Wednesday, November 25, 2020

UKIFANYA HIVI UTATUNZA FURAHA YAKO

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

MMOJA wa marafiki zangu aliwahi kuniambia kuwa yeye na mkewe huwa wanaanza siku mpya wakiwa na kila kitu kipya. Mwanzo sikumwelewa.

Ila baada ya kumsikiliza kwa makini nikajua nini alikuwa anamaanisha. Alichomaanisha ni kile ambacho kitaalamu tunakiita ‘live day tight compartment.’

Yaani kila siku inabidi uishi kwa kuitazama siku kwa namna yake. Yale ya jana yawe ya jana na ya leo yahusike na leo.

Kitaalamu ni ujinga kulia kwa sababu ya maumivu ya jana, ila inafaa kucheka na kusherehekea furaha yako ya leo. Yaani upate kitu na uhisi madhara au furaha ya kitu husika katika siku ilipotokea. Si unaumizwa jana unalia mpaka leo. Haifai!

Ili ujitengenezee mazingira ya amani na furaha zaidi, ya jana usiyape nafasi katika maisha yako. Leo ndiyo kuna kila kitu kwako. Tayari ulishamaliza siku ya jana na mambo yake, sasa yaweke kando.

Yakuchukua ni yale tu yenye faida katika nafsi yako kwa sababu ndiyo yenye uwezo wa kuiboresha zaidi siku yako ya leo. Uchukuaji wa mambo mabaya ya jana, hutengeneza ubaya wa siku ya leo.

“Kaka, mimi na mke wangu tuko katika maisha ya furaha sana kwa kipini kirefu. Kila siku ni siku ya furaha katika nyumba yetu.

“Mwanzo kutokana na wote kuoana vijana, wengi walidhani ndoa yetu haitafika mbali. Ila imekuwa tofauti. Sasa nipo katika ndoa kwa zaidi ya miaka nane na bado kila siku katika maisha yangu ni njema. Tuna amani na furaha sana!

“Mimi na mke wangu si kwamba hatukorofishani, hapana. Tunakorofishana sana na tena kuna nyakati ugomvi kati yetu huwa mkubwa sana wewe ni shahidi (mara nyingi huwa wananitumia katika gomvi zao). Ila mimi na mke wangu huwa hatulali na ugomvi,” akaendelea!

“Kama tumekoseana hujitahidi kwa kila hali kurekebisha makosa ya leo na kuombana msamaha leo leo. Na uzuri ni kwamba kati yetu hakuna mjuaji. Kama akinikosea yeye hujirudi huniomba msamaha na pia kama nikimkosea mimi, pia namwomba msamaha mara moja.”

Japo alinieleza mengi ila tuishie hapa!

Matatizo yako na mpenzi wako huwa yanafikia wapi? Huwa unaacha mpaka kesho au unapuuzia? Kama kweli unahitaji furaha kamili ya mahusiano yako inabidi uwe na mtindo tofauti wa maisha.

Gomvi zako na mume/mke wako, inabidi zipewe nafasi za pekee na mbinu mwafaka za kuzimaliza. Hakikisha kila siku kunapozuka kutoelewana na mwenzako, unamaliza hali hiyo kabla haijaingia siku ya pili.

Siku nyingine inabidi ikukuteni katika hali ya furaha na upya wa mawazo. Kitaalamu unapotatua tatizo lako mapema unajitengenezea nafasi ya kuwa na furaha na amani zaidi katika uhusiano wako.

Tathmini zinaonesha kila unapochelewa kutatua tatizo na mpenzi wako ndipo hatari ya kukufikiria vibaya zaidi humnyemelea na matokeo yake unakuta mahusiano yanaanza kupoteza ladha na thamani.

Kumbuka furaha yako kwanza inajengwa na maamuzi na matendo yako. Kama umemkosea kwanini usiwahi kumwomba msamaha ili myamalize? Kama ukimkosea na kisha kupuuzia kumwomba msamaha, jua unapata tafsiri tofauti katika akili yake.

Kwanza anakuona kama mtu usiyejali wala kuthamini uwepo wake na hisia zake za kimapenzi. Na kwa matokeo ya fikra hizi ni kwamba, anaweza kuanza kufikiria hitimisho la mapenzi yenu.

Pili, atakuwa anakufikiria na kufikiria makosa mengine uliyomfanyia. Kwa sababu hiyo utakuwa unazidi kuweka sumu katika nafsi yake na matokeo yake anakuona kama mtu usiye na stahiki katika moyo wake.

Maliza kila tatizo linalozuka baina yenu mara moja. Omba msamaha, tumia kila mbinu kumfanya akusamehe.

Ni suala dogo kusamehewa, ila lina thamani sana katika kuweka mahusiano yako katika hali ya usalama na bora zaidi.

ramadhanimasenga@yahoo.com

Ushauri ni kwa malipo!

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -