Saturday, October 31, 2020

Umezipata takwimu hizi za Ligi Kuu England?

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

LONDON, England

MPAKA sasa ni michezo 10 imepita tangu kuanza kwa mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England.

Hata hivyo, mbali na burudani ya uwanjani, tayari kuna takwimu mbalimbali zimeshawekwa.

Mabao yaliyofungwa

Liverpool na Manchester City ndizo timu pekee zilizopachika mabao mengi tangu kuanza kwa msimu huu.

Liver na Man City zimefunga mabao 24 kila moja.

Hata hivyo, Liver wameruhusu nyavu zao kutikiswa mara 13 huku Man City wakifanya hivyo mara tisa.

Tottenham wameruhusu mabao matano pekee na wamecheza michezo mitano bila kupoteza.

Vijana wa Old Trafford ambao msimu huu mambo yameanza kuwaendea kombo wamefunga mabao tisa pekee.

Mashuti yaliyopigwa

Kikosi cha Liver kinachonolewa na kocha raia wa Ujerumani, Jurgen Klopp, kina uhaba wa mashuti.

Mpaka kuanza kwa msimu huu wa 2016-17, wakali hao wa jijini Merseyside wamefanya hivyo mara 78.

Wakati Man City wakipiga mashuti 88, Chelsea wamefanya hivyo mara 90, Tottenham (97) na Arsenal 101.

Manchester United wanaoshika nafasi ya nane kwenye msimmo wamepiga mashuti 182.

Nafasi za mabao

Spurs wametengeneza nafasi 136 za mabao nyuma ya Liver waliofanya hivyo mara 148.

Sunderland ambao hawajashinda mchezo wowote mpaka sasa, wametengeneza nafasi chache kuliko timu zote msimu huu wakiwa wamefanya hivyo mara 59.

Timu zinazoongoza kwa pasi na kumiliki mpira

Mpaka sasa Man City ndiyo timu inayoongoza kwa kumiliki mpira.

Wastani wa kumiliki mpira kwa vijana hao wa Guardiola ni asilimia 65.

Wanaofuata ni Liver (61.4), Tottenham (59.5), Arsenal (58.8) na Man United (55.4).

Liver inaongoza kwa pasi nyingi ikiwa imefanya hivyo mara 6,027.

Nafasi ya pili inashikwa na Arsenal (5,998) na Man City (5,913).

West Brom ina hali mbaya katika kumiliki mpira ikiwa na asilimia 35.4.

Pia, West Brom ina pasi 2,882 pekee na hilo linawafanya kuburuza mkia katika suala hilo.

Msimu uliopita, kufikia hatua hii ya mechi 10, Leicester walikuwa na asilimia 42 ya kumiliki mpira lakini msimu huu wana asilimia 43.2.

 

Wafungaji na ‘asisti’ zao

Staa wa Chelsea, Diego Costa, ndiye anayeongoza orodha ya wafungaji akiwa amepasia nyavu mara nane.

Mhispania huyo ameshatoa pasi mbili zilizozaa mabao ‘asisti’.

Sergio Aguero wa Man City anashika nafasi ya pili akiwa na mabao yake saba na nafasi ya tatu iko mikononi mwa Romelu Lukaku mwenye mabao sita.

Lukaku ameonekana kuimarika zaidi chini ya Ronald Koeman na ndiye mchezaji pekee kufunga ‘hat-trick’ tangu kuanza kwa msimu.

Kwa pamoja, Costa na Eden Hazard mwenye mabao matano wamecheka na nyavu mara 13.

Alexis Sanchez amepasia nyavu mara sita huku akitoa asisti tatu.

Waliokosa nafasi nyingi za mabao

Zlatan Ibrahimovic wa Man United alianza ligi vizuri.

Alianza kazi na Bournemouth, akapachika mawili alipokutana na Southampton kabla ya kufunga dhidi ya Man City.

Mpaka sasa amekosa nafasi nane za wazi na ndiye mchezaji pekee kuwa na rekodi hiyo msimu huu.

Wachezaji wengine wanaoongoza kwa kukosa nafasi za wazi za mabao ni Theo Walcott (6), Jermain Defoe (5) na Lukaku (4).

Muingereza Daniel Sturridge wa Liver amekosa nafasi mbili za wazi msimu huu.

Mastaa wanaoongoza kwa pasi

Jordan Henderson wa Liver ndiye aliyepiga pasi nyingi tangu kuanza kwa msimu huu.

Kiungo huyo ameshapiga pasi 830 na nafasi ya pili inakamatwa na Fernandinho (733).

Mastaa wengine waliopiga pasi nyingi ni Daniel Drinkwater (673), N’Golo Kante, Paul Pogba (630) na Idrissa Gueye (604).

Makipa waliookoa nafasi nyingi za mabao

Tangu kuanza kwa msimu huu wa 2016-17, Tom Heaton wa Burnley ndiye mlinda mlango aliyeonesha umahiri wa hali ya juu kwenye lango lake.

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 30, ameokoa nafasi 52 msimu huu.

Nafasi ya pili inashikwa na Muingereza mwenziye Jordan Pickford ambaye ‘ameziba’ mabao 36 ya wazi.

Mlinda mlango wa Leicester, Kasper Schmeichel, anaingia ‘top three’ akiwa amezuia mipira 35 kuingia kwenye nyavu zake.

Wengine ni Ben Foster wa West Brom (35) na Adrian (34).

Kwa walinda mlango waliocheza dakika zote 90 msimu huu, ni Fraser Forster wa Southampton pekee ambaye ameokoa mabao machache. Kipa huyo amezuia mipira 15 pekee.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -