Sunday, November 1, 2020

TUNAMCHUKIA WEMA SEPETU NA KUMSAHAU MUNGU?

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA HASSAN DAUDI


SIKU chache zilizopita, tasnia ya burudani nchini ilichangamshwa kama si kutikiswa na sekeseke zito la vitendo vya imani za kishirikina.

Kama ilikupita, mastaa wa filamu na mitindo, Wema Isack Sepetu na Hamisa Mobetto na mwanamuziki, Naseeb Abdul ‘Diamond’, ndio waliokuwa wahusika wakuu wa filamu hiyo iliyokuwa na mguso mkubwa mitandaoni na hata katika vyombo vingine vya habari (magazeti, redio na runinga).

Balaa lilianza pale Wema alipoonekana kushabikia kitendo cha Mobetto kutajwa kumwendea kwa mganga baba mtoto wake, Diamond, ambaye ni mwimbaji, mwandishi wa nyimbo, bosi wa lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) na mmiliki wa kituo cha runinga, Wasafi Tv.

Moto ulikolezwa zaidi na ‘timu’ za waigizaji hao wa filamu (Wema na Mobetto) kwani ndizo zilizokuwa ‘bize’ kutupiana vijembe katika mitandao ya kijamii.

Lengo la makala haya si kulizungumzia kwa undani tukio hilo la aibu na lisilovutia, hasa kwa vijana wanaotamani kufikia mafanikio waliyonayo nyota hao.

Mbali ya angalizo hilo, ieleweke kuwa makala haya hayalengi kuwa na upande katika mtifuano huo wa warembo hao wa tasnia ya burudani, Wema na Mobetto.

Kwa ufupi, kutokana na ukubwa wa majina yao, labda ingependeza zaidi kuona wakimaliza tofauti zao kuliko kuungana na mmoja wao katika hiki kinachoendelea.

Nikirejea katika maudhui ya makala haya, binafsi nilifuatilia kwa karibu ‘komenti’ za pande hizo mbili, asilimia kubwa wakiwa ni wale waliokuwa wakimponda Wema kwa ‘kushadadia’ tukio hilo la Mobetto kufedheheka.

Hata hivyo, nikiri wazi kuwa nilikwazwa na baadhi ya mashabiki waliokuwa wakimtupia madongo Wema, walionesha wazi kuwa si sehemu ya jamii ya wastaarabu.

Isieleweke kwamba, namtetea mshindi huyo wa taji la Miss Tanzania katika shindano la mwaka 2006, lakini ukweli ni kwamba wengi waliokuwa wakimkosoa juu ya kutokushika ujauzito hawakuwa wakimtendea haki.

Sina shida na majina yote ya kejeli aliyokuwa akipewa Wema na mashabiki hao ila kuitwa mgumba kulikengeuka misingi ya utu na ni katika jamii ya washenzi ndiko utaweza kusikia mwanamke akitaniwa kwa jina hilo.

Nakiri kuwa Wema anatakiwa kuadhibiwa kwa maneno makali kutoka kwa mashabiki au wapinzani wake pale anapowakosea, lakini hebu tujiulize, hili la kutoshika ujauzito ni uamuzi wake?

Niseme tu kuwa kwa kujua au kutokujua, waliokuwa wakitumia kauli hiyo kama fimbo, eti wakijipambanua kuwa ni mashabiki wa Mobetto, walikuwa wakifanya ukosoaji dhidi ya kazi ya Mungu.

Licha ya mvutano wao wa sasa, hapo naona namna ambavyo hata Mobetto anaweza kutofurahishwa na kejeli hiyo dhidi ya mwanamke mwenzake.

Kama walivyo wanawake wengine, hakuna ubishi kuwa Wema naye angetamani kuwa na mtoto na kama Muumba angeamua, basi huenda ni kitendo ambacho kisingechukua zaidi ya dakika moja.

Ni wazi wakosoaji wake katika sekeseke lake na Mobetto walitumia nguvu kubwa zaidi dhidi yake? Huenda alistahili kuadabishwa, lakini kuitwa ‘mgumba’ haikuwa adhabu ya kawaida.

Kwa upande mwingine, unaweza kuitafsiri kuwa ilikuwa ni chuki kubwa zaidi dhidi yake na kwa bahati mbaya iliambatana na kufuru (kufanya kinyume cha matakwa ya Mungu).

Hao wanaomsema Wema kwa kutozaa wanajua ni wanawake wangapi ulimwenguni, hata wengine maarufu na wenye fedha zao zaidi yake, wanateswa na hali hiyo?

Hawakuona kama kumtukana kwa kigezo hicho ni kuwahuzunisha na kuwaliza wanawake wengine wanaohaha usiku na mchana kupata ujauzito?

Lakini je, kwa hiki kinachoendelea sasa kati ya wawili hao, endapo Wema angekuwa ndiye mama mtoto wa Diamond, leo hii hao wanaomwita mgumba wasingeelekeza kauli chafu hiyo kwa Mobetto?

Niseme tena, kwamba labda Wema alistahili kila kauli chafu kama waliokuwa wakimkosoa waliamini amewakosea ila haikuwa sahihi kumhukumu kwa uamuzi huo wa Mungu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -