Wednesday, October 21, 2020

TUPO VIZURI KISANAA ILA MWAKA 2017 TUREKEBISHE HAYA

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

MWAKA 2016 umekuwa wa mafanikio kwenye sekta ya burudani Tanzania. Wasanii, wakishirikiana na wadau wa sanaa kwa nguvu kubwa kutoka kwa wewe shabiki, wamefanya makubwa tunayoweza kujivunia.

Tukianza kwenye tasnia ya muziki wa kizazi kipya, tumeshuhudia maendeleo makubwa kuwahi kutokea. Hatua za kwenda mbele zimepigwa na wasanii wetu na wameweza kuliteka soko la muziki wa Afrika.

Hivi sasa chati kubwa za muziki kwenye redio na runinga za kimataifa nyimbo kadhaa za Bongo Fleva hazikosekani. Hiyo yote imetokana na ukweli kwamba, uwekezaji mkubwa umefanyika kuanzia kwenye audio hadi video za muziki huu.

Ukuaji huo wa muziki umefanya wasanii wetu watajwe kushiriki kwenye tuzo kubwa za muziki Afrika. Mwaka huu ndiyo wasanii wengi zaidi wamepata nafasi ya kuchomoza kwenye tuzo hizo, kitu ambacho ni ishara tosha ya ukuaji wa Bongo Fleva.

Hali kadhalika tumeshuhudia muziki wa singeli unaoakisi maisha ya Watanzania wengi ukichipua na kukua kwa haraka, huku ukiwaneemesha wasanii wake na kukata kiu ya burudani kwa mashabiki.

Wakati muziki ukizidi kufanikiwa, kwenye upande wa filamu bado hatujaona makali, bado tasnia hii haijawa tishio kwa nchi nyingine za Afrika, kitu ambacho kinafanya ionekane imelala, japokuwa ina wasanii wazuri wenye uwezo na vipaji vya haja.

BINGWA tunafurahi kuona sanaa yetu inapiga hatua. Hongereni wasanii, wadau na mashabiki kwa ujumla kwa kuwa ndio mmekuwa chachu ya mabadiliko haya yaliyosubiriwa kwa muda mrefu.

Safari bado ni ndefu, tunahitaji muda kutafakari njia rahisi ya kupunguza kasoro zilizojitokeza mwaka huu na zikaturudisha nyuma. Mambo ya ushabiki usio na maana (timu) yametuponza mno mwaka huu.

Yamefanya wasanii fulani wakose tuzo. Sasa kwanini sisi kwa sisi turudishane nyuma? Haifai, tunapaswa kuacha ushabiki usio na faida na kuondoa tofauti zetu pale tunapovuka mipaka ya Tanzania.

Muziki wa dansi umesahaulika, hakuna anayeutazama, mikono ya wadau imeishikilia Bongo Fleva pekee ilhali dansi ina mashabiki wengi.

Mwaka 2017 tusiutupe muziki huu, wadau tuweke nguvu zetu huko ili matunda ya ukuaji wa muziki yawe kwa wasanii wa aina zote za muziki bila ubaguzi unaoendelea sasa.

Jambo lingine la msingi kwa wasanii wetu ni kuongeza ubunifu katika kazi zao. Tunaweza kusema kwenye filamu hakuna jipya, ila tukija kuchunguza tutabaini hakuna ubunifu, wasanii wanafanya kazi kimazoea.

Mwisho kabisa suala la kufanya kazi zisizo na maadili limejitokeza sana mwaka huu. Wasanii wa muziki wamefungiwa kazi zao na mamlaka husika, hiyo yote inaweza kuzuilika na kazi zinazozingatia mila, desturi na tamaduni zetu zikatutambulisha vyema kimataifa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -