Wednesday, October 28, 2020

UNAMJUA MWENZAKO VIZURI? KWANINI HUJUI ANAYOPENDA?

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

WEWE na mwenzako ni kama mwili mmoja. Kwa sababu hiyo na nyingine nyingi ndiyo maana mbali na kuwa na mamlaka na mwili wako, ila mwenzako pia ana jukumu hilo.

Unaweza kuona nguo fulani dukani na ukanunua ila kutokana na sababu atakazotoa unaweza usiivae.

Na siyo kuwa unaacha kwa sababu unamuogopa, hapana. Ila kuna heshima na hisia fulani baina yenu zinazofanya kuona kama ukikataa jambo hilo kwa mwenzako hautakuwa na furaha kamili ya kuvaa nguo husika.

Maana furaha yako inategemea namna anavyokutazama na namna anavyokuchukulia. Ikiwa mwenzako ana mtazamo hasi juu yako na wewe unalijua hilo, itakuwa ngumu sana wewe kuwa katika hali ya amani na furaha. Halikadhalika na kwa mwenzako, ikiwa na wewe una mtazamo hasi juu yake hata siku moja hawezi kuwa na furaha na amani katika nafsi yake.

Na ili raha na amani kamili ya mahusiano iweze kupatikana, inabidi kila mmoja amjue mwenzake vizuri. Ikiwa unamjua mwenzako vizuri mahusiano yako hayawezi kuwa na shida na mashaka mengi. Utajua ufanye nini ili awe vipi, utajua ukifanya nini atasema nini! Unajua ni kitu gani anapenda mwenzako?

Ikiwa kweli unahitaji utulivu na furaha ya kweli katika mahusiano yako, kumjua mwenzako ni suala muhimu sana. Katika kumjua na kumuelewa ndipo utaweza kujua vizuri namna ya kufanya mahusiano yako yawe unavyotaka wewe. Nini anapenda mwenzako?

Ikiwa hujui ni vitu gani anapenda mwenzako basi unajiweka katika mazingira ya kumfanyia mambo ya kumkera na kumdhoofisha kihisia. Ni kwa vipi utaepukana na suala hili ikiwa hujui ni kwa vitu gani huwa anakuwa katika hali gani?

Mbali na kumfanya kuwa na furaha na amani, ila kumjua mwenzako pia itachangia kumfanya ajue ni kwa namna gani alivyo na umuhimu katika maisha yako.

Ugomvi mwingi unaotokea katika mahusiano mbali na sababu nyingine, ila pia huchangiwa na watu kutojuliana vizuri na matokeo yake unakuta mtu anafanya mambo ambayo mwenzake hayapendi. Unafikiri kwanini watu huachana ilhali wakati mwingine huwa bado wanapendana?

Ni kwa sababu kila siku huumizwa na baadhi ya mambo na kuona kama anafukuzwa kwa mlango mwingine. Amani ya mpenzi wako inakutegemea sana wewe, kama ilivyo wewe kwake. Ila pia una jukumu la kurekebisha ama kuzamisha mapenzi yako ikiwa hautakuwa makini katika matendo na maneno yako. Na kimsingi umakini  baina yenu unajengwa kutokana na kiwango cha uelewa kwa mwenzako.

Yafanye mahusiano yako kama pepo ya mapenzi kwa matendo yako. Chunguza vitu vyote anavyopenda mwenzako. Isiishie tu katika vyakula na mavazi, hata aina ya vitu anavyoshabikia. Kwa kufanya hivi, unakuwa unamsogeza karibu zaidi katika dunia yako ya mapenzi na kumfanya aone kwake wewe ni kila kitu.

Wengi wanawaumiza wenzao si kwa sababu wanapenda kuwafanyia hivyo, hapana. Ila ni kwa kuwa hawajui ni vitu gani wenzao wanapenda.

Pia hapa inabidi uwe makini na mjanja kwa maana mapenzi ya vitu kwa mtu yanakwenda yakitofautiana. Kama ulikuwa na Jack anapenda mtu mkimya usidhani hata Hassan anapenda mtu wa aina hiyo. Hapa inabidi uwe makini na mjanja kumsoma mwenzako na siyo kutaka kuishi kwa mazoea.

Ikiwa utafanikiwa kumsoma kwa makini na kugundua aina ya vitu vyote anavyopenda, hata ukiacha kuvifanya vyote ila utakuwa umetengeneza kitu kitakacholeta amani na furaha sana katika mahusiano yako.

ramadhanimasenga@yahoo.com 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -