Wednesday, October 28, 2020

UMUHIMU WA DANSA KWENYE SANAA YA MUZIKI

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NINAENDELEA kufarijika na maoni ya wasomaji wangu mnayonitumia na nitaendelea kuyafanyia kazi kadiri nipatapo muda, kwa lengo la kuboresha kile ambacho nimekuwa nikiwapatia kupitia ukurasa huu kwenye gazeti hili la BINGWA.

Kuna ambao wamekuwa wakiuliza umuhimu wa dansa katika sanaa ya muziki na wengine wanajenga hoja kwamba huenda sanaa ya muziki ikafanyika pengine bila uwapo wa madansa. Sikatai kabisa kwamba muziki unaweza kufanyika bila dansa, lakini je, huu unakuwa muziki wa namna gani? Unamvutia mtazamaji?

Ninavyoamini mimi ni kwamba, muziki hata kama unausilikiza tu kwa namna moja au nyingine, ukikugusa vilivyo ama utatingisha kichwa au kiungo chochote cha mwili wako kufuatisha mapigo ya muziki huo na kwa mwenda ukumbini kuangalia maonyesho ya muziki, ninaamini hatapata ladha halisi ya muziki alioulipia kama akafika na kukuta wasanii wamekaa  kwenye viti jukwaani wanaimba.

Sipati picha ya onyesho la muziki la aina hii ya wasanii kukaa jukwaani na kuimba, bila shaka utakubaliana nami kwamba onyesho hilo halitakuwa na ladha kabisa, hapa ndipo tunaona umuhimu wa mtu anayeitwa dansa kwenye majukwaa ya muziki. Na si dansa tu, bali ni dansa mweledi ambaye ana uwezo wa kuucheza muziki unaopigwa kwa ustadi mkubwa kiasi cha kuburudisha macho na akili za watu wanaomtazama.

Dansa anachezaji kwa ustadi, mirindimo tena kwenye mwendo na muanguko wake, ndiyo maana macho ya watazamaji husuuzika sana wanapowatazama madansa jukwaani badala ya kuwatazama watu waliojipanga kwenye foleni wakiimba.

Tatizo tulilonalo ni moja kwa nchi kama Tanzania na pengine nchi nyingine za Kiafrika na zinazoendelea, hatuna madaraja ya madansa. Katika nchi zilizoendelea kwenye masuala ya sanaa kila aina ya sanaa imewekewa madaraja, hivyo kwa madansa kuna wale wa kulipwa na wao wapo kwenye viwango tofauti.

Hapa ninamaanisha kwamba kwa wenzetu yapo majukwaa ambayo dansa wa daraja (grade) fulani hawezi kupanda kutokana na daraja lake kuwa la chini. Ndiyo maana hata kwenye matukio makubwa ya kimataifa haya ya kimchezo si kwamba anachukuliwa msanii yeyote, bali ni wasanii wa madaraja fulani tu ndio hupewa nafasi kufanya shoo kwenye matukio hayo.

Dansa ni mtu anayenogesha muziki au ngoma, yeye anaupa ladha na thamani kuzidi kutazamika mbele ya macho ya watu hasa pale unapofanyika jukwaani. Kama hakuna dansa jukwaani basi sidhani kama kuna sababu ya kuwa na maonyesho ya muziki makujwaani.

Kwa kuwa dansa anaongeza thamani ya muziki wa kuatazamwa hivyo basi umuhimu wake ni mkubwa sana kwenye fani ya sanaa ya muziki hasa katika dunia ya sasa ambayo watu wanapenda zaidi kuangalia maonyesho ya mubashara kuliko kusikiliza muziki kwenye CD.

Wanaokweda kwenye kumbi za disco hawa wanaweza kuwa na hoja tofauti kabisa, wao wanakwenda huko kwa sababu burudani yao si kuwangalia madansa, bali burudani yao ni ya masikio na kushughulisha miili yao katika kudansi, hawa wanadansi wao wenyewe. Lakini wanaoningia kwenye kumbi za majukwaa msanii akiimba amesimama tu, haitoshangaza kuona mtu huyo amepigwa mawe na kuzomewa ashuke jukwaani.

Ukiyafikiria kwa kina haya mambo utaona wazi kwamba dansa ana umuhimu mkubwa sana kwenye muziki na thamani yake haipaswi kuwa hii tunayoiona leo hii. Fikiria kama Diamond Platinumz angekuwa hatikisiki jukwaani au hana madansa pale mbele, wafikirie Twanga Pepeta au Koffi Olomide, wote wakiimba bila madansa je, shoo zao zitakuwaje?

Pia ikumbukwe kwamba ninapozungumzia madansa hapa nalenga sanaa ya muziki wa majukwaani, muziki ambao utazamwa na si ule wa unaosikilizwa au ule wa kumbi za disko ambako mtu mwenyewe anakuwa dansa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -