Sunday, November 29, 2020

Unajua kwamba Man City, Uefa ni chui na paka?

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

MANCHESTER, England

MANCHESTER City inajaribu kuangalia uwezekano wa kujenga utawala wao wa soka barani Ulaya, hasa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Msimu uliopita, wakiwa chini ya kocha Manuel Pellegrini, safari ya Man City katika michuano hiyo iliishia hatua ya robo fainali.

Mabingwa wa soka wa La Liga, Real Madrid, ndio waliozika ndoto ya timu hiyo kutinga nusu fainali ya mashindano hayo yenye heshima kubwa barani Ulaya.

Haitakuwa rahisi kivile, kwani iliwachukua Barcelona miaka 30 kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kwa upande wa mahasimu wao, Real Madrid, baada ya kushindwa kuchukua ubingwa wa mashindano kwa mara ya sita, walisubiri kwa kipindi hicho kupata taji lao la saba.

Katika kuhakikisha wanatimiza ndoto yao ya kulitia mkononi taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, mabosi wa Man City wamemchukua kocha Pep Guardiola, ambaye alilipata mara mbili alipokuwa Barca.

Hata hivyo, licha ya kuhitaji kwa udi na uvumba ubingwa wa michuano hiyo mikubwa barani Ulaya kwa ngazi ya klabu, Man City wamekuwa na uhusiano mbovu na waandaaji wake, yaani Shirikisho la Soka barani humo (Uefa).

Mara kadhaa klabu hiyo imejikuta ikiingia matatizoni na Uefa na hata mashabiki wake wamekiri kuwa wanalichukia shirikisho hio.

Aprili 2012

Miaka minne iliyopita, Man City walikuwa Ureno kucheza na mabingwa wa soka nchini humo katika mtanange wa Ligi ya Europa.

Mchezaji wao, Mario Balotelli, ambaye hivi sasa anakipiga katika klabu ya Nice, alifanyiwa vitendo vya ubaguzi wa rangi na mashabiki wa Porto.

Kutokana na tukio hilo, Porto walitozwa faini ya euro 20,000 na Uefa.

Kilichowakera zaidi mashaiki wa Man City ni kitendo cha timu kutakiwa kulipa zaidi ya kiasi hicho (euro 30,000) eti kwa sababu walichelewa kuingia uwanjani kwa dakika moja katika mchezo mwingine dhidi ya Porto.

Hoja ya Man City ni kwamba, kosa lao halikustahili faini kubwa kuliko lile la ubaguzi wa rangi lililofanywa na mashabiki wa Porto.

Oktoba 2013

Ni kipindi hiki ndipo staa wao, Yaya Toure, alipokumbana na ubaguzi wa rangi katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya CSKA Moscow.

Mashabiki wa Warusi hao walimfanyia vitendo vya ubaguzi wa rangi kiungo huyo, ingawa timu yao iliambulia kipigo cha mabao 2-1.

“Nimesikitishwa, nimesikitishwa sana na kile kilichofanywa na mashabiki (wa CSKA Moscow),” alisema Toure baada ya mechi hiyo.

“Nafikiri Uefa wanatakiwa kuchukua hatua kwa sababu huenda wakawaunga mkono kutokana na kuwa na rangi zinazofanana.”

Adhabu waliyotoa Uefa kwa CSKA Moscow ya kucheza mchezo mmoja bila mashabiki haikuonekana kuwafurahisha Man City, ambapo walidai ilitakiwa kuwa kubwa zaidi.

Pia, kwa kuzuia mashabiki kuingia uwanjani, Man City walihisi kama zimeadhibiwa timu mbili licha ya kosa kufanywa na CSKA.

Mei 2014

Klabu ya Man City ilishukiwa na rungu la Fifa kwa kitendo chao cha kukiuka sheria za matumizi ya fedha ‘Financial Fair Play’.

Moja kati ya adhabu waliyopewa na Uefa ni kuwa na wachezaji 21 badala ya 25 katika kikosi chao cha Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Lakini pia, walitakiwa kulipa faini ya pauni milioni 50 na hilo liliwafanya mabosi na mashabiki wa Etihad kuona wanaonewa na Uefa.

Oktoba 2014

Mchezo ambao CSKA Moscow walitakiwa kucheza bila mashabiki ni ule uliowakutanisha tena na Man City.

Wakati mashabiki wa Man City wakibaniwa kuuziwa tiketi kutokana na adhabu hiyo, wenzao 200 wa CSKA walifanikiwa kuingia uwanjani na kuutazama mtanange huo mwanzo mwisho, jambo lililoonekana kuwakera sana matajiri wa Etihad.

Kutokana na nguvu kubwa ya mashabiki wake, CSKA ilipata sare ya mabao 2-2.

Novemba 2015

Ni kipindi ambacho Uefa waliifungulia mashitaka klabu ya Man City baada ya mashabiki wake kuzomea wimbo wa shirikisho hilo.

Tukio hilo lilitokea katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Sevilla.

Hata hivyo, kesi hiyo ilifutwa kutokana na ukosolewaji mkubwa wa madai hayo ya Uefa.

Ikiwa ni sehemu ya kuonyesha hasira zao, mchezo uliofuata ulishuhudia mashabiki wa Etihad wakiwa na mabango yaliyokuwa yakilitupia vijembe shirikisho hilo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -