Thursday, December 3, 2020

Unajua nini? Hebu ngoja nipige stori na Kichuya…

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

SIHITAJI kusimuliwa binafsi nazijua tabia za wachezaji wa Kitanzania, zinafanana sana na huwa zinanikera kwa sababu kwa kiasi kikubwa zimechangia hadi leo hii kuwa na wachezaji wachache wanaofanya vizuri nje ya nchi.

Tena hata kutumia neno wachache nimewapendelea kwa sababu kiuhalisia tuna mchezaji mmoja tu ambaye anafanya makubwa nje ya mipaka ya ardhi hii ya Mlima Kilimanjaro.

Hapa namzungumzia Mbwana Samatta anayefanya makubwa sana akiwa na kikosi cha KRC Genk, ambaye naamini amefika pale alipo si kwa sababu ana kipaji cha pekee sana kulinganisha na wachezaji wengine wa Kitanzania, hapana!

Samatta yuko pale kwa sababu ya kuwa Mtanzania mwenye tabia za Afrika Magharibi za kutokuridhika na mafanikio anayoyapata na kupambana kusaka mafanikio zaidi na zaidi.

Lakini potelea mbali ngoja nimpumzishe Samatta, kwanza kama kuandikwa ameshaandikwa sana na hana tena cha kuthibitisha tayari Afrika na dunia inajua jina lake.

Nirudi hapa nyumbani kwa sababu leo nataka kupiga stori na mdogo wangu, Shiza Kichuya ambaye sasa hivi jina lake linatikisa kila kona ya Tanzania kutokana na lile bao alilomtungua Ally Mustapha ‘Barthez’ siku ya Kariakoo ‘Derby’.

Lakini kabla ya kuanza stori zetu kwanza mdogo wangu nakuomba mtazame kijana mmoja hapo Simba anaitwa Manyika Peter Jr. Ukimaliza kumtazama huyo tafuta njia ya kuweza kumcheki dogo mmoja yuko pale Jangwani anaitwa Geofrey Mwashiuya.

Najua unashangaa kwanini nimekuambia uwaangalie hawa jamaa wawili, lakini usiwe na wasiwasi katika stori zetu nitakueleza sababu ya kukutuma uwacheki hawa madogo.

Lakini wakati ukiendelea kuwaangalia hawa wawili mtazame nahodha wako, Jonas Mkude, kisha mtafute mtu akusimulie kuhusu wakongwe wawili; Athuman Iddi ‘Chuji’ na Haruna Moshi ‘Boban’, halafu urudi hapa tuendelee kuzungumza.

Kwa Mkude nitakuambia hili tu ‘kipaji chake na kasi yake ya ukuaji kisoka haviendani, lakini hii yote kwa sababu ya mambo yake mengi ya nje ya uwanja’ ambayo sitaki kuyasema yapi, ila naamini kama asingekuwa anayafanya uwezo wake uwanjani kwa sasa ungekuwa mara 10 zaidi ya huu.

Lakini kwa wakongwe Chuji na Boban unatakiwa kujua hili, hawa ni moja kati ya viungo bora zaidi katika soka la Tanzania kwenye zama za karibuni, ila amini nakuambia kama Taifa halijafaidi kilele cha ubora wao kwa sababu tu ya zile tabia ambazo awali nilisema nazijua sana.

Kuhusu Manyika Jr na Mwashiuya hawa nadhani ni umri wako, ila nitakuhadithia stori zao kidogo ili uelewe zaidi dhumuni la mimi kutaka kuzungumza na wewe.

Iko hivi;- Mwashiuya alitua Yanga akitokea Kimondo akiwa na uwezo mkubwa sana wa kutumia guu lake lile la kushoto kama wewe hivyo, kasi na mashuti yake yalimfanya atabiriwe makubwa katika ulimwengu wa soka la Bongo.

Moto alioanza nao Jangwani hakuna asiyeukumbuka, lakini bahati mbaya kwake akashindwa kuendana na presha ya kuchezea klabu kubwa huku sifa za mashabiki zikimvimbisha kichwa na kumpoteza.

Inawezekana kwa sasa anasumbuliwa na majeruhi, lakini kiukweli hata kabla ya jeraha la goti alilolipata tayari alishaanza kupoteza mwelekeo, hiyo yote kwa sababu tu alishindwa kuendana na ustaa uliokuja kwake kwa kasi.

Hivyo hivyo ilikuwa kwa Manyika, huyu yeye alianza kwa kudaka kwenye mechi ya Simba na Yanga huku akionyesha uwezo mkubwa sana na kutokana na kipaji chake watu waliamini kuwa yeye ndiye alikuwa mtu aliyekuja kuvaa viatu vya Juma Kaseja ambavyo kwa miaka mingi vimekosa mtu pale Msimbazi.

Lakini bahati mbaya kwake maisha ya nje ya uwanja na Instagram, yakakiteka kichwa chake kiasi cha kufikia kuandika ‘upuuzi’ kwenye mtandao wake wa kijamii kuonyesha jinsi gani alikuwa kavimba kichwa.

Sasa unajua kilichomkuta? Yuko tu hapo Msimbazi anazidi kunenepa, huku akisugua benchi kila kukicha na kumfanya Vincent Angban (ambaye niwe mkweli uwezo wake si mkubwa hivyo, lakini anadaka Simba kwa sababu Manyika ameshindwa kuendana na kipaji chake) akijihakikishia namba ya kudumu katika timu hiyo.

Unaweza kunishangaa kwanini nawazungumzia watu wengine wakati dhumuni langu ni kupiga stori na wewe, lakini ondoa shaka, nitakuambia.

Ukweli ni huu, inawezekana sasa hivi jina lako ni kubwa zaidi ya lile la Laudit Mavugo pale Simba, lakini hiyo isiwe sababu ya wewe kubweteka na kuvimba kichwa, huku ukilewa sifa zisizo na msingi.

Mdogo wangu Kichuya napiga stori na wewe kwa sababu nataka kukufikishia ujumbe huu, unahitaji kucheza soka huku ukijua wazi kuwa kipaji si kufanikiwa unahitaji kujitambua na kupambana kujua nini unataka.

Samatta yuko pale leo kwa sababu alilijua hilo, lakini hawa wengine niliokuambia wako hapa walipo leo hii kwa sababu walihisi kipaji pekee kilitosha kuwavusha wakalewa sifa na kushindwa kujitambua.

Kichuya sifa za Kariakoo zisikuleweshe mdogo wangu, kaa chini kumbuka ulikotoka, iangalie Simba kama njia ya kufikia mafanikio yako kwa sababu ukijisahau hawa wanaoimba jina lako leo ndio watakaokutukana kesho ukivimba kichwa.

Hivyo kwa mifano hii na stori hizi tulizopiga sitarajii kukuona ukipotea kwa sababu najua guu lako la kushoto lina vitu vingi sana ambavyo bado hatujaviona na ni wewe pekee ambaye unaweza kufanikisha hilo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -