Saturday, November 28, 2020

UNAFAHAMU MAKOCHA HAWA WATAZIBAJE PENGO LA SANCHEZ?

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LONDON, England

MKATABA wa staa wa klabu ya Arsenal, Alexis Sánchez, umebakiwa na muda wa miezi 18 huku bado akiwa hajasaini mkataba mpya hadi sasa.

Kwa kile kilichotokea wikiendi iliyopita dhidi ya Liverpool, kimezua mijadala kuwa huenda winga huyo mwenye kasi na nguvu akatimka Arsenal mara baada ya msimu huu wa 2017/18 utakapomalizika.

Kutomwanzisha kwenye mchezo dhidi ya Liverpool kulidaiwa kuwa ni mbinu aliyotaka kuitumia Arsene Wenger ya kucheza mipira mirefu, hivyo basi ni wazi Arsenal imeonesha nia ya kuendelea na Sanchez na lengo lao huenda likawa ni kumng’ang’aniza asaini mkataba mpya.

Lakini iwapo watachukua hatua hiyo, watalazimika kuishi na mtu asiye na furaha zaidi huku kukiwa na hatari ya kumpoteza bure kitu ambacho kina uwezekano mdogo wa kutokea. Unafahamu ni kwanini?

Sanchez bado analipa, kiwango chake kina uwezo wa kuishawishi timu yoyote kubwa Ulaya na ikatoa kiasi kikubwa cha fedha ambacho kitawaacha ‘The Gunners’ na faida nzuri. Lakini hawatakuwa na mshambuliaji mwenye kiwango cha dunia.

Hivyo basi, makala haya yanaangazia ni kocha yupi kati ya hawa watatu atakayebahatika kuinoa Arsenal msimu ujao na usajili wake utakuwa ni wa aina gani kuhakikisha timu hiyo inakuwa na straika anayetishia maisha ya walinzi wa timu pinzani. Kulingana na mbinu zao za soka zilivyo.

Thomas Tuchel – Pierre-Emerick Aubameyang

Aubameyang ameuwasha moto msimu huu chini ya kocha Tuchel. Kiwango chake ndani ya klabu ya Borusia Dortmund kimemsaidia kujulikana duniani kwamba na yeye ni mshambuliaji hatari akiwa na jumla ya mabao 22 ya Bundesliga pekee.

Iwapo Tuchel angekuwa kocha wa Arsenal, ni wazi angehitaji huduma ya straika mwenye mbio ambaye angefiti kwenye mfumo wake wa soka la kasi.

Kule Ujerumani, Tuchel amekuwa akipata changamoto pindi anapomkosa Aubameyang kwenye kikosi chake, kutokana na mfumo wake kumhitaji mshambuliaji mwenye kasi itakayowarahisishia viungo kumpenyezea pasi ndefu na zenye macho wakati timu ikifanya shambulizi la kushtukiza.

Aubameyang ni mwepesi miguuni, mbio zake ni zaidi ya kasi ya mawimbi ya sauti na kwa jinsi alivyozoeana na Tuchel isingekuwa kazi ngumu kumshawishi atue Emirates na kuwa silaha muhimu ya Tuchel kwenye vita ya ubingwa.

Leonardo Jardim – Kylian Mbappe

Asilimia kubwa ya dunia ya soka tayari imeshashuhudia aina ya soka linalochezwa na klabu ya Monaco inayonolewa na kocha Leonardo Jardim.

Hebu vuta picha Arsenal inamnasa Jardim kwa ajili ya msimu ujao. Ni wazi Arsenal watakuwa wamemasa fundi wa mbinu za ushambuliaji wa kutisha, akiwa anaifanya Monaco ing’ae msimu huu.

Kylian Mbappé, ndiye kifaa muhimu cha maangamizi ndani ya kikosi hicho, kinda la miaka 18 linaloonesha maajabu ya soka msimu huu.

Kwenye zile ligi tano kubwa Ulaya, Mbappé anatisha. Ni mchezaji anayeizalishia timu yake mabao ya kutosha (mabao tisa na asisti tano).

Sanchez akitimka Arsenal na Jardim akitua hapo, ni wazo kinda wa Kifaransa atapata nafasi moja kwa moja kwenye kikosi ambacho kitaendelezwa kwa tamaduni zile zile za Wenger (soka la pasi na kasi).

Jardim atadumu mno na Mbappe na huenda pia akamfanya kuwa mchezaji bora kwa miaka mingi zaidi.

Massimiliano Allegri – Alvaro Morata

Kama Allegri atatua Emirates, Arsenal watakuwa imemnasa kocha bora zaidi mwenye uwezo wa kutumia mifumo tofauti kila inapobidi. Pia watakuwa wamempata kocha mwenye uzoefu wa kushindania mataji akiwa na timu kubwa mbili (AC Milan na Juventus).

Hivyo basi, Arsenal itampata daktari atakayetibu magonjwa mawili kiufasaha.

Mbinu atakazokuja nazo Allegri ni pamoja na kuchezesha washambuliaji wawili, ambapo mtu kama Olivier Giroud atajikuta akirudi kwenye kikosi cha kwanza.

Kama Giroud atakuwa mshambuliaji wa mwisho, ni lazima atahitajika mshambuliaji mwingine mnyumbulifu nyuma yake ambaye ni Morata. Patamu hapo!

Morata ni straika mwenye ufundi mwingi licha ya umbo lake kuwa refu kama alivyo Giroud, lakini ana kingine zaidi ya hicho; nacho ni takwimu nzuri ya mabao na asisti licha ya kucheza dakika 818 tu akiwa na Real Madrid msimu huu (mabao nane na asisti mbili).

Kwa msimu huu, Morata atapata shida kuingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Zinedine Zidane licha ya kwamba ni mchezaji mwenye faida pindi anapotokea benchi.

Mhispania huyo ana nafasi ya kufanya vizuri kwenye mechi za wiki baada ya wiki pale Emirates chini ya Allegri.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -