Sunday, October 25, 2020

UCHAGUZI MKUU SIMBA MO DEWJI KIULAIIINI

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA ZAITUNI KIBWANA


KAMATI ya Uchaguzi ya Simba imetangaza kuwa Novemba 3, mwaka huu ndio watafanya uchaguzi wa kuchagua viongozi wapya wa klabu hiyo.

Uchaguzi huo utahusisha wajumbe sita ambao wataingia moja kwa moja kwenye bodi ya wakurugenzi watakaoungana na wengine nane watakaoteuliwa na mfanyabiashara, Mohammed Dewji.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba, Boniface Lyamwike, alisema nafasi zinazowaniwa ni ile ya mwenyekiti pamoja na wajumbe watano ambao wataingia kwenye bodi ya klabu hiyo.

“Uchaguzi utakuwa ni wa watu sita ambapo baadaye mwenyekiti atakuwa na ruhusa ya kuongeza watu wawili ambao wataungana na wale nane wa Mo kutimiza idadi ya watu 16 watakaounda bodi ya wakurugenzi ya klabu hii,” alisema Lyamwike.

Lyamwike alizitaja sifa kuu za kugombea nafasi ya mwenyekiti ni lazima uwe na elimu ngazi ya shahada na wajumbe wanne wanatakiwa kuwa na elimu ya kidato cha nne.

“Nafasi zinazowaniwa ni sita, ambapo mwenyekiti awe na shahada ya kwanza na mjumbe mmoja kati ya watano naye anapaswa kuwa na elimu kama hiyo ya mwenyekiti.

“Wajumbe wangine wanne wanatakiwa kuwa na elimu ya kidato cha nne, lakini pia katika nafasi hizo lazima kuwapo na mwanamke na katiba ya mwaka 2018 ndiyo itatumika katika uchaguzi huu,” alisema Lyamwike.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Steven Alli, alisema zoezi la uchukuaji fomu litaanza leo kwenye makao makuu ya klabu hiyo.

“Fomu ya nafasi ya mwenyekiti ni shilingi 500,000 wakati nafasi za wajumbe ambao wanaingia moja kwa moja kwenye bodi ya wakurugenzi ni shilingi 300,000 kwa kila mgombea,” alisema Alli.

Alisema zoezi hilo la uchukuaji fomu litakamilika Septemba 11, mwaka huu ambapo baada ya hapo wagombea watarudisha fomu hizo kuanzia Septemba 11 hadi 15, mwaka huu.

Kuanzia Septemba 16 hadi 18, mwaka huu zoezi la usaili litafanyika na Septemba 21 hadi 23, mwaka huu wanachama wataruhusiwa kuwasilisha pingamizi.

Ali alisema kuwa Septemba 24 hadi 26, mwaka huu ni siku ya kupitia pingamizi na Septemba 27 hadi 29, mwaka huu kitakuwa ni kipindi cha kusikiliza pingamizi ambapo Oktoba 1, mwaka huu yatatolewa maamuzi ya pingamizi.

“Kamati yetu kuanzia Oktoba 2, mwaka huu itatangaza majina yaliyokidhi vigezo na baada ya hapo Oktoba 3 hadi Novemba 2, mwaka huu ni siku rasmi ya kuanza kampeni kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu,” alisema Alli.

Ikumbukwe Simba ilifanya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu kutoka wa uanachama hadi wa uuzaji hisa, huku mfanyabiashara, Mohammed Dewji ‘Mo’, akipata baraka zote kumiliki asilimia 49 ya hisa na zile 51 zilizobaki zikiachiwa wanachama.

 

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -