Friday, December 4, 2020

UKITELEZA KWISHNEI

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA ASHA KIGUNDULA
MIAMBA ya soka nchini, Simba na Yanga, leo wana vibarua vigumu vya kusaka pointi zote tatu katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara ili kuzidi kuifukuzia Azam iliyopo kileleni mwa msimamo wa kipute hicho.

Kutokana na kasi ya Azam, ni wazi kuwa timu yoyote itakayoteleza leo kati ya Simba na Yanga na kupoteza pointi, itaweza kujikuta ikiishia kunawa katika mbio za ubingwa wa ligi hiyo.

Hali hiyo inatokana na ukweli kwamba kasi ya Azam si ya kitoto kwani hadi sasa haijapoteza mchezo wowote wa ligi hiyo, ikishinda yote saba, hivyo kuendelea kukalia usukani wakiwa na pointi zao 21.

Simba inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 13 baada ya kucheza mechi tano, sawa na Yanga iliyopo nyuma yao, Wekundu wa Msimbazi hao wakiwa juu kutokana na kuwa na idadi kubwa ya mabao ya kufunga.

Kwa upande wa mabao ya kufungwa, Yanga ndiyo timu pekee iliyoruhusu nyavu zake kutikishwa mara chache zaidi.

Wakati Azam ikiwa imefungwa mabao mawili sawa na Simba, Yanga nyavu zao zimetikishwa mara moja tu.

Ukiachana na hayo, kilichopo akilini mwa wapenzi, wachezaji na viongozi wa Simba na Yanga kuelekea mechi zao za leo, ni kupata ushindi tu na si vinginevyo.

Kutokana na mwenendo wa timu zote hizo tatu za juu, iwapo Simba au Yanga itapoteza leo, ni wazi itakuwa imetoa mwanya kwa wapinzani wake kuzidi kuchanja mbuga katika ligi hiyo.

Kwa kufahamu hilo, Simba wameapa kupigana kufa au kupona ili kuvuna pointi zote tatu watakapoikabili Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Mandela, mjini Sumbawanga, Rukwa kama ilivyo kwa Yanga watakaoikaribisha Polisi Tanzania, Dimba la Uhuru, Dar es Salaam.

Kikosi cha Yanga kinashuka uwanjani kikiwa na kocha mpya kutoka Burundi, Cedric Kaze, kikihitaji pointi tatu muhimu ili kiweze kuendelea na harakati zake za kuusaka ubingwa wa msimu huu wa 2020/21.

Yanga ipo kambini Kimbiji, nje kidogo ya jijini la Dar es Salaam, huku Kaze akiwataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanjani kushuhudia soka tofauti na walilozoea.

Yanga ikiwa na nyota mbalimbali kama Michael Sarpong, Yacouba Songne, Wazir Junior, Ditram Nçhimbi, Feisal Salum ‘Fei Toto’, Haruna Niyonzima, Mukoko Tonombe, Deus Kaseke, Farid Mussa, Tuisila Kisinda, Carlos Carlinhos na wengineo, wataingia uwanjani wakiwa na lengo moja tu, kuzoa pointi zote tatu dhidi ya Polisi Tanzania.

Yanga wanaingia kwenye Dimba la Uhuru wakiwa na kumbukumbu ya kushinda mchezo wao uliopita kwa kuifunga Coastal Union mabao 3-0, wakati wageni wao Polisi Tanzania, wakitoka kugawana pointi na Gwambina kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.

Akizungumzia mchezo wao huo, Kaze alisema licha ya ugeni alionao Tanzania, anahitaji kupata pointi tatu katika mchezo wa leo.

“Nina timu nzuri ya ushindi, nahitaji pointi tatu muhimu za mchezo huu na nyingine zinazofuata, kikosi changu kipo sawa, kina ari kubwa sana ya kimchezo,” alisema kocha huyo.

Polisi Tanzania chini ya kocha, Malale Hamsini, inategemea wachezaji wao Tariq Seif, Maulid Hassan, George Mpole, Marcel Kaheza na wengineo ambao wamekuwa wakitoa mchango mkubwa kwa timu yao.

Wakiwa wamecheza mechi sita, wameshinda tatu, kufungwa moja na kutoka sare miwili na kufungwa moja, hivyo kufikisha pointi 11. Simba chini ya kocha wao, Sven Vandenbroeck, wanaingia uwanjani wakihitaji pointi tatu ili kutwaa ubingwa kwa mara ya nne mfululizo. Katika mchezo wao wa leo, Simba itawakosa nyota wake watatu tegemeo, Pascal Wawa, Meddie Kagere na Clatous Chama ambao hawajaambatana na kikosi mjini Sumbawanga, huku jahazi likibaki mikononi mwa Chris Mugalu, Rally Bwalya, Luis Miquissone, Bernard Morrison, Francis Kahata, Ibrahim Ajib, Muzamiru Yassin na wengineo. Prisons chini ya kocha Salum Mayanga, wanaingia uwanjani wakitaka kuendelewa rekodi yao ya kutofungwa na Simba, iwe ni nyumbani au ugenini. Pamoja na hayo, Sven ameliambia BINGWA kuwa anahitaji pointi tatu muhimu licha ya kutambua haitakuwa kazi nyepesi kutokana na upinzani mkali walionao Prisons. Alisema Prisons wana timu nzuri ambayo ina uwezo wa kupambana na kupata matokeo kama wanayotaka wao, hivyo kwake anahitaji kuendeleaa rekodi ya kukusanya pointi na mabao mengi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -