Thursday, December 3, 2020

UBINGWA VPL SASA NI KWA KUOMBEANA MABAYA SIMBA, YANGA

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA ZAINAB IDDY,

NI Simba au Yanga? Ndilo swali lililokuwapo kwa mashabiki wengi wa soka hapa nchini na nje ya mipaka ya Tanzania katika suala zima la bingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Kwa miaka ya hivi karibuni ilizoeleka kuwaona Yanga na Azam FC wanaopigana vikumbo kulisaka taji hili la ligi, lakini msimu huu hali imekuwa tofauti baada ya Wanamsimbazi kuibuka na kuonyesha changamoto kubwa  huku Azam wao wakionyesha wazi hawana mbavu za kulinyakua kombe hilo msimu huu.

Simba imeingia kwenye mbio hizo ikiwa ni takribani misimu minne kushindwa kuonja ladha ya ubingwa wa VPL, kitu kinachotoa shauku ya kutaka kuona wanafuta kilio cha mashabiki wao msimu huu.

Wanajangwani wao mwaka huu wameonekana kujipanga vilivyo kurejea kwenye ubora wao tangu mwanzoni mwa msimu, baada ya kufanya usajili kabambe hususani kwa kusajili wachezaji damu changa wenye uchu wa mafanikio.

Awali ilionekana Simba wasingeweza kucheza soka la ushindani kutokana uwepo wa wachezaji wengi wapya na wamekutana na benchi jipya la ufundi, hivyo wangechukua muda kuungana na kufanya mambo makubwa ikiwamo kutwaa ubingwa jambo ambalo kwa sasa limekuwa kinyume.

Kucheza soka la nidhamu, kujituma na maelewano mazuri baina ya wachezaji kwa wachezaji, wachezaji na benchi la ufundi chini ya kocha Mcameron, Joseph Omog aliyekabidhiwa majukumu hayo mwanzoni mwa msimu huu pamoja na viongozi wameweza kufanya kikosi hicho kuwa moto wa kuotea mbali wawapo dimbani.

Wakati wachezaji wake wakionyesha hali ya kuhitaji kitu msimu huu, viongozi na wanachama wa timu hiyo waliongeza chachu kwa kutoa motisha pindi wanapopata ushindi wa pointi tatu au sare kwenye mchezo wowote.

Ubora wa kikosi chao umewafanya waongoze ligi hadi sasa wakiwa na pointi 54 mbele ya Yanga wenye pointi 49 na hivyo kupishana alama tano huku Wanajangwani wakiwa na mechi moja mkononi ambayo walicheza jana dhidi ya Ruvu Shooting.

YANGA

Hawa ndio mabingwa watetezi wa VPL  licha ya kupitwa na Simba kwa pointi tano kabla ya mechi yao ya jana dhidi ya Ruvu Shooting, lakini wana nafasi ya kulitetea taji lao na bado wanapewa nafasi kubwa ya kutetea msimu huu iwapo kama watashinda mechi zote na wapinzani wao kwenye mbio hizo kupoteza.

Kabla ya ligi kuanza msimu huu Yanga walikuwa wakijivunia upana wa kikosi chao pamoja na uzoefu walioupata katika michezo ya kimataifa ya klabu bingwa na Kombe la Shirikisho mwaka jana.

Mbali na hilo, ujio wa kocha Georege Lwandamina kutoka Zambia aliyevaa viatu vya Mholanzi, Hans van de Pluijm ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Ufundi wa  Yanga, kungeweza kuwafanya kikosi chao kuwa moto wa kuotea mbali jambo ambalo limeshindwa kuonekana msimu huu.

Licha ya upana wa kikosi chao lakini jambo lililokuwa linawapa mashaka mashabiki wao ni uchovu kwa wachezaji kutokana na kutopata muda wa kupumzika kwani tangu msimu wa ligi iliyopita  umalizike wao wanaendelea na michuano ya CAF kisha kukutana na ligi  ya msimu huu.

Yanga wao walikuwa na michezo nane kabla ya ule wa jana na iwapo kama watashinda yote watatimiza pointi 73 lakini wakiendelea  kuwa nyuma ya Simba wenye mechi saba na kama nao watashinda watafikisha 75.

Ubingwa wa Simba SC unasimama kwenye alama 2 endapo Yanga hatapoteza hata mechi moja lakini Yanga anaomba Simba SC apoteze mechi moja na sare kadhaa ili aweze kutetea taji lake.

Hali hiyo ipo pia kwa Simba wanaiombea Yanga ipoteze mchezo ili waweze kuwapita kwa alama nyingi na hivyo kutangaza ubingwa mapema.

Kwa hali hiyo, je, ni Simba au Yanga atakayeweza kulipata taji la Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu?

Mechi zilizobaki kwa Yanga

Yanga vs Ruvu Shooting (Imechezwa jana)

Mtibwa Sugar vs Yanga

Yanga vs Kagera Sugar

Yanga vs Azam FC

Yanga vs Mbeya City

Yanga vs Toto Africans

Yanga vs Tanzania Prisons

Mbao Fc vs Yanga

Mechi za Simba

Simba vs Mbeya City

Kagera Sugar vs Simba

Mbao FC vs Simba

Toto Africans vs Simba

Simba vs Mwadui FC

Simba vs Stand United

Simba vs African Lyon

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -