Monday, November 30, 2020

UNAKUMBUKA: Dua alikata kilimilimi cha Yanga 1993

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

KATIKA safu ya unakumbuka wiki hii tunajikumbusha tukio moja lililofanywa na mshambuliaji mahiri wa zamani wa Simba, Dua Said la kukata kilimilimi cha Yanga baada ya kuifungia timu yake bao 1-0. Dua baada ya kufunga bao hilo ilikuwa ni kulipiza kisasi cha timu yake kufungwa mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza. Mechi hiyo ambayo ilikuwa ni kali na ya kusisimua wakati wote wa dakika 90, ilichezwa siku ya Jumamosi Julai 17, 1993 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam (sasa Uhuru). Mchezaji aliyetoka na huzuni kubwa uwanjani ni Zamoyoni Mogela ‘DHL’, ambaye mbali na kutolewa katika nafasi yake iliyochukuliwa na John Alex katika kipindi cha pili, Zamoyoni aliishia kumpiga mateke mtazamaji mmoja baada ya filimbi ya mwisho kupulizwa. Haikueleweka mara moja chanzo cha vurumai yao ilikuwa ni nini, lakini Mogela akiwa amekasirika alimshushia mateke mtu huyo na polisi waliingilia kati kwa kumzuia mshambuliaji huyo ambaye katika kipindi cha umaarufu wake alikuwa akichezea klabu ya Simba. Baada ya Simba kushinda katika mchezo huo kwa kiasi fulani kulizima mgogoro wa uongozi uliokuwa ukifukuta chini kwa chini. Katika mchezo huo Simba ilitawala mechi hiyo na kuwazidi wapinzani wake Yanga katika kila idara. Ukimwondoa Method Mogela (marehemu) ‘Fundi’ wa Yanga ambaye aling’ara na kucheza vizuri, kazi yake ilishindwa kutoa matunda kwa vile wachezaji wengine wa timu hiyo walikuwa wamezimwa na walishindwa kufurukuta kabisa. Wakati winga, Edibily Lunyamila wa Yanga alilindwa vikali na beki Kasongo Athumani, mshambuliaji hatari Mohamed Hussein ‘Mmachinga’ wa Yanga alizimwa kabisa na kushindwa kutamba chini ya ulinzi wa Iddi Seleiman ‘Mayor’ huku Said Mwamba ’Kizota’ akichungwa vilivyo na beki Fikiri Magoso wa Simba. Wachezaji wa Simba kama wangetulia vizuri wangetoka uwanjani na ushindi mkubwa, kwani katika kipindi cha kwanza ilipoteza nafasi mbili za wazi zilizopotezwa na Damian ‘Kimti’ na Dua Said. Kipindi cha pili pia ‘Kimti’ na Malota Soma waliikosesha Simba mabao. Ukiondoa purukushani za hapa na pale katika lango la Simba hakuna hata moja ya nafasi ya wazi ambayo Yanga waliipata ya kufunga bao katika mechi hiyo ambayo pia ilitawaliwa na mchezo wa rafu. Mchezaji pekee aliyepeleka msiba Mtaa wa Jangwani na Twiga na furaha ya aina yake Mtaa wa Msimbazi makao makuu ya Simba alikuwa ni kijana mdogo winga wa kushoto, Dua Said. Dua alifunga bao safi kwa kichwa baada ya kupokea pasi murwa ambapo kabla pasi tano za vichwa vilipigwa na wachezaji wa Simba ambao ni Malota Soma, Edward Chumila ‘Smile Boy’. Dua Said alijitosa katikati ya mabeki wa Yanga na kuwahi mpira ambao aliupiga kichwa na kupishana na kipa Stephen Nemes aliyekuwa anatoka langoni na kutuama polepole kimiani na kuasha shangwe za aina yake kwa wapenzi na mashabiki wa Simba. Ushindi huo ulimfanya aliyekuwa kaimu mwenyekiti wa Simba, Fakhroudin Amijee, apumue kutokana na upinzani uliokuwa unamkabili kutoka kwa baadhi ya wanachama wa klabu hiyo ambayo walitaka nafasi hiyo iliyoachwa na marehemu Mikidadi Kasanada ichukuliwe na mmoja wa wanachama wawili, Dk. Lutter Nelson au Amiri Bamchawi. Baada ya mchezo huo kumalizika wapenzi na mashabiki wa Yanga walianza kumsakama kocha wao kutoka Burundi, Tauzany Nzoyisaba na wengine wakidai kuwa alifanya mabadiliko mabaya kwa kuwatoa Zamoyoni Mogela, Stephen Mussa na nafasi zao kuchukuliwa na John Alex, Hamisi Tobias ‘Gagarino’. Kocha wa Simba wakati huo alikuwa ni Mansour Magram ambaye kabla ya mechi hiyo alikuwa akifundisha soka la kulipwa Uarabuni, alifanya kazi ya kuinoa Simba akisaidiana na kocha Abdallah ‘King’ Kibadeni na Anteneh Ashete kutoka Ethiopia. Hamdun kutoka Kigoma ambaye alimudu vilivyo mchezo huo kwa kuwa makini tokea dakika ya kwanza tu ya mchezo na alidhihirisha kwamba yeye ni mmoja wa waamuzi ambao taifa hili linaweza kujivunia. Katika mchezo huo, Simba iliwakilishwa na Mohamed Mwamejal Kasongo, Athumani, Rashid Abdallah, Fikiri Magoso, George Masatu, Iddi Seleiman ‘Mayor’, George Lucas ‘Gazza’, Ramadhani Lenny (marehemu)/Abdul Mashine, Damian Mrisho ‘Kimti’/Edward Chumila (marehemu), Malota Soma ‘Ball Juggler’ na Dua Said. Yanga iliwakilishwa na Stephen Nemes, Mwanamtwa Kiwhelo, Kenneth Mkapa, Willy Mtendamema, Salum Kabunda (marehemu), Method Mogela (marehemu), Zamoyoni Mogela/ John Alex, Stephen Mussa/Hamisi Tobias ‘Gagarino’ (wote marehemu), Said Mwamba ‘Kizota’ (marehemu), Mohamed Hussein ‘Mmachinga’ na Edibily Lunyamila. Mwamuzi wa mchezo huo alikuwa ni Nassoro

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -