Tuesday, December 1, 2020

UKIACHANA NA USHINDI WA MAN CITY KULIKUWA NA MAMBO MATAMU ETIHAD

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

MACHESTER, England

MECHI kati ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya mtoano iliyomalizika kwa Manchester City kushinda mabao 5-3 dhidi ya Monaco, ilikuwa ya aina yake.

Mashabiki waliohudhuria mechi hiyo iliyopigwa juzi Jumanne kwenye Uwanja wa Etihad walibaki midomo wazi, baada ya kumwona Radamel Falcao akirejea Jiji la Manchester kivingine.

Ukiachana na mchezaji wa zamani wa Manchester United, Falcao kurejea Manchester akiwa mwiba na ushindi wa Man City ambao waliupata baada ya kutoka nyuma kwa mabao 2-1, kulikuwa na mambo mengine matamu.

  • Aguero kupata nafasi

Bao lake la kwanza linaweza likawa ni zawadi kutoka kwa mlinda mlango wa Monaco, Danijel Subasic, lakini Sergio Aguero, ana kila sababu ya kujivunia.

Nyota huyo wa Argentina alikuwa na hofu kutokana na kucheza mechi sita bila ya kufunga na kukosa nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza kufuatia kuwasili kwa Gabriel Jesus, amerejea kwenye kikosi hicho baada ya mshambuliaji huyo wa Brazil kupata majeruhi.

Katika Ligi ya Mabingwa Ulaya amecheza dakika 522 bila ya kufunga, baada ya bao hilo la kwanza alifunga lingine.

  • Mbappe ametisha

Akiwa na kasi ya ajabu, nguvu, uwezo wa kupiga miguu yote miwili na huku akifukuziwa na Arsenal chipukizi Kylian Mbappe, ameanza kufananishwa na mshambuliaji wa zamani wa Ufaransa, Thierry Henry.

Ni mchezaji wa tatu wa Ufaransa kufunga bao Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na umri wa miaka 18, baada ya kufunga bao la pili dhidi ya Man City na alikuwa akishangiliwa uwanjani kila alipokuwa akikokota mpira kuelekea langoni mwa City.

Alipohamia upande wa kushoto na kukaa kulia kwa Radamel Falcao katika kipindi cha kwanza, alimsumbua sana Nicolas Otamendi, ambapo aliwafungasha virago mabeki na kufunga bao hilo la pili.

3) Mashabiki wasusa

Kulikuwa na siti tupu kibao kwenye uwanja huo wa Etihad wakati mchezo unaanza, hiyo inatokana na mashabiki wa Man City kutokuvutiwa na Ligi ya Mabingwa. Kutokana na kawaida yao hata pamoja na ujio wa Pep Guardiola, ambapo mashabiki waliokuwapo walizomea wimbo wa Uefa. Lakini mashabiki wengi walioonekana kuwa nje ya uwanja walianza kuingia taratibu, lakini bado City wanahitaji kufanya kitu kwa mashabiki wao.

  • Falcao karejea Manchester

Ilisikitisha sana kwa Radamel Falcao kushindwa kutakata katika misimu yake miwili ya mkopo Ligi Kuu England, alianza Manchester United, ambapo alifunga mabao manne katika mechi zake 29, kisha alihamia Chelsea, alikokuwa na hali mbaya zaidi kwa kufunga mabao 12. Majeruhi yake yalimkosesha nyota huyo wa Colombia fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil, lakini tangu amerejea Monaco ameonekana kuwa mpya na kufunga mabao 22 msimu huu, yakiwemo mabao yake mawili kwenye Uwanja wa Etihad.

Moja ya bao lake kali ni lile aliloinua mpira juu ya kipa wa Man City kwenye eneo la hatari huku mabeki wawili wakiwa upande wake wa kulia na kushoto, ingawa baadaye alikosa penalti.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -