Tuesday, October 27, 2020

UCHAGUZI RIADHA KUTINGA KORTINI

Must Read

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo,...

Katwila: Sitaidharau Mbeya City

NA VICTORIA GODFREY KOCHA wa timu ya Ihefu, Zuberi Katwila, amesema hawaraidharau  Mbeya City...

NA JACKLINE LAIZER, ARUSHA

UONGOZI wa Chama cha Riadha Mkoa wa Arusha (ARAA), umejipanga kutinga mahakamani kupinga mchakato wa  uchaguzi mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) unaotarajiwa kufanyika Desemba 10, mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa mjini hapa jana na Katibu Mkuu wa ARAA, Alfredo Shahanga, alisema walikaa pamoja na uongozi mzima wa ARAA na kuangalia mwenendo wa uchaguzi wa RT na kuona ni batili.

Alisema kwa kuona hivyo tayari wamemwandikia barua Waziri mwenye dhamana katika michezo, Nape Nauye, kuulalamikia uchaguzi huo na kuupinga kwa kuwa ni batili na umekiuka katiba ya RT.

Shahanga alisema sababu za wao kuupinga uchaguzi huo na kuuita ni batili, ni Baraza la Michezo Taifa (BMT) kutangaza uchaguzi huo, kwani limevunja sheria ya sura ya 14 (C) ya katiba ya RT.

Alisema uchaguzi unaitishwa na chama chenyewe kwa kupitia bodi teule ya uchaguzi.

Alitaja sababu nyingine kuwa ni kutaka katiba mpya ambayo ni rasimu na haijapitishwa kwa kuwa ina upungufu ambao unamnyima haki mgombea, kwani kuna vifungu vinasema mgombea wa urais katika uongozi wa RT lazima awe na shahada.

Alisema na haijafafanua kuwa awe na shahada gani kama ni ya michezo au yeyote ile, kwani wanaona ni jinsi wanavyoilazimisha kutumika ili iendelee kuwalinda kwa manufaa yao na si ya chama.

Shahanga alisema watakwenda mahakamani iwapo hawatasikilizwa malalamiko yao kwa lengo la kutafuta haki.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...

Katwila: Sitaidharau Mbeya City

NA VICTORIA GODFREY KOCHA wa timu ya Ihefu, Zuberi Katwila, amesema hawaraidharau  Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu...

Kocha apokea kipigo kwa shingo upande

 NA  VICTORIA GODFREY KOCHA wa timu ya Mwadui, Khalid Adam, amesema amesikitishwa na kipigo cha mabao 6-1 kutoka kwa...

KMC kumaliza hasira kwa Gwambina

NA WINFRIDA MTOI BAADA ya kuchezea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Yanga, kocha msaidizi wa timu ya Manispaa...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -