Sunday, January 17, 2021

UNAHITAJI MUDA ZAIDI KUIELEWA MIPANGO YA BEN POL

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA CHRISTOPHER MSEKENA

HUTAWEZA kuipata sauti ya Ben Pol kwenye wimbo wako kama hujatenga fungu la dola za Kimarekani 5,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 10 za Tanzania huku akidhamiria gharama hiyo ianze kutumika mapema mwakani.

Anakuwa ni msanii wa kwanza kuweka hadharani kiwango ambacho atahitaji alipwe ili aweze kuingiza sauti yake kwenye wimbo anaotaka kushirikishwa, wengi huwa hawafanyi hivyo kutokana na sababu mbalimbali.

Kolabo ni kitu kinachoweza kujenga au kumbomoa msanii, si kila kolabo inaweza kuwa na neema, nyimbo nyingine za kushirikishwa huwaingiza wasanii kwenye janga la kuchokwa na mashabiki.

Wingi wa kolabo hupunguza utamu wa msanii kwa mashabiki. Watu wanachoka kumsikia kwenye kila wimbo kwa kuwa kila kitu kitamu kinapitia hatua tatu na hatimaye huonekana kibaya. Hicho ndicho kinawatokea wasanii wengi waofanya kolabo bila mipango.

Kinachofanya msanii mmoja kupata kolabo nyingi yaani kushirikishwa mara nyingi na wasanii wenzake ni kuwa kwenye nafasi fulani ya juu kwa wakati huo. Nadhani tunakumbuka enzi za Chid Benz.

Huyu ni rapa aliyewindwa na kila msanii. Alifanya kolabo nyingi kwa wakati mmoja, sauti yake nzito na mistari mikali aliyokuwa anaiandika ilisikika mara kwa mara kwenye masikio ya mashabiki kupitia kolabo hizo.

Sijajua kama alikuwa anatoza fedha kwa kila kolabo au alikuwa anafanya kishkaji. Maana kuna nyimbo nyingine alizoshirikishwa hazikuwa na mbele wala nyuma ila zilibebwa tu na mistari aliyoichora Chid Benz.

Utamu wa nyimbo za msanii huyo ukawa wa kawaida na baadaye ukawa mbaya, leo hii mtu akifanya kolabo na Chid Benz sidhani kama itawashtua watu kama ilivyokuwa kipindi kile.

Tusogee mpaka kwa bingwa wa kolabo za kimataifa, Diamond Platnumz. Baada ya kupata umaarufu Afrika wasanii mbalimbali wa Nigeria, Afrika Kusini na nchi nyingine wakaanza kuiwinda sauti yake.

Diamond amefanya kolabo nyingi ambazo zaidi zimewapa faida wale waliomshirikisha. Wasanii hao wamenufaika kwa kufanya biashara ya nyimbo zao huku wakitengeneza mtaji wa mashabiki.

Majina ya wasanii kama K Cee, Akothee, AKA, Jah Prayzah yamepata umaarufu zaidi hapa Bongo baada ya kufanya kolabo la Diamond. Sijajua faida alizozipata Diamond kufuatia kufanya kolabo alizoombwa na wasanii hao wa Afrika.
Ieleweke kuwa kolabo si kitu kibaya kwa msanii, ni kitu kizuri kwa sababu muziki bila kuchanganya ladha huwezi kupata burudani mujarabu inayotakiwa, ni lazima msanii mmoja na mwingine waungane, wafanye kazi itakayokuwa na faida kwa wote wawili.
Sina shaka na maamuzi ya Ben Pol, muuaji wa viitikio (chorus killer) ambaye hajawahi kuharibu katika kila wimbo anaoshirikishwa. Anajua nini afanye anapokutana na rapa hali kadhalika anatambua njia ipi nzuri ya kunogesha kolabo atakayoombwa na mwimbaji mwenzake.
Tusiende mbali, tubaki hapa hapa kwa Darasa, staa wa singo ya Muziki. Ben Pol ana mchango mkubwa kwa rapa huyu toka Kiwalani, Dar es Salaam. Ndiye aliyesababisha watu wakamfahamu Darasa kupitia wimbo wa Sikati Tamaa na leo hii amefanya makubwa kwenye wimbo wa Muziki.
Hebu tuache maneno mengi na tuweke muziki kama biashara halafu vuta picha baada ya kolabo hiyo na Darasa ni wasanii wangapi watataka kufanya kolabo na Ben Pol? Jibu ni wengi sana, sasa sidhani kama Ben Pol anataka kolabo sisizo na mipango.
Kiwango hicho cha fedha alichokitaja kitafanya Ben Pol afanye kolabo chache zenye uhakika. Asipoteze muda wake kufanya kitu ambacho hajui mwisho wa siku yeye atanufaika vipi na zaidi kinamwongezea thamani yake mwaka 2017. Asante.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -