Sunday, January 17, 2021

Unamjua wa kuamua furaha yako?

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

KILA aliye katika mahusiano ya kimapenzi huamini alie naye ndiye hasa ana jukumu la kumfanya ajihisi amani, furaha na wa thamani. Ni kweli. Hakuna mtu mwingine kando ya wazazi wako anayetakiwa kukupa amani na furaha kama si mpenzi wako.

Mpenzi wako ni mtu wa kwanza kukupa amani na furaha baada ya wazazi wako. Sahau kuhusu watoto wako, mtoto ni tumaini la mzazi, ila ni mpenzi ambaye huweza kujenga amani na furaha kwako. Mtoto anaweza kukuhangaisha kutwa nzima umnunulie jambo fulani hata kama umesema huna hela na asijali, ila mpenzi hawezi kufanya hivyo.

Katika mapenzi ya kweli, mhusika akimwona mwenzake yuko katika hali mbaya ya kiafya ama kiuchumi, hali ile uihisi hata yeye. Hata siku moja mpenzi wako halisi hawezi kukulazimisha umpe hela hata kama umesema huna na mazingira yanaonesha hivyo.

Mpenzi huwa tulizo katika wahka, huwa pozo katika joto la kimaisha. Siku zote yeye huwa mtu wa kwanza kuhisi maumivu yako kuliko mwingine. Swali, je, unamjua mtu wa kuamua furaha yako?

Furaha yako inatakiwa kuishi katika maneno na matendo ya mwenzako. Japo ni kweli furaha yako ni jukumu lako binafsi ila katika mapenzi dhana hii inakosa nguvu. Ukosefu wa  nguvu unatokana na ukweli kwamba ukiwa katika mapenzi unapaswa kumwangalia mwenzako kwa karibu kwa anachofanya na anachosema.

Kwa hali hiyo ya kumwangalia mpenzi wako kwa jicho la karibu, hujitokeza jambo jipya katika akili yako linalofanya hali yako ya furaha isiwe jukumu lako pekee. Jambo hilo ni kuishi na picha ya mwenzako katika akili yako kwa kila jambo unalofanya.

Hii kitu inakuwa inakutoa katika hali ya peke yako na kukufanya uwe katika hali yenu. Yaani unajikuta huwazi kitu katika mtindo binfasi bali unawaza kitu katika mtindo shirikishi. Ukiwaza kujenga nyumba, picha inakujia katika akili yako kuwa katika nyumba hiyo utakuwa wewe na mwenzko.

Ukitaka  kununua nguo, unaiona  kwanza katika akili yako mwenzako atakavyofurahia na namna utakavyopendeza. Unajua furaha yako inaamuliwa na nani?

Kama mtu kaamua kwa dhati kuinga katika Mapenzi, anapaswa kufahamu kuwa kwa zaidi ya asilimia hamsini furaha ya mwenzako inamtegemea sana yeye. Kwa mantiki hiyo, kila analofanya anatakiwa kumfikiria na mwenzake. Ni ujinga na uzuzu wa kimapenzi mtu kujitazama zaidi yeye katika mambo yake bila kujali mwenzake atamchukuliaje.

Bila mwenzako kufurahia namna ulivyo, namna unavyofanya mambo yako, jua bado hauko katika mahusiano halisi ya kimapenzi. Mahusiano halisi ya kimapenzi yanatakiwa kila mmoja ajione ana dhima kwa mwenzake ya kumpa amani, furaha na raha.

Kama mwenzako anasababisha wewe kulia kila siku, kama mwenzako ni mwepesi kukwepa majukumu yake ila ni hodari kutaka wewe utimize majukumu yako kwake, mtazame katika jicho la umakini zaidi.

Vijana  wengi wa kileo wanaitwa wapenzi ila kiuhalisia sio, basi wanaitwa hivyo kulaghaika ili wenzao waweze kutimiza malengo yao kwao. Jitazame wewe si mmoja wa watu hao?

Njia ya kujua kama wewe ni mmoja wao ama sio, ni nyepesi sana. Angalia furaha yako inasababishwa na yeye kwa asilimia ngapi? Tazama huzuni yako inamalizwa na yeye kwa asilimia ngapi?

Kama asilimia kubwa ya machozi yako yanasababishwa na yeye, jua hauko katika mahusiano halisi. Mahusiano halisi ni yale yanayomfanya mhusika kujiona wa kipekee kwa furaha na raha anazopewa.

Kama mwenzako anakwambia ‘nakupenda’ kisha anaenda kinyume na maneno yake, jua mwenzako ni mmoja kati ya wale malaghai yanayotumia neno mapenzi kutimiza malengo yao.

Mahusiano halisi ya kimpenzi yanapaswa kukupa amani na raha. Mahusiano halisi ni yale yanayomfanya mtu anayepaswa kuwa na huzuni kuwa na furaha na kujiona ana bahati kubwa katika maisha yake. Mpenzi wako anakufanya kuwa na amani na raha? Mpenzi wako anajua kuwa  matatizo yako ni yake na anaonekana kuyabeba?

Ukiona uko na mtu ambaye anajiona yeye ndiye mwenye shida zaidi kuliko wewe na mwenye kupenda kulaumu bila kukuangalia uko katika hali gani, mtazame kwa jicho pana zaidi. Mpenzi halisi hapendi kukufanya wewe kuwa kitega uchumi ama suluhu ya matatizo yake huku yako akikwepa.

Watu walio katika mahusiano halisi ya kimapenzi huoneana huruma, hujidai kwa walio nao na hujihisi faraja. Ukiona mwenzako hajali kuhusu huzuni yako ni yuko tayari kuisababisha ili tu yeye afurahi, jua upo katika eneo lisilo sahihi kwako.

Anayesababisha wewe ufurahi hata katika mazingira magumu huyo ni mtu sahihi kwako, anayejitazama yeye tu bila kujali hali yako, huyo hafai kuitwa mpenzi, labda umuite jina jingine. Mpenzi wa kweli hutamani mwenzake awe na furaha na raha kutokana na yeye.

ramadhanimasenga@yahoo.com

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -