Friday, November 27, 2020

TUNATAKA KANDANDA SAFI TAIFA LEO

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

TIMU za Simba na Azam zinatarajiwa kupambana leo katika mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu soka  Tanzania Bara utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Pambano la Simba na Azam linatarajiwa kuwa la ushindani kutokana na historia ya timu zote mbili, mbali na hilo pia matokeo ya mwisho ya mchezo wa fainali Kombe la  Mapinduzi zilizofanyika visiwani Zanzibar ambapo Simba ilifungwa bao 1-0 yanachagiza mchezo huo.

Hivyo katika mchezo wa leo, Wekundu hao wa Msimbazi watahitaji kulipa kisasi na kupata matokeo mazuri ili kujihakikishia wanaendelea kutamba kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.

Kwa upande wao Azam nao watahitaji kuendeleza ubabe dhidi ya Simba, lakini pia kupata pointi tatu ili kujiweka kwenye nafasi nzuri katika msimamo wa ligi hiyo.

Simba wanaongoza kwenye msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi 45 mbele ya watani wao wa jadi, Yanga wakiwa nafasi ya pili na pointi 43 huku Azam ikiwa nafasi ya tatu na pointi 31.

Sisi BINGWA tunaamini kwamba mchezo wa leo tutaona kandanda safi, pia waamuzi wafuate sheria 17 za mchezo huo zilizowekwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

Tunafahamu kwamba Simba na Azam zote ni timu kubwa na zina wachezaji wazuri, wenye majina makubwa na wakimataifa pia, lakini wanahitaji kutulia kucheza kwa ustadi na kuweza kuzipatia timu zao matokeo yanayostahili.

Mara kadhaa kumekuwa na malalamiko kwa waamuzi kutokana na maamuzi yao yasiyofaa na wengine wakilalamikiwa kuchezesha kwa mapenzi huku wakizipendelea timu wanazozipenda.

Kwa kufanya hivyo wanaharibu taaluma yao lakini pia mara kadhaa kutokana na maamuzi yao mabovu wamekuwa wakisababisha vurugu kutoka kwa wachezaji husika na kwa mashabiki wa timu hizo.

Bingwa tunawatakia kila la kheri timu zote mbili katika mchezo huo na waamuzi wawe makini na kila kitu kiende sawa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -