Sunday, November 1, 2020

UNAKUMBUKA? HOSSAN ALIVYOPELEKA SIMANZI MAJIMAJI 1999

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA HENRY PAUL


HISTORIA ya timu ya National Al-Ahly ya Misri kuziadhiri timu za Tanzania katika michuano ya kimataifa, ilijirudia kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam (sasa Uwanja wa Uhuru), ilipoilaza timu ya Majimaji ya Songea mabao 3-0, katika mchezo wa awali wa Kombe la Washindi Afrika.

Majimaji ilipata tiketi hiyo baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi ya Muungano mwaka 1998.

Alikuwa ni mshambuliaji bora wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 1998, iliyofanyika mjini Ouagadougon, Burkina Faso, Hossam Hassan wa Misri ambaye aliifungia timu yake ya National Al-Ahly mabao yote matatu ya ushindi.

Katika mchezo huo, Majimaji ilianza kuonesha kandanda safi kwa kucheza gonga fupifupi, lakini tatizo kubwa lilikuwa umaliziaji.

Katika kipindi cha kwanza washambuliaji wa timu hiyo walipiga mashuti makali matatu tu kuelekea langoni kwa Wamisri na mawili yalipigwa na winga wa kulia Stephen Mapunda ‘Garrincher’ aliyeng’ara katika mchezo huo na lingine lilipigwa na beki Omari Kapilima aliyepanda juu kuongeza nguvu ya mashambulizi.

Baada ya Al-Ahly kugundua udhaifu wa Majimaji, timu hiyo ilifanya shambulizi kali katika dakika ya 25 na kupata kona ambayo ilichongwa na Sayed Abdelhafiz, ilipanguliwa vibaya na golikipa Doyi Moke na mpira ulimkuta Hossam aliyepachika bao la kwanza. Bao hilo lilidumu hadi mapumziko.

Kipindi cha pili Al-Ahly, ilibadilika na kuanza kucheza kwa uelewano zaidi kuliko kipindi cha kwanza na ilifanikiwa kupata mabao mawili zaidi yote yakiwa yamefungwa na Hossam katika dakika ya 52 na 86.

Majimaji wangeweza kujipatia bao la kufutia machozi katika kipindi hicho, lakini kama ilivyokuwa kipindi cha kwanza washambuliaji walishindwa kupiga mashuti langoni kwa wapinzani wao.

Katika dakika ya 79, Mapunda alitoa pasi nzuri kwa Godfrey Kikumbizi ambaye alimsogezea mpira Maalim Saleh aliyeingia kuchukua nafasi ya David Mjanja, lakini alipiga mpira nje akiwa nadani ya mita 18.

Kadhalika Fortunatus Dello aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Ali Mopero alipiga shuti kali sekunde chache kabla ya mchezo kumalizika, lakini liligonga mwamba na kutoka nje.

Baada ya mchezo huo kumalizika, Kocha Mkuu wa Majimaji, Nzoyisaba Tauzany, alisema maandalizi duni na ugeni katika michuano ya kimataifa ndiyo kiini cha timu yake kufungwa.

“Hatukuwa na asilimia kubwa ya kushinda mchezo huo kutokana na hali halisi ya maandalizi yetu. Tumewekwa kwenye kambi ambayo haina maji wala umeme na pia wachezaji hawakupata huduma kikamilifu.

“Wachezaji hao ndio walipaswa kupambana na wenzao waliofikia Shelaton (sasa Serena Hoteli),” alisema Tauzany na kuongeza:

“Mbali na huduma hizo, tatizo lingine ni kwamba wachezaji wengi ni wageni katika michuano ya kimataifa. Nadhani mmeona wachezaji kama Stephen Mapunda, Willy Martin, David Mjanja na Omari Kapilima, wao wana uzoefu kiasi ukilinganisha na wengine. Kwa kweli hilo nalo limechangia kufungwa kwetu,” alisisitiza.

Naye aliyekuwa meneja wa timu ya Al-Ahly, Thabet El Bahat, alisema kuwa Majimaji ilicheza vizuri hususan winga Mapunda, kwani alikuwa hatari kwa timu yao, Stephen alicheza vizuri katikati, lakini alikosa ushirikiano na wenzake.

“Kitu kilichojionesha dhahiri kati ya timu mbili hizi ni kwamba Majimaji hawana uzoefu wakati sisi tuna uzoefu na michuano mikubwa. Tumepata nafasi chache na tumezitumia vyema,” alisema.

Aliyekuwa mfadhili wa klabu ya Simba, Azim Dewji, naye alisema uzoefu mdogo wa Majimaji ndio kiini cha kufungwa kwao katika mchezzo huo.

Pia, aliyekuwa kocha wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Ernest Mokake, alisema kocha wa Majimaji alipaswa kuwatumia wachezaji wazoefu kama Kelvin Haule (marehemu).

“Wachezaji wengi hawana uzoefu na wapo wenye uzoefu kama Kelvin Haule, kwanini hakumtumia?” Alihoji Mokake.

Mgeni rasmi katika mchezo huo alikuwa ni Mjumbe wa Kudumu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, marehemu Mzee Rashid Kawawa.

Kikosi cha Majimaji: Doyi Moke, Omari Kapilima, Omari Hussein, Amri Said, Willy Martin ‘Gari Kubwa’, Ambrose Mwingira, Stephen Mapunda ‘Garrincher’, Twaha Omari/Said Mshamu, Godfrey Kikumbizi, Ali Mopero/Fortunatus Dello na David Mjanja/Maalim Saleh.

Kikosi cha Al-Ahly: Essam Elhadar, Ebrahim Hassan, Ibrahim Said, Mohamed Youssef, Hussein Shoukry, Saved Abdelhafiz, Yussin Yakub/Osma Oraby, Hishar Hanafi/Hady Kashada, Hossam Hassan, Yasser Rayan na Mahir/Alaf Ibrahim.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -