Sunday, January 17, 2021

ULIMWENGU ATUA YANGA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA ZAITUNI KIBWANA

SI siri tena kuwa Yanga wanaitaka saini ya Thomas Ulimwengu, aliyeachana na klabu yake ya TP Mazembe, lakini miamba hiyo ya Jangwani ina mtihani mkubwa wa kuonyesha jeuri ya fedha kutokana na timu nyingine zinazomsaka straika huyo wa kimataifa wa Tanzania.

Unaambiwa saini ya Ulimwengu imekuwa lulu kila kona, kuanzia Afrika Kusini, Misri hadi China, lakini bado timu ya washauri wa staa huyo inaweka ‘pozi’ kuhusiana na sehemu ya kumpeleka straika huyo kutokana na ukweli kuwa hawataki kumpoteza.

Harakati hizo za kupigana vikumbo kuwania saini ya Ulimwengu ndiyo zinazidi kuiweka Yanga kwenye wakati mgumu, lakini huwezi kuamini kwa sababu uongozi wa timu hiyo umegoma kukata tamaa na umeamua kukomaa naye hadi mwisho.

Yanga, ambao wamepania kufanya makubwa zaidi kwenye michuano ya Afrika mwakani, imepania kuimarisha kikosi chake kwa kuleta wachezaji wenye uzoefu na ubora wa kupambana kimataifa na ndiyo maana jina la Ulimwengu limekuwa gumzo sana ndani ya kambi ya timu hiyo.

Kutokana na kufahamu kuhusiana na harakati za Yanga kuisaka saini ya Ulimwengu, BINGWA liliamua kumsaka Meneja wa staa huyo, Jamal Kisongo, ili kujua ukweli halisi ni upi na kipi wao kama wasimamizi wa straika huyo wanataka kufanya.

Kisongo, ambaye pia ni meneja wa Mbwana Samatta, ameliambia BINGWA kuwa Ulimwengu alishatoka Tanzania, hivyo wakati wake kwa sasa ni kwenda mbele zaidi.

“Ulimwengu ameshatoka Tanzania, hivyo sasa tunaangalia mbele, tunahitaji changamoto mpya na si kurudi nyuma,” alisema.

Alisema  wamekataa ofa mbalimbali kutoka timu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, El Ahly ya Misri na timu kutoka China na Canada.

“Tumekuwa tukipata ofa kibao kila siku, mfano Canada, Sauth Afrika na sehemu nyingi, ila tumekataa kwa sababu tunataka tufanye maamuzi taratibu,” alisema.

Alipoulizwa dili la Yanga, Kisongo alihoji hivi Yanga ni bora kuliko Tp Mazembe? Aje Yanga ataonekana na nani, hebu tusubiri muda ukifika mtajua Ulimwengu anakwenda wapi.

Ulimwengu, ambaye yupo na kikosi cha Taifa Stars, yupo Dar es Salaam kwa sasa baada ya kumaliza mkataba wake na TP Mazembe, ambapo kwa sasa anasaka timu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -