Wednesday, October 28, 2020

UBABAISHAJI HUU KWENYE SOKA HADI LINI?

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA SALMA MPELI

WACHEZAJI wawili wa kigeni wa Simba, Daniel Agyei na James Kotei kutoka Ghana, wameingia matatani baada ya kuelezwa kwamba wamechezeshwa katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Ndanda wakiwa hawana kibali cha kuishi na kufanya kazi nchini.

Mechi hiyo Simba walishinda mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.

Wachezaji hao waliosajiliwa na Simba katika dirisha dogo la ligi kuu lililofungwa Desemba 15 mwaka huu, inadaiwa hawakupaswa kucheza mchezo huo kutokana na uongozi wa klabu hiyo kutokamilisha baadhi ya vitu kwenye usajili wao ikiwa ni pamoja na hivyo vibali vya kazi.

Kwa mujibu wa sheria zilizopo, raia wa kigeni hawezi kuishi katika nchi yoyote tofauti na yake bila kuwapo kwa kibali cha kufanya kazi, ingawa Simba walifuata taratibu zote za uhamisho wao katika soka.

Suala hilo linaonekana kuibua maswali mengi kuliko majibu kutoka kwa wadau wa soka nchini, ambao wengi wanahitaji kujua kama Simba waliwachezesha bila kufuata sheria za nchi.

Simba waliwachezesha wachezaji hao wakijua kwamba wanahitaji kuombewa vibali ili waweze kuitumikia klabu yao, lakini hilo pengine halikufanyika.

Pengine kama lingefanyika kusingeibuka masuala mengi kuhusu wachezaji hao, ambao wamesajiliwa muda mfupi kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

Naamini kwamba Simba walikuwa na muda wa kuwaombea kibali wachezaji wao, kwani walijua mapema kwamba ratiba ya mzunguko wa pili ingeanza kwa kuwachezesha na wachezaji wapya waliosajili katika dirisha hilo.

Kama haitoshi, Simba hawakupaswa kufanya haraka kuwachezesha wachezaji hao, pasipo kufuata taratibu zao nchi kwani walikuwa bado wana muda wa kuwaombea kibali.

Ninaona hivyo kutokana na ukweli kwanza mzunguko wa pili umeanza tu wiki iliyopita na walikuwa na nafasi ya kucheza katika mechi inayofuata kama Simba walikuwa hawakamilisha mchakato wa kuwaombea vibali.

Kwa kuwa viongozi wetu wa soka wanafanya mambo kwa mazoea na ubabaishaji mwingi sana, imesababisha kuvunja hata sheria za nchi.

Viongozi wengi wa soka ni wababaishaji kwani wamekuwa ni vigumu kufuata taratibu na hilo si kwa Simba peke yake hata klabu nyingine unaweza kukuta wana matatizo yanayofanana.

Ni hivi karibuni tu wachezaji wa kigeni wa African Lyon walionekana kutokuwa na uhamisho katika klabu walizokuwa wanachezea nchini kwao, lakini Shirikisho la Soka Tanzania Bara liliwahalalisha kucheza Ligi Daraja la Kwanza msimu uliopita.

Ukiondoa sakata la wachezaji wa kigeni wa Simba, kuna madudu mengi yanayofanyika hapa nchini kwani baadhi ya viongozi wanaosimamia soka wanakosa uaminifu kwa Serikali.

Lakini kitu ambacho ninauliza ni lini ubabaishaji kwenye soka la Tanzania litamalizika? Maana leo Simba wamebainika kuwachezesha wachezaji wa kigeni bila kufuata sheria za nchi na kesho utasikia Yanga au Azam wamefuata njia ile ile ambao wenzao wamekuwa wakifanya.

Pamoja na jambo hilo halijapatiwa majibu ya kutosha kutoka kwa viongozi wa Simba na Serikali, kulikuwa na uhitaji gani wa haraka kuwatumia wachezaji hao katika mchezo mmoja ambao pengine usingeathiri harakati zao za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Huu ni ubabaishaji wa viongozi ambao walizoea kufanya vitu kwa mazoea, wakati kuna sheria za nchi ambazo wanatakiwa kufuata kabla ya TFF kuruhusu mchezaji wa kigeni kuanza kufanya kazi.

Hapa tunaona pamoja na Simba kudaiwa kwamba waliwachezesha kimakosa, lakini TFF hawawezi kukwepa katika hilo, kwani walitakiwa kufahamu Simba wamefuata hatua zote pamoja na kuwaombea kibali cha kuishi na kufanya kazi nchini na wapewa leseni.

Hilo linaonekana halikufanyika kwa upande wa TFF, udhaifu wa Simba kuwachezesha wachezaji hao linaweza kuanzia kwa shirikisho hilo la soka hapa nchini.

TFF wanaonekana kupoteza umakini wa kusimamia soka la Tanzania, hasa wanapohurusu klabu kutumia wachezaji wa kigeni bila kuweka masharti ya kuwaleta nchini bila kufuata sheria.

Pengine TFF pamoja na klabu zinazosajili wachezaji wa kigeni wangekuwa makini kuhakikisha wanawaombea mapema vibali vya kufanya kazi nchini kabla ya kupata uhamisho wao.

Katika hilo TFF wamechangia Simba na klabu nyingine ambayo haijawaombea vibali wachezaji wa kigeni kujiona wao wapo juu ya sheria za nchi.

Ni wakati sasa viongozi wa soka kuachana na ubabaishaji huu, unaonekana kwa wachezaji wa Simba kuingia nchini kinyemela bila kufuata taratibu.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -