Tuesday, November 24, 2020

UNAHITAJI MWENZA MWENYE MAPENZI YA DHATI, HUYU HAPA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA MICHAEL MAURUS,

NDUGU wasomaji, karibuni sana kwenye safu hii ya mambo ya mahusiano ambayo huwajia kila Jumanne na Jumamosi, ikilenga kujuzana hili na lile kuhusiana na mambo ya uhusiano wa kimapenzi.

Kabla ya kuendelea na mada ya leo, niwashukuru wote ambao wameonekana kuguswa na mada zangu na kutoa maoni yao huku wengine wakiuliza maswali mbalimbali.

Ama kwa hakika, inaonyesha kuwa mambo ya mahusiano ya kimapenzi yanawagusa wengi, kuanzia vijana wadogo wa makamo hadi wazee, ikiwa ni wa jinsia ya kike na ya kiume.

Baada ya salamu hizo, nigeukie katika mada ya leo inayosomeka ‘Unahitaji mwenza mwenye mapenzi ya dhati, huyu hapa’, ikilenga kukujulisha ni vipi unaweza kumfahamu au kumpata mpenzi wa kulienzi penzi lako kwa kiasi kile kile au zaidi ya unalomwonyesha.

Ndugu msomaji, ni ukweli usipingika kuwa ni vigumu mno kufahamu kama mpenzi uliye naye anakupenda kwa dhati kutokana na ukweli kwamba upendo wa mtu kwa mwingine, hauwezi kuonekana kwa macho bali ni hisia zake zilizopo moyoni mwake.

Wapo wanaoamini yule anayekununulia zawadi mara kwa mara au anayekuvulimia nyakati za shida, ndiye akupendaye kwa dhati, wengine

wakiamini wapenzi ambao ni wavumilivu kwa wenza wao, wenye kusamehe pale wanapokosewa, wasio wachoyo na wanaopenda ndugu wa upande mwingine, wenye wivu, wepesi wa kuomba msamaha wanapokosea na mengine kama hayo, ndiyo wenye mapenzi ya kweli.

Lakini tujiulize, ni wangapi walikuwa na wapenzi wenye sifa kama hizo lakini mwisho wa siku walitendwa?

Bila shaka ni wengi mno. Sasa ni vipi tunaweza kufahamu wapenzi wenye mapenzi ya kweli? Ipo njia ambayo ni rahisi mno na isiyo na gharama yoyote ya kuwa na wapenzi wenye mapenzi ya dhati.

Njia hiyo si nyingine bali ni kutotumia macho yetu kuchagua wapenzi.

Kama kweli haupo tayari kutendwa na mpenzi wako, hata siku moja usikubali macho yako yakuchagulie mwenza.

Macho yetu mara zote yamekuwa yakiangalia aidha uzuri wa sura wa mtu, uwezo wake kifedha, rangi, elimu, kimo, umaarufu wake, huku wengine na sisi tukibabaishwa zaidi na urefu wa nywele zake au ametokea kabila ambalo linasifika kwa ‘mambo fulani’ au la.

Kwa hali kama hiyo, huwezi kubaini kama huyo unayemtolea macho anaweza kuwa na mapenzi ya dhati na wewe.

Tufanye nini sasa? Ni rahisi mno. Kama haupo tayari kuteseka kimapenzi, ni vema kumshirikisha Mungu wakati unapotaka kupata mwenza wa kuanzisha naye uhusiano wa kimapenzi.

Unachotakiwa kufanya ni kuongea na Mungu wako kuwa unahitaji mwenza atakayekuwa na mapenzi ya dhati. Katika hilo, unatakiwa kuwa makini kwani wakati ukifanya hivyo, kumbuka shetani naye atakuwa akisikia, hivyo anaweza kutangulia kukuletea watu wa kila aina, hasa wale anaoamini ndio ‘ugonjwa’ wako.

Hivyo basi, kwa kila atakayekuja mbele yako, ni vema ukamuuliza Mungu wako kama huyo ndiye sahihi kwako kulingana na ubora au udhaifu wako.

Ni wazi iwapo utamshirikisha Mungu katika kutafuta mwenza wa kumkabidhi moyo wako, hawezi kukuangusha hata kidogo.

Hata hivyo, epuka kutanguliza mbele vigezo kama nilivyovitaja hapo juu kwani kufanya hivyo, unaweza kujikuta ukimkataa mpenzi atakayelienzi penzi lako ati tu kwa sababu si mweupe kama unavyotaka na kujikuta ‘ukiingia mkenge’.

Ndugu msomaji, kwa leo niishie hapo, usikose toleo la Jumamosi wiki hii ambapo nitawaletea mada inayohusiana na sababu za uchumba kuyeyuka ndani ya muda mfupi. Tuma maoni yako kupitia namba na anuani pepe hapo juu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -