Friday, October 30, 2020

ULINZI UCHAGUZI TOC HAUNA MFANO

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA WINFRIDA MTOI

UCHAGUZI wa Kamati ya Olimpiki Tanzania(TOC), umepanga kufanyika leo mkoani Dodoma ,huku ulinzi ukiimarishwa katika Hotel ya Dodoma utakapofanyika uchaguzi huo.

Jumla ya wagombea 23, watachuana kwenye kinyang’anyiro hicho  cha kugombea nafasi mbalimbali za uongozo wa kamati.

Akizungumza na BINGWA, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TOC, Lloyd Nchunga alisema jana uchaguzi hyuo utashuhudiwa na  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana ambaye atakuwa mgeni rasmi.

Nchunga alisema wamewasiliana na vyombo vya usalama mkoani humo,ili kiimarisha  ulinzi na kuhakikisha amani inakuwepo muda wote.

“Hadi sasa hakuna tatizo lolote wagombea na wajumbe ambao ni wapiga kura wamewasili  Dodoma na kusajiliwa. Pia vitu vyote vinavyohitajika kama karatasi za kupigia kura tumekamilisha,” alisema Nchunga.

Alisema suala kubwa wanalozingatia ni kukizi vigezo kwa wagombea na vitu vingi walishaambiwa tangu wanachukua fomu  hivyo  hawatarajii  kama wataenda kinyume na taratibu zilizowekwa.

“Taratibu za uchaguzi zinajulikana siku zote, inajulikana wazi kura ni kitu cha siri, sasa  kama mtu atakiuka hilo atajiweka  kwenye matatizo,” alisema.

Kuhusu ratiba ya uchaguzi, alisema  utaanza saa 8:00 mchana baada ya kumalizika kwa shughuli za utawala na mkutano wa wajumbe.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -