Monday, August 10, 2020

Tusila, Mozizi tayari Yanga

Must Read

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi...

NA MMVITA MTANDA

YANGA kupitia wadhamini wao, GSM, wamefanikiwa kumalizana na nyota wawili wa kigeni, Tusila Kisinda wa AS Vita na Mpiana Mozizi (FC Lupopo) zote za DR Congo.

Akizungumza na BINGWA jana, meneja wa wachezaji hao, Nestory Mutuale, alisema ameshakamilisha mazungumzo yote na GSM, hivyo ataongozana na nyota hao kuja kukamilisha mikataba yao.

Alisema atawasili nchini mapema Julai wakati ligi ikiwa inakaribia kwisha, ili wajiunge na wenzao kwenye maandalizi ya asimu mpya (Pre-seasons).

“Nashukuru kwamba tayari nimeshakamilisha mipango ya kuwapeleka wachezaji wangu Yanga, tunazungumza na GSM mara kwa mara, pia wameshafuatilia CV (wasifu) zao na wamejiridhisha, nawaletea wachezaji bora ambao hawatajutia kuwasajili,” alisema Mutuale.

Mutuale alisema kama isingekuwa tatizo la janga la virus vya corona, tayari wachezaji hao wangeshafika Tanzania.

@@@@@@

Molinga apelekwa Azam

NA MWAMVITA MTANDA

KLABU ya Azam ya FC, inakaribia kuinasa saini ya straika wa Yanga, David Molinga, ambaye anatarajia kumaliza mkataba wake na Wanajangwani hao Julai, mwaka huu.

Molinga alitua Yanga mwanzoni mwa msimu huu, ikitokea FC Lupopo ya DR Congo na kusaini mkataba wa mwaka mmoja.

Akiwa ni miongoni mwa wachezaji wa Yanga wanaotajwa kuwa katoka orodha ya watakaotemwa, Meneja wake, Nestory Mutuale, amepanga kumpeleka Azam.

Akizungumza na BINGWA jana, Mutuale alisema kuwa anahofia Yanga watamwacha Molinga, hivyo tayari ameshaanza mazungumzo na Azam ambao wapo tayari kumchukua.

Alisema kuwa Molinga ni mchezaji mzuri ila Yanga wameshindwa kumtumia ipasavyo ndio maana anaonekana kuwa na kiwango cha chini.

“Molinga ni mchezaji ambaye alikuwa anafanya vizuri katika Ligi ya Congo na kuwa na mabao mengi, ndio maana hata Mwinyi Zahera alimkubali, lakini nashangaa nini kinamkuta sasa.

“Kama watamwacha, atakwenda Azam nao pia wanamuhitaji sana, najua atakwenda kufanya vizuri zaidi, kwani bado umri wake ni mdogo anaweza kufika mbali akijituma,” alisema Mutuale.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa timu hiyo kuwa atajituma na...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi katika klabu ya Simba kwa...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -