Tuesday, November 24, 2020

UKO TAYARI KUIONA VITA YA POGBA WAWILI EUROPA?

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

MANCHESTER, England

PAUL Pogba atajikuta kwenye vita ya kuwania ushindi dhidi ya kaka yake, Florentin, pale Manchester United itakapoikaribisha Saint Etienne kwenye mchezo wa Ligi ya Europa, Alhamisi ya wiki hii.

‘The Pogbas’ watakuwa ni ndugu wawili wa kwanza kukutana Old Trafford tangu Rio na Anton Ferdinand walipokabiliana mwaka 2012.

Florentin mwenye umri wa miaka 26, alisema licha ya kwamba atafurahia mpambano wao huo, lakini upendo wake kwa mdogo wake hautapungua kamwe.

“Nitaendelea kumjali mdogo wangu. Nikiwa kama kaka yake, najua hata nikimpa presha mchezoni halitakuwa jambo baya,” alisema.

Florentin ambaye kiasili ni beki wa kati kabla ya kuhamia upande wa kushoto, alianza kuichezea klabu ya Celta Vigo ya Hispania.

Anawakubali mno Jordi Alba na Marcelo kutokana na uchezaji wao na wazazi wa vijana hao wanatarajiwa kuwa na furaha isiyoelezeka pindi watakapowaona dimbani.

Furaha yao hiyo inatarajiwa kutukumbusha mama wa watoto wawili, Granit na Thaulant Xhaka ambaye aliwapa sapoti wanawe hao kwenye mchezo wa michuano ya Mataifa ya Ulaya (Euro 2016), baina ya Uswisi na Albania.

Granit anayekipiga katika klabu ya Arsenal, ni Mswisi huku kaka yake akiwa ni Mualbania, lakini mama yao huyo hakupata shida ya kuchagua nani amshangilie na kuamua kuvaa fulana iliyochapishwa muunganiko wa bendera za nchi hizo mbili.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -