Tuesday, November 24, 2020

Tyson kula shavu Marekani ya Trump?

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NEW YORK, MAREKANI

BINGWA wa zamani wa ndondi za kulipwa duniani, Mike Tyson, Januari mwaka huu aliwahi kutabiri kuwa Donald Trump angeshinda kiti cha urais wa Marekani katika uchaguzi mkuu uliofanyika mapema mwezi huu, tofauti na wengi waliokuwa wakimpa nafasi kubwa mwanamama Hilary Clinton.

Utabiri huo wa Tyson ulionekana kama ndoto ya mchana kwani wengi waliamini mfanyabiashara huyo bilionea, asingefurukuta kwa Hilary ambaye ana uzoefu wa mambo ya uongozi, lakini pia akiwa ni mmoja wa wake wa marais wa nchi hiyo, yaani Bill Clinton.

Japo kuna watu wengine maarufu hawakuwa wakizungumza lolote kuelekea uchaguzi huo, lakini ilionekana wazi kuwa wengi walikuwa wakitamani Hilary autwae urais wa nchi hiyo kuchukua nafasi ya Barrack Obama anayemaliza kipindi chake cha miaka nane.

Kadiri siku zilivyozidi kwenda, hakukuwa na dalili zozote za Trump kuibuka kidedea katika uchaguzi huo, kwani Hilary alikuwa akifanya vema katika kura za maoni na midahalo mbalimbali.

Bila shaka, Tyson alishajiona kama anaelekea kushindwa katika ndoto zake za kumwona Trump akitangazwa kuwa Rais wa Marekani.

Kwa waliokuwa wakimnyima nafasi Trump kuwa kiongozi wa nchi hiyo, wengi wao walikuwa ni wale wenye asili ya Kiafrika ambao walikuwa wakimpinga kutokana na sera zake za wazi wazi za ubaguzi wa rangi.

Lakini tofauti na wengi walivyotarajia, kuanzia Wamarekani wenyewe hadi wale wa mataifa mengine, zaidi ikiwa ni Waafrika, Trump alimpiga mweleka Hilary wiki iliyopita na kutwaa kiti kinachoachwa na Obama.

Katika maelezo yake juu ya Trump, Tyson alisema: “Tunafanana kwa tabia, namuamini kuchukua madaraka, ana ushawishi katika nyanja yoyote ile, tunahitaji mtu wa aina hiyo na hivyo ndivyo tunavyofanana mimi na yeye.”

Bingwa huyo wa zamani uzito wa juu, alisema anamuunga mkono Trump kwa sababu alimheshimu na ni marafiki wa muda wa miaka kadhaa.

Akizungumza katika mahojiano na The Daily Caller, Tyson alisema: “Hakika mtu huyu anafaa, mimi ni mweusi kutoka mji ulio masikini kuliko yote nchini na nimepitia mengi katika maisha.

“Namfahamu na kila mara ninapokutana naye, ananisalimu kwa kunishika mikono na kuiheshimu familia yangu. Hakuna kati yao, iwe Barrack au yeyote aliyewahi kufanya hivyo. Wataendelea kuwa wao na kunipuuzia mimi na familia yangu.”

Tyson alifafanua: “Sisi ni marafiki wazuri, rejea mwaka 1986 na 1987, mapambano yangu bora kabisa yalifanyika katika kumbi za hoteli za Trump na hakuwa kiongozi wangu, lakini alinisaidia sana katika kesi zangu.”

Bondia huyo alishtakiwa kwa kubaka mwaka 1992 na alikutwa na hatia na kutumikia kifungo cha miaka mitatu.

Na sasa Trump akiwa ndiye Rais wa Marekani, ni wazi Tyson atakuwa akisubiri kwa hamu kuona iwapo kiongozi huyo atamkumbuka katika ‘ufalme’ wake wa White House, hasa kwa kipindi hiki ambacho mbabe huyo kutangaza kufilisika.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -