Friday, October 30, 2020

UHAI WA RAMOS HATARINI KISA MO SALAH

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

LONDON, England


 

NAHODHA wa Real Madrid, Sergio Ramos, amethibitisha kuwa yeye na familia yake walikabiliwa na vitisho vya kuuawa kufuatia rafu aliyomchezea winga wa Liverpool, Mohamed Salah kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita.

Ikiwa ni miezi minne tangu Ramos asababishe Salah adumu uwanjani kwa dakika 30 tu kabla ya kutoka nje ya uwanja akiugulia maumivu ya bega, juzi katika mchezo wa kirafiki kati ya taifa lake la Hispania na England, beki huyo alizomewa mno na mashabiki wa timu pinzani.

England iliikaribisha Hispania katika Uwanja wa Wembley, lakini ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1, huku Ramos akikabiliwa na wakati mgumu dhidi ya mashabiki hao.

Hata hivyo, Ramos alisema hajali kuhusu vitendo hivyo kwani anaamini hadi leo kuwa hakudhamiria kumuumiza Salah na hajioni kuwa ni ‘mtuhumiwa’.

Aidha, Ramos alisema mapokezi hayo ya mashabiki wa England ni madogo, kwani baada ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, yeye na familia yake walipokea vitisho vya kuuawa.

“Nilitishiwa kifo mimi na familia yangu. Watu wanakumbuka kilichotokea fainali lakini hawataki kufikiria jinsi gani maisha yangu yalivyokuwa hatarini kwa tukio ambalo sikudhamiria kulifanya,” alisema Ramos.

“Nadhani wanahisi labda kilichonitokea ni utani na ndio maana walikuwa wakinizomea. Nilishasema tangu awali, sitarudia tena. Sikudhamiria kumuumiza Salah.

“Kuna watu nadhani pia hawakunielewa. Si mbaya, ndivyo soka lilivyo. Sitatetereka kamwe, iwe uwanjani au maisha yangu binafsi,” alisema Ramos.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -