Wednesday, November 25, 2020

UNAKIFAHAMU KILICHOZIKUTA TIMU ZILIZOSHINDA MECHI MFULULIZO EPL

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LONDON, England 

USHINDI wa mwishoni mwa wiki ambao Chelsea iliupata dhidi ya  West Brom ulifanya ifikishe mechi ya tisa bila kufungwa tangu ulipoanza mwezi Oktoba mwaka huu.

Na mwingine ambao iliibuka nao juzi usiku dhidi ya Sunderland ukawafanya wafikishe idadi kama hiyo kwa mara ya tatu katika historia ya Ligi Kuu England.

Hata hivyo, kuna swali la kujiuliza, huwa kunakuwapo na manufaa yoyote kwa timu zinazofanya hivyo ifikapo mwisho wa msimu?

Ifuatayo ni orodha ya timu ambazo zimewahi kufanya hivyo na ni kitu gani zilikipata baada ya hapo.

 Arsenal – Mechi 10  

Kuanzia Machi 11, 1998 – hadi Mei 3, 1998

Ukiwa ni msimu wake wa kwanza mzima kwa Arsene Wenger tangu alipotua Highbury, ilishuhudiwa Arsenal ikiweka rekodi ya kushinda mechi 10 na huku ikiwa njiani kutwaa ubingwa msimu wa 1997/98. Na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Everton ukatosha kutwaa taji hilo na hivyo kumfanya Wenger awapumzishe wachezaji wake muhimu kwa ajili ya mechi mbili za mwisho na hivyo kutimiza nia yake ya kutwaa mataji mawili baada ya kuichapa  Newcastle United katika mechi ya fainali ya michuano ya kombe la FA.

Chelsea – Mechi 10  

 Kuanzia Novemba 19, 2005 hadi Januari 15, 2006

Ikiwa imeshauanza msimu wa 2005/06  kwa kupata ushindi wa mechi tisa mfululizo, kikosi hicho cha Jose Mourinho kilikuwa kimejikita kileleni mwa ligi kutokana na kuwa kilikuwa kimeshashinda nyingine 10 katika kalenda ya mwaka 2005.

Kwa kushinda mechi hizo, tayari ilitosha kutawazwa kuwa mabingwa, wakiwa mbele kwa pointi nane.

Liverpool – Mechi 10

Kuanzia Oktoba 29, 2005 hadi Desemba 31, 2005

Ni katika kipindi hicho ambacho  Chelsea walikuwa wakiziburuza kila timu na Liverpool nayo ilikuwa ikifanya hivyo kwa kushinda mechi 10 mfululizo  na hivyo kuwapo na mchuano mkali katika mbio za kuwania ubingwa wa 2006.

Hata hivyo, tatizo lililowapata walikuwa wameshinda mechi mbili kati ya nane za mwanzoni mwa msimu na wakajikuta wakikumbwa na janga kama hilo mwanzoni mwa mwaka mpya na hivyo kujikuta wakizinduka na kushinda nyingine tisa za mwisho wa msimu zilizowasaidia kumaliza ligi wakiwa nafasi ya tatu.

Chelsea – Mechi 11  

 Kuanzia Aprili 25, 2009 hadi Septemba 20, 2009

Matumaini ya Chelsea ya kutwaa ubingwa msimu wa 2008/09 yalitoweka  katika kipindi ambacho ilianza kupata mfululizo mwishoni mwa Aprili.

Katika kipindi hicho iliweza kushinda mechi tano, ikiwa chini ya Guus Hiddink  na kufanikiwa kumaliza ikiwa nafasi ya tatu, nyuma ya Manchester United na  Liverpool.

Liverpool – Mechi 11  

 Kuanzia Februari 8, 2014 hadi Aprili  20, 2014

Liverpool iliweza kushinda mechi 11 bila kupoteza pointi, jambo ambalo liliwafanya kuchupa kutoka nafasi ya nne na hivyo kuonekana kuwa mbioni kutwaa ubingwa wao wa kwanza wa Ligi Kuu baada ya kipindi cha miaka 20.

Hata hivyo, pamoja na kufanya hivyo, wakajikuta wakivurunda katika mechi za mwisho na hivyo wakamaliza msimu wakiwa nafasi ya pili.

Manchester City – Mechi 11

 Kuanzia 19, 2015 – hadi Septemba 12 2015

Manchester City, ambao walikuwa mabingwa watetezi, waliuanza msimu huo vibaya kwa kupoteza mechi nne kati ya sita za msimu uliopita 2014/15, lakini baadaye wakaja kushinda sita za mwisho na hivyo wakafanikiwa kushika nafasi ya nne na huku Leicester City wakiibuka  kuwa mabingwa.

Manchester United – Mechi 11  

 Kuanzia Desemba 26, 2008 hadi Machi  4, 2009

Man United walikuwa wameshatwaa ubingwa mara kadhaa wakati walipofika sikukuu ya Krismasi ya mwaka 2008 wakiwa nafasi ya tatu.

Hata hivyo, wakiongozwa na mastaa  Cristiano Ronaldo na Wayne Rooney, wakashinda 11 kabla ya Machi kupoteza mbili, lakini baadaye wakazinduka na kufanikiwa kutetea taji lao.

 Manchester United – Mechi 12  

Kuanzia Machi 11, 2000 hadi Agosti  20,  2000

Kikosi hicho cha Sir Alex Ferguson kilikuwa tayari kileleni mwa msimamo wa ligi wakati kilipoanza kuvurunda  mwishoni mwa msimu wa 1999/2000.

Hata hivyo, baadaye kikazinduka na kushinda 11.

Arsenal – Mechi 14  

Kuanzia Februari 10, 2002 hadi Agosti  18, 2002

Arsenal walikuwa hawajafungwa hadi wakati wa sikukuu ya Krismasi, jambo ambalo liliwaweka kwenye mazingira ya kutwaa ubingwa kwa kushinda mechi  13 za msimu wa 2001/02.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -