Saturday, November 28, 2020

UKIFANYA HAYA HATA AWE MZURI KAMA HALLE BERRY, UTAMPATA TU-2

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

KARIBUNI wapenzi wasomaji wangu katika safu hii ya mambo ya mahusiano inayowajia kila Jumanne na Jumamosi ikilenga kujuzana hili au lile kuhusiana na suala zima la mapenzi.

Awali ya yote, nianze kutoa shukrani zangu za dhati kwa wote ambao wamekuwa wakichangia mada zangu wakiwamo wale wanaouliza maswali ambayo hata hivyo ni vigumu kumjibu mmoja mmoja.

Baada ya salamu hizo, nigeukie mada ya leo ambayo inatokana na baadhi ya maswali ya wasomaji wangu ambao wamekuwa wakitaka kufundishwa jinsi ya kutongoza wasichana.

Kama nilivyobainisha katika toleo la Jumamosi ya wiki iliyopita, kutongoza ni kitendo cha kumshawishi mtu kwa njia yoyote ili kukubaliana na matakwa yako.

Katika suala zima la mapenzi, kutongoza umekuwa ni mtihani mzito kwa baadhi ya wanaume kwani unaweza kumkuta mtu akiwa anampenda msichana fulani, lakini akitumia muda mrefu kufikiria jinsi ya kumnasa.

Wapo ambao wamekuwa wakitumia fedha ama kuwanunulia vitu vya thamani kama njia za kuwapata wasichana. Katika hilo, wapo wanaofanikiwa huku wengine wakiishia ‘kula za pua’.

Njia hiyo ya kutumia fedha au mali, inaweza kuzaa matunda kwa wasichana malimbukeni na washamba wa fedha au kitu husika. Lakini pia inaweza kuwa njia sahihi kwa wasichana ‘wadangaji’.

Lakini pia, wapo wale wanaowaeleza moja kwa moja wasichana kuwa wanawapenda na mwisho wa siku kufanikiwa kuwa nao ndani ya muda mfupi.

Ndugu msomaji, kwa msichana mwenye msimamo, anayejielewa na anayejiheshimu, kamwe huwezi kumpata kwa njia hizo hapo juu.

Wavulana au wanaume wengi wamejikuta wakigonga mwamba kwa wasichana wa aina hiyo na mwisho wa siku kujikuta wakiishia kuwakashifu kwa kila namna kisa tu wamekataliwa.

Kwa faida ya wale waliotaka kufahamu jinsi ya kuwatongoza wasichana, wafahamu kuwa kutongoza ni sanaa inayohitaji ubunifu wa hali ya juu kama ilivyo katika sanaa ya uigizaji na nyinginezo na kwamba hakuhitaji kiwango cha juu cha elimu kuwa na fedha au mali nyingi, utanashati, cheo na mengine kama hayo.

Kuna njia ambazo zinaweza kumsaidia mwanamume kumnasa kirahisi mwanamke, hata awe mrembo kama Mmarekani, Halle Berry, anayetajwa kuwa mwanadada mweusi mkali kuliko wote duniani, akiwa ni mwigizaji na mwanamitindo aliyetwaa tuzo kibao.

Katika toleo lililopita, nilitaja moja ya njia hizo ambayo ni kufahamu udhaifu wa msichana husika kuona ni vipi unaweza kutembelea udhaifu huo kumnasa.

Njia nyingine ni kuepuka kuuliza maswali yanayoweza kuzaa maswali yatakayokubana kuendelea na ‘topic’ yako.

Mathalani unapokutana na msichana kwa mara ya kwanza na kubaini kuwa unamtaka kimapenzi, kamwe usimuulize iwapo ana mpenzi kwani kwa wale wanaojielewa kama atakwambia anaye, ukiendelea kumng’ang’ania anaweza kukuuliza swali litakalokuacha midomo wazi au kumpa pointi kwa kufahamu uwezo wako wa kuelewa au tabia yako.

Yupo rafiki yangu mmoja alikutana na msichana aliyemtaka kimapenzi, badala ya kujinadi, alianza kwa kumuuliza iwapo ana mpenzi, yule msichana akajibu ni kweli anaye mpenzi wake.

Yule rafiki yangu alipojibiwa hivyo, aliendelea kumng’ang’ania yule msichana ambapo aliulizwa: “Unanifanya mimi malaya ehee, nimekwambia nina mpenzi wangu halafu bado unaning’ang’ania. Inaonekana wewe ni kiwembe usiyepitwa na kitu, ingekuwa mimi ndio mpenzi wako ungefurahi kusikia ninatembea na mwanamume mwingine?”

Kauli hiyo ya yule msichana ilimwacha hoi na kubaki aking’atang’ata maneno kwa aibu.

Lakini mwisho wa siku kosa lake kubwa ni kuuliza swali la kijinga lisilo na mantiki. Unapokutana na mwanamke ukimpenda, hata siku moja usipende kujua mahusiano yake mengine kama kweli umempenda, tumia njia zozote zilizopo ndani ya uwezo wako kumshawishi ili akuone wewe ndiye mtu sahihi kwake.

Njia nyingine inayoweza kumsaidia mwanamume kumnasa msichana au mwanamke wa aina yoyote ni utulivu.

Utulivu ninaouzungumzia hapa ni katika mazungumzo ambayo yatakusaidia kutokukurupuka kujibu maswali kadha wa kadha utakayoulizwa, kujieleza kwa ufanisi, kujenga hoja wakati wa majadiliano ya mambo mbalimbali, lakini pia kukabiliana na changamoto mbalimbali, hasa unapokutana naye akiwa na rafiki zake.

Wanaume wengi wamejikuta wakigonga mwamba kwa wanawake kutokana na papara zao katika mazungumzo ambapo hujikuta wakitoa maelezo mengi kuhusiana na maisha yao hata bila kuulizwa.

Unaweza kumkuta mwanamume akijianika kupita kiasi ambapo ndani ya muda mfupi, msichana au mwanamke anajikuta akifahamu mambo mengi yanayomhusu hata yale ambayo hakupaswa kufahamu.

Kwa mwanamke anayejielewa, hawezi kukubali kuwa na uhusiano na mwanamume kama huyo ambaye ni mwepesi wa kuyaweka wazi maisha au mipango yake akiamini ipo siku anaweza kuwasimulia rafiki zake mambo anayofanya na mwenza wake.

Ndugu msomaji, kwa leo hebu tuishie hapo, tukutane Jumamosi ambapo tutaendelea na mada hii kwa faida ya wale walioomba kusaidiwa katika hilo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -