Wednesday, October 28, 2020

TWITE NENDA, RAGE ATAKUKUMBUKA DAIMA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

KIUNGO Mnyarwanda mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mbuyu Twite, anatarajiwa kuagwa rasmi leo na mashabiki wa Yanga wakati timu yao itakapovaana na JKU ya Zanzibar katika mchezo wa kirafiki utakaopigwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, ikiwa ni baada ya klabu hiyo kumsajili Mzambia, Justine Zulu.

Twite mwenye uwezo wa kumudu namba nyingi awapo uwanjani, alijiunga na Wanajangwani hao mwaka 2012 akitokea St. Eloi Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Yapo mengi ya kukumbukwa kutoka kwa kiungo huyo mwenye mbwembwe nyingi akiwa uwanjani, lakini kubwa ni lile zengwe lake kwenye usajili.

Licha ya mwenyewe kuahidi kuwapo Tanzania na ataonekana kwenye ligi ya Bongo kama kawaida, bado ile fitina aliyoifanya ya kusaini Yanga ipo kichwani mwa mashabiki wa Simba mpaka sasa.

BINGWA limeyachambua matukio yake ambayo kamwe mashabiki wa soka hawawezi kumsahau hata kama ataendelea kuwapo nchini au kuonekana katika timu nyingine.

Alimliza Ismail Aden Rage

Kiraka huyo atakumbukwa na mengi kwenye soka la Bongo hasa Mwenyekiti wa Simba enzi hizo, Ismail Aden Rage alipomwaga machozi baada ya kutoa kituko cha aina yake kwa kuanza kusaini Simba Julai 2012 mjini Kigali, Rwanda akiwa mchezaji wa APR lakini siku chache baadaye akasaini na Yanga kama mchezaji wa St. Eloi Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Rage alikwenda Kigali kumsajili Twite na kumpa dola za Marekani 30,000 na akafuata taratibu zote hadi kupewa uhamisho wake na Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA), lakini baadaye mchezaji huyo akasaini Yanga na ikaelezwa alikuwa anacheza kwa mkopo kutoka Lupopo ambayo ndiyo walikuwa wana haki ya kumhamisha na si APR.

Tukio hilo limemsikitisha sana Rage ambaye alijinasibu kumalizana na beki huyu na kumpa namba jezi iliyoitangaza wakati wa Tamasha la Simba Day, Uwanja wa Taifa na matokeo yake akayeyuka na kusaini Yanga.

Rage ambaye pamoja na uzoefu wake wote katika masuala ya usajili na fitina za mpira, lakini kwa Twite alichemka na badala yake mashabiki wa klabu hiyo wakaamua kumtupia lawama lukuki.

Mashabiki wa klabu hiyo waliitoa thamani klabu yao kwa ajili ya Twite hasa baada ya kukumbuka wapinzani wao walivyomchukua Kelvin Yondan na kumsainisha mkataba ambao mpaka leo bado anaendelea kukipiga kwenye kikosi hicho cha Wanajangwani.

Wakati Simba wakiumia, Yanga wao kauli yao ilikuwa ‘mnakumbuka Victor Costa? Mlivyofanya msilalamike sana huu mchezo hauhitaji hasira’, jambo lililokuwa likizidi kuwatia uchungu Wekundu wa Msimbazi hao.

Lakini mwisho wa sakata hilo, Twite aliyetoka Lupopo alipitishwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kucheza  Yanga na ile ITC ya Simba ikitupwa.

Simba walichobahatika ni kurudishiwa fedha zao dola 32,000 baada ya TFF kuwaamuru Yanga kuzirudisha.

Mikono yake bado historia

Uwezo wa mikono yake bado ni historia baada ya kiraka huyo kuweka rekodi ya pekee ligi kuu (VPL) mzunguko wa kwanza, kufuatia kurusha mpira na kumtungua kipa wa Mbao FC, Emmanuel Mseja na kusaidia ushindi wa timu yake wa mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Uhuru.

Uzembe wa kipa Mseja uliiwezesha Yanga kupata mabao yake yaliyofungwa na mabeki Vincent Bossou, Twite na mshambuliaji Amissi Tambwe kipindi cha pili.

Twite ameweka rekodi ambayo ni adimu sana kuiona hata barani Ulaya, baada ya kuweza kurusha mpira huo na kumshinda kipa wa Mbao na kuingia nyavuni.

 Anena bado yupo yupo Tanzania

 Akizungumzia mustakabali wake, Twite amezikaribisha ofa mezani kutoka timu yoyote inayomtaka na atakuwa tayari kama watakubaliana.

Alisema alipenda kuongeza mkataba na Yanga lakini wao hawakuwa tayari kuendelea naye, hivyo anashukuru kwa yote na anaitakia mafanikio timu hiyo katika mashindano yote yajayo.

“Nipo nyumbani nimepumzika nikijipanga kwa mipango mingine nikisubiri ofa mbalimbali, niko tayari kucheza kwenye timu yoyote ambayo tutakubaliana kimasilahi hivyo klabu yoyote inayonihitaji ije tuongee,” alisema.

Twite alithibitisha kuendelea kuonekana kwenye ligi kuu itakayoanza Desemba 17 huku akitarajiwa kucheza mechi mojawapo dhidi ya Yanga.

“Subirini nimalize kusaini mkataba mpya, kila kitu kitajulikana na timu ninayokwenda. Nitaendelea kucheza hapa hapa Tanzania kwenye ligi kuu,” alisema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -