Monday, November 23, 2020

UKIBUGI HAPA IMEKULA KWAKO NNE BORA EPL?

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LONDON, England

TIMU za Chelsea na Tottenham ndizo zinazochuana vikali kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, huku zikiviacha vigogo vingine vinne vikiwania nafasi mbili zilizobaki katika kinyang’anyiro hicho ili ziweze kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Ukiachana na vigogo hao, Liverpool wao ndio kwa sasa wanashika nafasi ya tatu, lakini timu nyingine zina mechi kibindoni ikilinganishwa na wao.

Kutokana na hali hiyo, katika Makala haya BINGWA itajaribu kuangalia jinsi vita ilivyo ili kubaini nani anaweza kutinga hatua hiyo ya Ligi ya Mabingwa na yupi anaweza kuteleza.

 

1.Liverpool – imecheza mechi 31 ina pointi 60.

Mechi ilizobaki nazo

Aprili 8, 2017 vs Stoke (ugenini)

Aprili 16, 2017 vs West Brom (ugenini)

Aprili 23, 2017 vs Crystal Palace (nyumbani)

Mei mosi, 2017 Watford (ugenini)

Mei 7, 2017 vs Southampton (nyumbani)

Mei 13, 2017 vs West Ham (ugenini)

Mei 21, 2017 Middlesbrough (nyumbani)

Jambo ambalo lilikuwa limempa unafuu wiki hii Kocha Jurgen Klopp ni kushinda mtanange dhidi ya Everton, maarufu kama Merseyside na huku washindani wake watatu wakipoteza pointi.

Hata hivyo, alijikuta akimpoteza nyota wake, Sadio Mane, kutokana na kuwa majeruhi na hivyo kukosekana kwake katika mechi zilizobaki msimu huu linaweza kuwa pigo kubwa kwa kiwango cha timu hiyo.

Hali hiyo ilidhihirisha Jumatano, wakati ilipojikuta ikiwa nyumba dhidi ya Bournemouth na huku ikijikuta ikihitaji dakika za mwisho ili iweze kuambulia sare.

Hii ni mara ya pili msimu huu Liverpool kupoteza pointi dhidi ya Bournemouth.

Mbali na hilo, licha ya kuwa bado ipo katika vita hiyo, lakini nafasi yake ni finyu kutokana na kwamba timu za Arsenal, Man City na Man United zinaweza kuipita kutokana na mechi zilizonazo mkononi.

*Uwezekano wa kufuzu michuano hiyo ni: 3/5

2.Manchester City –Mechi ilizocheza 30, ina pointi 58

Mechi ilizobaki nazo

Aprili 8, 2017 vs Hull (nyumbani)

Aprili 14, 2017 vs Southampton (ugenini)

Aprili 27, 2017 vs Manchester United (nyumbani)

Aprili 30, 2017 vs Middlesbrough (ugenini)

Mei 6, 2017 vs Crystal Palace (nyumbani)

Mei 13, 2017 vs Leicester (nyumbani)

Mei 21, 2017 vs Watford (ugenini)

Licha ya kuonesha kiwango kizuri, lakini mabao manne iliyoruhusu na pointi moja iliyoivuna wiki hii haikuwa safari nzuri kwa vijana hao wa Pep Guardiola katika safari yao ya jijini London katika kipindi cha siku nne zilizopita.

Hata hivyo, endapo wataweza kushinda mechi yao waliyonayo mkononi, wataweza kuipiku Liverpool na kushika nafasi ya tatu na hivyo kuwa rahisi kwao kutinga hatua hiyo ya nne bora.

Nafasi nyingine ambayo timu hiyo inaweza kuitumia ni ile ambayo watakutana na Manchester United kutokana na kuwa watakuwa nyumbani na kama watacheza kama walivyofanya wakati miamba hiyo ilipokutana katika mechi ya kwanza iliyopigwa katika uwanja wa Old Trafford Septemba mwaka jana na kuondoka na ushindi wa mabao 2-1, itakuwa ni faida kubwa sana kwao.

Mbali na hilo, faida nyingine ambayo wanayo ni kwamba wana mechi tano kati ya nane zilizobaki ambapo watakuwa katika uwanja wao wa Etihad.

*Uwezekano wa kufuzu michuano hiyo ni: 4/5

3.Arsenal – mechi ilizokwishacheza 29, ina pointi 54.

Zilizobaki

Aprili 10, 2017 vs Crystal Palace (ugenini)

Aprili 17, 2017 Middlesbrough (ugenini)

Aprili 26, 2017 vs Leicester (nyumbani)

Aprili 30, 2017 Tottenham (ugenini)

Mei 7, 2017 vs Manchester United (nyumbani)

Mei 13, 2017 vs Stoke (ugenini)

Mei 21, 2017 vs Everton (nyumbani)

TBC Sunderland (nyumbani)

TBC Southampton (ugenini)

Baada ya matumaini ya kutwaa ubingwa kutoweka kwa sasa, Arsenal inatakiwa kukaza buti dakika hizi za mwisho ili iweze kutinga hatua ya nne bora na kufuzu kucheza kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Ushindi ilioupata wiki hii dhidi ya West Ham na jinsi ilivyocheza dhidi ya Man City inadhihirisha kuwa huenda makali yao yamerejea.

Na endapo itashinda mechi zake mbili ilizonazo mkononi dhidi ya Liverpool na moja dhidi ya Man City, ina maana kwamba itakuwa imekata tiketi hiyo na hata wapinzani wao kutoka Anfield watashinda kila mechi.

*Uwezekano wa kufuzu hatua hiyo ni: 2.5/5

  1. Manchester United – mechi ilizokwishacheza ni 29, ina pointi 54.

*Ilizobaki nazo

Aprili 9, 2017 vs Sunderland (ugenini)

Aprili 16, 2017 vs Chelsea (nyumbani)

Aprili 23, 2017 vs Burnley (ugenini)

Aprili 27, 2017 Manchester City (ugenini)

Aprili 30, 2017 vs Swansea (nyumbani)

Mei 7, 2017 vs Arsenal (ugenini)

Mei 13, 2017 vs Tottenham (ugenini)

Mei 21, 2017 Crystal Palace (nyumbani)

TBC Southampton (ugenini)

Kikosi hicho ambacho ni cha gharama katika michuano ya Ligi Kuu England, wiki hii kimejikuta kikirejea katika nafasi yake ya siku zote ambayo ni ya sita.

Hata hivyo, kocha wake, Jose Mourinho, anamlaumu mwamuzi, Luke Shaw kwamba ndiye aliyewasababishia kurudi nyuma katika mbio zao za kuwania nafasi ya nne bora.

Kwa sasa timu hiyo inaweza kuwa sawa na Liverpool endapo itaweza kushinda mechi zake mbili ilizonazo kibindoni, lakini kutokana na kuwa inakabiliwa na mechi ya michuano ya Ligi ya Europa na mechi tano za Ligi Kuu kabla ya msimu kumalizika na majeruhi ilionao, unaweza kuwa mlima mrefu kwao kufuzu hatua hiyo.

Mbali na mlima huo, pia mechi nne kati ya nane ilizobaki nazo inakutana na timu ambazo zipo juu yake, tofauti na wapinzani wake.

Kutokana na hali hiyo, ili waweze kupata nafasi hiyo, itawalazimu kuifunga Man City na Arsenal na endapo watateleza katika mechi hizo itawabidi kuelekeza nguvu zao katika michuano ya Ligi hiyo ya Europa kutokana na kwamba hawatakuwa na biashara katika ligi ya mabingwa.

*Uwezekano wa kufuzu hatua hiyo: 2/5

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -