Sunday, January 17, 2021

Tunataka kuona burudani Simba, Yanga

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

Simba-vs-Yanga.-1

NA WINFRIDA MTOI

PAMBANO la watani wa jadi la Ngao ya Jamii, Simba na Yanga, linatarajiwa kupigwa Agosti 23, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Litakuwa ni pambano la aina yake kutokana na ukweli kwamba litavuta hisia za mashabiki wengi nchini na Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Pamoja na burudani wanayotarajia kupata mashabiki wa pande zote mbili, lakini mara nyingi katika pambano la watani kumekuwa kukijitokeza matukio mbalimbali ndani na nje ya uwanja.

Hiyo inatokana na presha ya mashabiki ambao wanakwenda uwanjani wakiwa na lengo moja la kuondoka na furaha ya ushindi.

Pambano la Agosti 23 litakuwa la nne kuwakutanisha watani hao wa jadi ambalo lilikuwa linaitwa Ngao ya Hisani, mara ya kwanza kucheza ilikuwa mwaka  2001 na  Yanga walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Baada ya hapo ikasimama, wakaja kukutana tena mwaka 2010 ikiwa inaitwa Ngao ya Jamii na Yanga kushinda kwa  mikwaju ya penalti 3-1, baada ya kumaliza dakika 90 bila kufungana. Mchezo mwingine ulikuwa 2011 ambapo Simba walishinda mabao 2-0.

Msisimko wa pambano la Ngao ya Jamii umezidi kuongezeka siku hadi siku, kitendo kinachoashiria kutakuwa na upinzani mkali.

Kuelekea  katika pambano hilo, tayari kila timu imejichimbia kivyake licha ya kwamba klabu zote zimeelekea visiwani Zanzibar, Yanga wapo Kisiwa cha Pemba na Simba Unguja.

Tunajua kwamba timu hizo zimekwenda kuweka kambi visiwani humo  kwa lengo la  kufanya maandalizi ya kutosha kuhakikisha  wanaweka vikosi tayari kwa  ajili ya mtanange huo  ambao ndio  ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Tofauti na maandalizi hayo, inafahamika timu hizo zimefanya usajili wa wachezaji wapya wa kuongeza nguvu na kuziba mapengo yaliyoonekana katika msimu uliopita.

Simba inaonekana kufanya usajili mkubwa zaidi kwa kuchukua wachezaji wengi ambao ni nyota kuliko wapinzani wao Yanga ambao kipindi cha usajili walikuwa wanakabiliwa na ukata.

Hata hivyo, kulingana na utamaduni wa mechi za mahasimu hao wawili, licha ya usajili na vitu vingine bado presha inaendelea kuwepo  ambapo  kinachoangaliwa zaidi ni matokeo ya uwanjani pekee.

Desturi hiyo imekuwa ikisababisha mechi ya Simba na Yanga kuchezwa katika hali ya tofauti na michezo mingine, kwani  mara nyingi hutawaliwa na ubabe, mabavu na kupoteza ladha halisi ya soka.

Tumezoea kuona mechi nyingi za Simba na Yanga zikikosa utulivu  kuanzia uwanjani kwa wachezaji  na waamuzi hadi mashabiki waliokaa jukwaani.

Ni kweli lazima mshindi apatikane, lakini  timu zijaribu kucheza soka  zuri la ushindani ambalo  litamfanya mshindi apatikane kishujaa na kumpa raha shabiki aliyetoa fedha na kupoteza muda wake kupata burudani.

Timu zitakapocheza vizuri kwa kufuata sheria na kujiamini kwa maandalizi waliyofanya, yale mambo tunayoshuhudia kila mara kama vurugu zisizokuwa na mpango hazitajitokeza kipindi hiki.

Sawa wapo wale ambao wamezoea vurugu na wanakwenda uwanjani wakiwa wamejipanga, lakini naamini wengi wao wanakwenda  kwa ajili ya kupata burudani ya soka na si vinginevyo.

Binafsi ninachoweza kusema ni kwamba klabu na mashabiki wajipange  kuzishangilia timu zao ili waweze kupata burudani  na matokeo  mazuri.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -