Monday, October 26, 2020

UNAMTAZAMA VIZURI AISHI MANULA?

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA OSCAR OSCAR

UKIAMBIWA utaje sababu za ukuta wa Azam FC kuwa imara katika kipindi cha misimu mitatu ya hivi karibuni, wengi watakumbuka ubora wa walinzi wa kati, Pascal Serge Wawa na Agrey Moris.

Bado nafasi ya mlinda mlango unaweza usiione kwa jicho la kawaida. Ukiendelea kuuliza swali hilo hilo, utatajiwa pia jina la mlinzi, Shomari Kapombe. Jina la Aishi Manula bado linaendelea kujificha. Ukiambiwa utaje shujaa wa mechi ya Fainali ya Mapinduzi Cup mwaka huu kule visiwani Zanzibar, wengi watamtaja Himid Mao Mkami.

Unaijua sababu? Ni rahisi tu. Huyu ndiye mfungaji wa goli lililoipatia Azam FC ubingwa wa michuano hiyo. Na hata ukiuliza Mfalme wa mechi ya wikiendi  iliyopita baina ya Simba na Azam FC, wengi watasema ni John Bocco. Sababu ni zile zile kama za Himid Mao.

Ni kama Aishi Manula hayupo vile kikosini, ni kama si mchezaji wa kikosi cha kwanza. Hii ndiyo changamoto ya nafasi ya mlinda mlango katika mchezo wa soka. Unaweza ukaokoa michomo 10 kwenye mechi na watu wasijali. Lakini ukifungwa goli moja tu, dunia nzima inaweza kukuangukia. Nafasi ya lawama zaidi kwenye mchezo wa soka!

Aishi Manula ni moja kati ya mashujaa wa Azam FC, moja kati ya wachezaji nguzo ndani ya chama hicho cha matajiri wa Jiji la Dar es Saaam. Kwa bahati mbaya, nafasi anayocheza inawafanya watu wengi wasimpe sifa anayostahili.

Si nafasi inayozikonga sana mioyo ya mashabiki wa soka. Dunia imejikita zaidi kuangalia wafungaji wa magoli na wanaotoa pasi za mwisho.Dunia ya soka inawasahau sana magolikipa. Hakuna anayejali umekaa langoni kwa dakika ngapi bila kuruhusu goli. Hakuna anayekumbuka baada ya mechi idadi ya mashuti aliyopigiwa mlinda mlango.

Watu wataondoka na jina la mfungaji tu, hayo mengine yanabaki pale pale uwanjani. Manula ni aina ya magolikipa wenye maumbo yasiyotisha langoni, lakini hajawahi kuiangusha timu yake. Anajua muda wa kuliacha lango, anajua muda wa kumwacha adui amalizane na walinzi wake. Ni mara chache sana dunia ya soka huwakumbuka walinda mlango.

Soko la magolikipa linaonekana kuwa ngumu zaidi hasa barani Afrika na hasa unapokuwa na umbo dogo kama la Aishi Manula. Ni umbo kama la Kipa wa Spurs, Hugo Lloris na  Kipa wa Porto, Iker Casillas, lakini hao niliowataja wana bahati ya kuzaliwa mwenye dunia ya kuanza. Maumbo kama ya Kipa wa Zamani wa Simba, Juma Kasseja, ni kazi sana kuuzika nje na hasa barani Ulaya.

Ukirejea kwenye mchezo baina ya Simba na Azam FC mwishoni mwa juma lililopita, utagundua kwamba Aishi Manula alikuwa kikwazo kikubwa kwa Simba kupoteza mchezo ule. Ni moja ya wachezaji waliokuwa kwenye kiwango bora kabisa ingawa dunia ya soka iliondoka uwanjani na jina la John Bocco. Hii ndiyo changamoto ya nafasi anayocheza Aishi Manula. Kama Azam FC watafika mbali msimu huu kwenye Kombe la Shirikisho barani Afrika, huenda Manula akapata heshima anayostahili.

Hata unapoitazama Bayern Munich, ni rahisi sana kuanza na Robert Lewandowski kuliko Manuel Neuer. Hata unapoitazama Chelsea, utaanza na Diego Costa kabla ya Thibaut Courtois. Ndiyo dunia ya soka ilivyo kwa sasa. Magoli kwanza, mengine baadaye. Huwezi kuanza kuizungumzia Arsenal kwa kumtaja Peter Cech, watu hawatakuelewa.

Alexies Sanchez kwanza, wengine baadaye. Pamoja na nafasi hii kutozingatiwa sana na mashabiki wa soka, lakini haiondoi ukweli kwamba hapo ndipo ulipo msingi wa timu. Na kwa mantiki hiyo basi, tuseme tu kuwa msingi wa Azam FC umejengwa kupitia Aishi Manula.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -