisha kwenye mwaliko huo ambao Makamu wa Rais alikuwa akiutumia kuwaaga wachezaji hao na kuwapa baraka zake na za Serikali wakati wakielekea kwenye michuano ya AFCON ya vijana baadaye mwezi ujao.

BINGWA tunapinga na kulaani kitendo hicho kilichofanywa na wakala huyo wa TRA hata kama ilikuwa kwa maelekezo ya nani, kwani mbali na kuwa ni kitendo dhalili kilichowadhalilisha wachezaji hao, lakini pia kuwasababishia usumbufu wa kiakili jambo ambalo hawatakiwi kuwa nalo katika kipindi hiki.

Kwa sasa Serengeti Boys walitakiwa kupewa kila aina ya sapoti na si kuwavuruga kwa kukosa ustaarabu kwa baadhi ya mawakala ambao kwao wanaona pengine ni sifa kubwa kwa mtu aliyewapa jukumu la kuidai TFF.

Hatupingi TFF kudaiwa, lakini si kwa utaratibu huu uliotumika ambao kwa namna moja au nyingine unaonekana kulenga zaidi kuidhalilisha TFF na sasa kuwadhalilisha wawakilishi wetu na kuwaharibia saikolojia yao ambayo vyombo vya habari na wadau wengine wamejitahidi kuwajengea wachezaji hao kuelekea katika michuano hiyo mikubwa.

Hatukutegemea kitendo hicho kufanywa na Watanzania wenzetu tena wasomi na ambao wanafahamu kinachoandelea pale TFF na kwa vijana hao.

Tunaamini wakala hao wa TRA waliolikamata basi na kuwashusha wachezaji, wangetumia busara tu baada ya kuwaona na kuwapa heshima yao na si wachezaji tu, lakini pia hata kama wangekuwa abiria wengine walipaswa kuheshimiwa kwani kulikuwa na njia nyingine ya kulishika basi hilo kama walikuwa wakilihitaji.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -