Tuesday, December 1, 2020

KWA EPL HII UKIZUBAA TU IMEKULA KWAKO!

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA ABDUL KHALID, TSJ


HIVYO ndivyo unavyoweza kusema kutokana na ushindani uliopo kwa sasa katika Ligi Kuu ya Uingereza maarufu kama ‘EPL’ katika mbio za kuelekea ubingwa, ambapo kila timu inaombea mwenzake apoteze mchezo ili aweze kumfikia ama kumpita katika mbio za kunyang’anyia ubingwa wa ligi hiyo pendwa zaidi ulimwenguni.

Hadi hivi sasa timu zote tayari zimeshacheza michezo 19, ambayo imekamilisha ule mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo ambao umetupa taswira kwa kiasi fulani ingawa wachambuzi wa soka wanadai ligi hiyo bado ni ngumu kutokana na kila timu kutokata tamaa ya kusaka matokeo kwenye michezo yake.

6. Manchester United

Mashetani hawa wekundu wamefikisha idadi ya pointi 36, ambazo zinawafanya washike nafasi ya sita katika Ligi Kuu ya EPL ikiwa tayari imeshacheza michezo 19, ikishinda michezo 10, sare sita, huku ikiwa imeambulia kipigo michezo mitatu.
Kikosi hicho kinachonolewa na kocha mwenye maneno mengi, Jose Mourinho, kimeachwa kwa jumla ya pointi 13 na vinara wa ligi hiyo Chelsea ambao wameonesha dhamira ya kulitaka kombe hilo la EPL msimu huu.
United bado wapo kwenye mbio za ubingwa baada ya kuamka na kushinda michezo yote mitano iliyopita kwenye ligi hiyo na kuongeza ushindani zaidi kwenye kinyang’anyiro cha ubingwa msimu huu.

5. Manchester City

Wapo nafasi ya tano katika msimamo wa ligi wakiwa wamefikisha pointi 39, huku wakiwa wametofautiana na mahasimu wao kwa idadi ya pointi tatu.
Licha ya kuanza vema msimu huu kwa kupata matokeo mazuri, kikosi cha kocha Pep Gurdiola, kimeonekana kupoteza ile kasi yake iliyokuwa ikizisumbua timu nyingi mwanzoni mwa msimu huu ikiwamo watani wao wa jadi, Manchester United inayonolewa na hasimu wake Mourinho.
Katika michezo mitano iliyopita City wamefanikiwa kushinda michezo mitatu huku wakiwa wamefungwa michezo miwili dhidi ya vinara Chelsea na ule wa juzi dhidi ya ‘majogoo wa London’ Liverpool.
Pep amekiri kuwa EPL ni ligi ngumu na timu yake bado hawajakata tamaa katika kinyang’anyiro cha ubingwa msimu huu.

4. Tottenham

Kikosi hiki cha kocha Mauricio Pochettino, kinakamata nafasi ya nne katika orodha ya msimamo wa ligi ya EPL kikiwa kimejikusanyia idadi ya pionti 39, sawa na Man City baada ya kushinda michezo 11, sare sita na huku ikiwa imepoteza michezo miwili tu.
Mifumo anayotumia kocha wao Pochettino imekuwa ikiwasaidia kupata matokeo chanya katika mechi zao nyingi jambo linalowafanya nao wawepo kwenye orodha ya klabu zinazowania ubingwa wa EPL msimu huu.
Katika michezo mitano iliyopita vijana hao wa Pochettino wamepoteza mchezo mmoja tu dhidi ya Man United mchezo uliopigwa katika dimba la Old Trafford na kuamuliwa kwa bao pekee la Mikhitaryan.

3. Arsenal

Kama tulivyozoea kuwaona vijana hawa wa kocha Arsene Wenger kuwamo kwenye ile vita ya kuwania ubingwa, licha ya kutobahatika kuunyakua ubingwa huo kwa takribani miaka 16 sasa.
Msimu huu wamekuwa na kiwango bora kulinganisha na misimu kadhaa iliyopita ambapo wamekuwa wakipata msaada mkubwa kutoka kwa wachezaji wao Alexis Sanchez pamoja na Mesut Ozil, ambao wapo kwenye viwango bora msimu huu.
Hadi hivi sasa washika bunduki hao wamefikisha idadi ya pointi 40, wakizidiwa na vinara Chelsea kwa pointi tisa baada ya kushinda michezo 12, sare nne huku wakiambulia vipacho mara tatu.

2. Liverpool

Kikosi chao kimeimarika sana msimu huu ambapo wameweza kutembeza vichapo kwa vigogo wenzao wanaowania ubingwa wa EPL zikiwamo timu za Chelsea pamoja na Man City.
Naweza kusema kocha Jurgen Klopp amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuirudisha ile Liverpool iliyokuwa ikisifika kuwa ni timu hatari zaidi kwenye miaka ya 2006.
Wanakamata nafasi ya pili wakiwa na pointi 43, wakiwa wamezidiwa pointi sita tu na vinara Chelsea huku takwimu zao zikiwa nzuri baada ya kushinda michezo minne huku wakitoka suluhu mchezo mmoja katika michezo mitano iliyopita.
Kasi na uimara wa kikosi chao umemfanya kocha wa Man City, Pep Guardiola, kusema kuwa ni miongoni mwa vikosi bora zaidi alivyowahi kukutana navyo akiwa kama kocha.

1. Chelsea

Hawa ndio wanaotuongozea msimamo wa ligi ya EPL wakiwa wamejizolea jumla ya pointi 49, hadi hivi sasa baada ya kushinda michezo 16, sare mchezo mmoja huku wakiwa wamepoteza michezo miwili.
Wakiendelea na kasi hii basi hakuna shaka ubingwa wa EPL ukaenda pale Stamford Bridge msimu huu, kwani hadi hivi sasa vijana hawa wa kocha Antonio Conte wanashikilia rekodi ya kutopoteza michezo 13 katika ligi hiyo ya EPL.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -