Saturday, November 28, 2020

UGANDA IMETUONYESHA UGUMU WA SAFARI YA YAOUNDÉ

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

MWAKA 1978 ndio mwaka ambao timu ya taifa ya Uganda, Uganda Cranes, walishiriki mara ya mwisho michuano ya Afcon. Ndio 1978!! Mwaka ambao walikuwa chini ya utawala wa Dikteta Idi Amin. Wakati huo hakuna hata mchezaji mmoja wa timu ya Taifa ya Uganda ya sasa alikuwa amezaliwa.

Miaka 39 imepita sasa Uganda wamepata nafasi ya kushiriki kwa mara nyingine tena michuano ya Afcon inayopigwa katika ardhi ya Gabon.

Kwa sasa ni ngumu kuamini kama wataweza kuvuka kwenda robo fainali kwa sababu kundi alilopangwa ni gumu mno. Ghana, Misri na Mali hao wote wanamwangalia Uganda kama daraja la kuvuka kwenda hatua inayofuata.

Ni ngumu hata kichaa kuwapa nafasi Uganda kuvuka hatua inayofuata, lakini kichaa huyo huyo anaweza kuwa na akili ya kuamini kile wanachokipata Uganda sasa kuwa ni silaha yao ya baadaye itayakayowafanya kuvuka kwenda Yaounde, Cameroon, 2019.

Haikuwa rahisi kwao kufika walipo sasa. Mipango ya safari yao ilipangwa na ikapangika kweli kweli. Sioni safari yao kama itafika mwisho hivi karibuni.

Msingi wa safari yao ulianzia katika kuwekeza nguvu kwa vijana. Mkakati uliofuata ni kuwapatia nafasi ya kuonyesha ujuzi wao. Kisha wakapanga mipango ya kuuza vijana wao nje ya mipaka yao.

Hapa kwenye biashara ya kuuza ndio ilipotupiga chenga Watanzania. Mafanikio ya Uganda hayatoki ndani ya Uganda. Yanatoka nje ambako wachezaji wao wanajenga vinasaba vya kuwa na uzoefu zaidi.

Kikosi chao cha sasa pekee kina  wachezaji waliochaguliwa kutoka ligi tisa tofauti hapa duniani. Haya ndio mafanikio sasa ambayo walianza kuyajenga miaka kadhaa nyuma.

Kingine ambacho Uganda wanakifanya ni kujifunza kutoka kwa timu kubwa za Afrika au nje ambazo wamekuwa wakicheza nazo katika kuwania nafasi au michezo ya kirafiki.

Miaka ya karibuni wamefanikiwa kucheza dhidi ya Ghana mara kadhaa. Katika kuwania kufuzu kushiriki Afcon walikuwa dhidi ya Burkina Faso, Botswana na Comoro.

Juzi bila shaka dunia ilibaki mdomo wazi kuona Uganda wanacheza na kumiliki dhidi ya Ghana iliyosheheni mastaa. Unadhani walibahatisha walichofanya? Hapana, kile  nistahili yao na ndiyo Uganda wapya hao kwenye soka la Afrika na duniani.

Wanasema ukitaka kuwa mamba jifunze kutoka kwa mamba mwenyewe. Uganda walishajifunza jinsi ya kucheza na Ghana, Ivory Coast na hata Misri. Wamejifunza kwa wakubwa na wao wana wachezaji nje ya nchi kama ilivyo Ghana, Misri na vigogo wengine. Japo bado hawajaonekana kama ni tishio, lakini wanakuja kuwa tishio.

Sioni wakipotea tena kuanzia sasa, zaidi ya hapo safari yao itawapeleka nchi ya ahadi ambayo wamepanga kufika, pengine si mwaka huu au katika michuano hii, lakini safari yao inaelekea kuzuri miaka kadhaa ijayo.

Ameshacheza na Ghana kwenye mashindano ya kuwania nafasi ya kufuzu Kombe la Dunia. Matokeo yalikuwa sare ya bila kufungana. Bado ana mchezo dhidi ya Misri katika kuwania tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia. Kumbuka hapo yupo kwenye kundi la kifo ambalo lina Ghana, Misri na Congo kwenye safari ya kuelekea Urusi.

Ukanda wa Cecafa wanajivunia kuwa na Uganda lakini bado mmoja hatoshi kubeba nchi zaidi ya tano. Nini kifanyike kuwasaidia wengine kuelekea wanakoenda Uganda?

Mipango na dhamira chanya zinaweza kutufikisha Cecafa tunakotaka kufika. Uganda wawe mfano kwa wengine kujituma na kujifunza.

Nafasi ya kufuzu Afcon ijayo anayo. Ndio ni uhakika kwa asilimia 100 sababu kundi alilopangwa sioni wa kumsumbua labda Cape Verde ambaye anaonekana kama mkubwa kwake.

Kundi hilo tumo Tanzania ambao hatuna kocha mkuu hadi hivi sasa, Lesotho ambao bado si wa kutisha lakini wanaweza kutoa changamoto. Pia kuna Cape Verde aliyewahi kuwa kibonde wa Tanzania, lakini sasa ni moja ya timu zinazoogopeka Afrika.

Kwa Watanzania wengi wanajipa matumaini ya kuvuka kwenye kundi hilo kuelekea fainali za Yaounde, 2019, lakini kwa kiwango kilichoonekana jana kwa Uganda ni wazi kwamba tuna kazi kubwa tena kubwa sana.

Tusiwaangalie Uganda kwa jicho la jirani zetu, hii itatuumiza vibaya sana, tusiwabeze kwa sababu wachezaji wao wanakuja kucheza hapa kwetu. Hawa jamaa wametuonyesha kwamba safari yetu ya kwenda Yaounde mwaka 2019 ni ngumu sana na inahitaji maandalizi ya uhakika.

Safari yake kwenye kundi la sasa Afcon ni finyu lakini bado wanaweza kutuonyesha hawakufuzu kwenda Gabon kwa bahati. Nendeni Uganda, sisi Tanzania tulishagawana timu za kushangilia Afcon hata kabla hatujaona kiwango chenu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -