Tuesday, October 20, 2020

Uliyanasa haya mzunguko wa kwanza VPL?

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA MAREGES NYAMAKA

MZUNGUKO wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara umeacha kumbukumbu ambazo zitabaki kwenye vichwa vya wapenzi wa soka nchini, ikiwamo kitendo cha Stand United kuzichakaza Yanga na Azam, lakini pia kukiwa na ‘hat-trick’ moja pekee kutoka kwa mchezaji mzawa na rafu mbaya aliyochezewa Abasirim Chidiebere.

Lakini pia kulikuwa na matukio kadhaa ndani na nje ya uwanja ambayo kwa namna moja ama nyingine, yaliongeza msisimko wa ligi hiyo.

BINGWA limeona ni vema kuwakumbusha mashabiki wake baadhi ya matukio hayo, tukiwa katika kipindi cha mapunziko kabla ya ligi hiyo kuendelea Desemba 17, mwaka huu.

Erasto Nyoni na rekodi ya kipekee

Baada ya kukaa muda mrefu nje ya uwanja akiuguza majeraha yake ya goti, mara aliporejea uwanjani katikati ya mzunguko huo, alianza kwa kasi mechi zote zilizokuwa zimesalia, akicheza dakika zote 90, ikiwamo dhidi ya Yanga ambayo aliweka rekodi ya kuonyeshwa kadi ya njano mapema zaidi, ikiwa hivyo dakika ya sita ya mchezo iliyofanana na namba ya jezi aliyovaa.

Katika mchezo huo uliomazika kwa suluhu, beki huyo wa kushoto alionyeshwa kadi baada ya kumchezea rafu kwa mara ya tatu winga wa Yanga, Simon Msuvu.

Mavugo awa ‘bingwa wa kuotea’

Mshambuliaji wa Simba, Laudit Mavugo, ambaye alionekana kuwa na usongo wa kuchana nyavu, mara nyingi alipopewa nafasi na kocha wake, Joseph Omog, alijikuta akipigiwa kipyenga cha kuashiria kuotea.

Mrundi huyo, katika michezo minne ya mwisho, alikuwa ameotea mara 15 na kumfanya kuweka rekodi ya aina yake ambapo katika mchezo dhidi ya Mwadui FC, aliotea mara tano kabla ya kutolewa dakika ya 43 na nafasi yake kuchukuliwa na Amme Ali.

Michezo mingine aliyofanya hivyo ilikuwa kwenye Uwanja wa Kambarage mbele ya Stand United, ambapo aliotea mara nne, dhidi ya African Lyon (mara tatu), kama ilivyokuwa pale kwenye Uwanja wa Sokoine dhidi ya Tanzania Prisons.

Majimaji yaingia anga za Yanga

Majimaji ya mjini Songea, mkoani Ruvuma, baada ya kupata tu dili nono la udhamini kutoka kwa kampuni ya GSM, muda mfupi baadaye, ikaonyesha jeuri ya fedha katika mechi zake za jijini Dar es Salaam, ikiwamo kwenye maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Simba.

Katika mazoezi yao ya siku mbili kabla ya mchezo dhidi ya Simba, timu hiyo ilifanyia mazoezi yake katika uwanja wa bei mbaya vya Gymkhana, viunga vilivyozoeleka na klabu ya Yanga. Wanalizombe hao pia waliachana na kulala hoteli za ‘uswahilini’ kama ilivyozoeleka na kuhamia kwenye zile za nyota tano katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Wazungu Yanga, Azam wanasa

Makocha wa kigeni kutoka barani Ulaya, Mholanzi Hans van der Pluijm (Yanga) na Mhispania Zeben Hernandez wa Azam, walijikuta wakiingia katika mtego mmoja wa kukumbana na adhabu ya kutolewa kwenye mabenchi ya ufundi na kupandishwa jukwaani kwa mashabiki.

Pluijm alikumbana na hali hiyo katika mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza dhidi ya Ruvu Shooting, kutokana na kuzozana na mwamuzi wa akiba kwa dakika kadhaa, huku Hernandez akikumbwa na ‘cheche’ hilo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, timu yake ilipopambana na Toto African.

Stand United akili ‘mingi’ sana

Licha ya kutibuliwa rekodi yao na Simba ya kutokupoteza mchezo katika uwanja wao wa nyumbani wa Kambarage, lakini bado itaendelea kujivunia matumizi mazuri ya dimba lao hilo na kuipa somo Azam.

Stand United, yenye kikosi cha bei kiduchu, imefanya kile kilichoshindwa kufanywa na matajiri wa soka la ‘Bongo’, Azam FC, yenye wachezaji wa bei ghali, wa ndani hadi nje ya nchi, ambao wamejikuta wakishindwa kutamba katika uwanja wao wa nyumbani wa Azam Complex, pale walipokubali kupoteza michezo miwili na sare tatu.

Mbeya City ‘wazee wa fasta fasta’

Ukiachana na Mbeya City kuvunja rekodi ya Yanga ya kutoondoka na pointi kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya baada ya kuwachapa Wanajangwani hao mabao 2-1, lakini pia timu hiyo ya Manispaa ya Mbeya imekuwa ya kisasa kuliko ilivyo Simba na Yanga kutokana na kuwa na tovuti hai (active) inayoendelea kutoa taarifa za klabu kila wakati.

Hatua yao hiyo imekuwa tofauti na ilivyo kwa wakongwe hao wa soka nchini, Simba na Yanga, hususan Wekundu wa Msimbazi, ambao tangu kuanza kwa msimu Agosti 20 hadi Novemba 10, mwaka huu, hakuna taarifa yoyote kuhusu klabu hizo iliyoripotiwa na tovuti yao, ikiwemo matokeo yote ya michezo 15.

Himid Mao, Mkude walitokaje?

Himid Mao wa Azam na Jonas Mkude wa Simba ambao nafasi zao uwanjani ni viungo wakabaji, wote wakisifika zaidi kutokana na uhodari wao wa kukaba na kupora mipira, walijikuta wakionyeshwa kadi nyekundu kwa makosa tofauti.

Mkude alionyeshwa kadi hiyo dhidi ya Yanga, Agosti Mosi na siku chache baadaye nahodha msaidizi wa Azam, Mao, akikumbana na kiama hicho katika dimba lao la nyumbani mbele ya JKT Ruvu, hatua hiyo iliwafanya kuingia kwenye rekodi mbaya.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -