Tuesday, October 27, 2020

Tusimchukulie poa yule ‘chotara wa Zimbabwe’

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

HARARE, Zimbabwe

MOJA kati ya matukio ya dharau kabisa mtu anaweza kukufanyia kwenye soka ni kukupiga bonge la bao, halafu anashangilia kama Cristiano Ronaldo kisha anaomba ‘sub’.

Wazimbabwe wametufanyia hivi!

Dakika ya 55, Matthew Rusike akiwa nje kidogo ya eneo la 18, alipokea pasi safi kutoka kwa Nyasha Mushekwi na kuamua kunyoosha msuli wake, akaachia bonge la shuti.

Nina hakika kabisa kijana wetu Aishi Manula aliruka ili kutoa lawama tu, lakini lilipopita lile kombora hakuliona hata chembe, Zimbabwe wakaandika bao la pili.

Kama haitoshi, Rusike akavua jezi yake na kuitupa chini kisha akatunisha mwili kama anavyofanya nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo.

Wallahi tena, nilipouona mwili wa Rusike namna ulivyojengeka kimazoezi, akili yangu ikajifikirisha kabisa mateso aliyokuwa akikumbana nayo Vicent Andrew ‘Dante’.

Lakini sekunde tu baada ya kushangilia, Rusike alipeleka macho yake kwa kocha wake na kuomba ‘sub’, alichoka au aliona angeendelea kutudhalilisha tu? Yeye ndiye anayejua zaidi!

Kumekuwa na mijadala mingi sana kwenye vijiwe vya soka hapa Tanzania juu ya Mathew Rusike, wengi wanatamani kujua historia yake na wapi anapocheza soka lake, yuko Afrika au Ulaya?

Makala hii imebeba majibu ya maswali yote hayo!

Jina lake kamili ni Matthew Tyrell Rusike, amezaliwa Juni 26, mwaka 1990 katika Jiji la Harare, Zimbabwe. Ukipiga hesabu za haraka, utagundua kuwa umri wake ni miaka 26.

Baba yake ni Philip Rusike, raia wa Zimbabwe na mama yake ni Sue Rusike, Mwingereza aliyechukua uraia wa Afrika Kusini. Bila shaka mpaka hapa utakuwa umeshafahamu uchotara wake ulipotokea.

“Baba yangu ni Mzimbabwe, amezaliwa pale na anaishi pale siku zote. Mama yangu ni raia wa Afrika Kusini na hii ndiyo sababu nina ‘passport’ mbili.

“Mama amechagua kuishi na baba Zimbabwe na anamiliki saluni yake kubwa ya kike,” alisema Rusike.

Rusike alianza maisha yake ya soka nchini England katika akademi ya kituo cha klabu ya Charton Athletic, kipindi hiki akiwa na miaka 16.

Lakini kwa bahati mbaya sana, straika huyu hakudumu sana England kutokana na kukwama kwa kibali chake cha kufanyia kazi nchini humo.

“Nilienda kujaribu bahati yangu pale lakini bahati mbaya sikuweza kukaa sana baada ya kukwama kwa kibali changu,” alisema Rusike alipofanya mahojiano na jarida la The Standard.

“Niliamua kurejea nyumbani na kucheza ligi ya hapa Zimbabwe, nilijiunga na klabu ya Monomotapa na katika mwaka wangu wa kwanza tulifanikiwa kubeba ubingwa.”

Baada ya hapo, Rusike alihamia nchini Afrika Kusini na kuzichezea klabu za Jomo Cosmos na Kaiser Chiefs kabla ya kwenda nchini Sweden.

Akiwa Sweden, Rusika alijiunga na klabu ya Halmstard BK kwa mtakaba wa mwaka mmoja na nusu kabla ya kuihama na kutimkia katika klabu ya Helsingborgs IF inayofundishwa na straika wa zamani wa Manchester United, Henrik Larsson.

Rusika anasifika kwa soka la kasi, nguvu na chenga za maudhi. Ni kipenzi cha mashabiki wa Zimbabwe kila anapokuwa na mpira mguuni kwake.

Ni miongoni mwa washambuliaji wanaotegemewa na taifa hilo kwenye fainali za Afcon zitakazoanza kutimua vumbi Januari 14, mwakani kule Gabon.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -