Friday, October 30, 2020

TWENDENI TUKAWALIZE CAPE VERDE

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA AYOUB HINJO

KIINGILIO cha kuiona timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, ikimenyana na Cape Verde leo ni buku mbili tu, ni rahisi kabisa, tujitokeze uwanjani na familia, marafiki na ndugu wa karibu kuishangilia Taifa Stars.

Kila Mtanzania alivunjika moyo baada ya Taifa Stars kupigwa mabao 3-0 na Cape Verde katika mchezo uliochezwa wiki iliyopita, jijini Praia na kutoa lawama nyingi kwa kocha wa kikosi hicho, Emmanuel Amunike.

Katika mchezo huo, wachezaji wa Taifa Stars walikosa mawasiliano mazuri na kupelekea kufungwa mabao mawili kipindi cha kwanza, hapo ndipo ukawa mwisho wa mchezo huo.

Kwa kiasi kikubwa, ili uweze kupata matokeo ya ushindi kwa aina ya michezo hiyo, inakuhitaji uwe na uhakika wa kutumia vizuri nafasi unazotengeneza lakini haikuwa hivyo kwa Taifa Stars ambao walishindwa kufunga bao.

Aina ya wachezaji waliosimama mbele huonekana bora na wenye msaada kama timu inatengeneza nafasi za kutosha, kila mmoja anafahamu ubora wa Mbwana Samatta, Simon Msuva na Thomas Ulimwengu ulipo.

TAYARI TUMEIONA SURA MOJA YA AMUNIKE

Katika michezo miwili aliyoiongoza Taifa Stars, Amunike, alionekana kutumia falsafa ya kujilinda zaidi, akitumia wachezaji wenye utimamu wa kuzuia wengi zaidi.

Alifanya hivyo katika suluhu dhidi ya Uganda kwenye Uwanja wa Mandela, pia, aliingia nao nchini Cape Verde ambako Stars waliambulia kichapo kikali cha mabao 3-0, ikiwa ni kipigo cha kwanza ndani ya Kundi L, ikiwamo Lesotho.

Hiyo ni sura ya kwanza ya Amunike katika michezo hiyo miwili aliyoiongoza Stars, huku Watanzania wengi wakionekana kutofurahishwa na falsafa hiyo ya kujilinda.

Mchezo wa tatu ni leo katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ambao ni nyumbani kwa Stars, kila mdau wa soka anasubiri kuona kipi kitaenda kutokea hasa kwa Amunike ambaye alijihami michezo miwili iliyopita.

Inaaminika timu inapokuwa nyumbani lazima ishambulie ili kupata matokeo ya ushindi kwa kutengeneza nafasi nyingi za mabao, mchezo wa kwanza uliochezwa katika Uwanja wa Chamazi, Stars walikosa nafasi nyingi za mabao na kufanya matokeo kuwa sare ya 1-1 na Lesotho.

Shambulia, shambulia, shambulia kwa nguvu, kila Mtanzania anaamini Stars inaweza kuvuna matokeo mazuri kwa kutumia staili hiyo ya kucheza katika mchezo wa leo.

Wachezaji wa aina hiyo wapo ndani ya kikosi hicho; Msuva, Samatta, John Bocco, Mudathir Yahya na wengine wengi wanaweza kuwa hatari zaidi kama timu itaamua kushambulia na kutengeneza nafasi za kutosha.

NYONI AITWA FASTA

Erasto Nyoni ni moja ya mabeki bora nchini kwa sasa akiwa anakitumikia kikosi cha Simba, amejumuishwa katika timu ya Stars kuongeza nguvu kwenye safu ya ulinzi.

Nyoni hana kasi kubwa lakini ni mwepesi kuuelewa mchezo na kutambua kipi cha kufanya kwa uharaka pindi anapokuwa na mpira au hana, pia ni kiongozi mzuri ndani ya uwanja.

Beki huyo ambaye amevaa jezi ya timu ya Taifa kwa miaka 11, ana uwezo mkubwa wa kutumika katika nafasi nyingi uwanjani, inawezekana akatumika kama kiungo mkabaji, beki wa kati au pembeni.

Kuitwa kwake kunamfanya kocha kuwa na machaguo mengi katika safu ya ulinzi na kutoa majukumu kwa wachezaji bila wasiwasi ukizingatia Hassan Kessy na Ulimwengu, wataukosa mchezo wa leo kwa adhabu ya kadi mbili za njano.

NAFASI BADO IPO KWA STARS

Mpaka sasa, Stars imevuna pointi mbili katika michezo mitatu waliyocheza kwenye Kundi L ambalo lina timu za Uganda, Cape Verde na Lesotho.

Kama Stars wakifanikiwa kupata ushindi leo watakuwa na pointi tano ambazo zitaongeza mwanga kwa Tanzania kufuzu katika michuano ya Mataifa Afrika ambayo mara ya mwisho ilikuwa mwaka 1980 nchini Nigeria.

Uganda wanaongoza kundi hilo kwa pointi saba, wakifuatiwa na Cape Verde wenye nne, huku Lesotho na Tanzania wakiwa na pointi mbili kila mmoja.

Kikosi cha Stars: Aishi Manula, Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Kelvin Yondani, Abdi Banda, Erasto Nyoni, Mudathir Yahya, Himid Mao, Simon Msuva, John Bocco na Mbwana Samatta.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -