Wednesday, November 25, 2020

UNAPENDA KUKASIRIKA? SOMA HAPA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

KUKASIRIKA ni hali yakuonesha kutopendezwa na jambo au neno uliloambiwa au kufanyiwa. Mara nyingine hali hii huchagia kumfanya mhusika kujirekebisha au kujirudi baada ya kwazo alilokufanyia.

Si mara zote mtu hutakiwa kuongea tu maneno, hata kufanya hivi pia huchangia katika mabadiliko ya mhusika. Na pia kila binadamu huwa na hali hii.

Kuwa na hali hii si mapungufu wala ujinga ila ni hali ya kuonesha hisia zako kutokana na jambo fulani. Hisia za namna hii ni kama zile za kufurahi tu. Yaani mtu akifurahishwa au kupendezwa sana na jambo mwenyewe hujikuta akicheka ama kutabasamu. Ni kama mtu akiwa na hasira ‘automatically’ hujikuta na hali ya kukasirika na kuwa tofauti.

Japo huo ndio ukweli ila hali kama hii kuna watu hupenda kuiigiza kiuthabiti. Kwa maneno mengine ni kuwa mtu huwa pengine hajafanyiwa kitendo cha kukera ila huamua tu kuwa katika hali ya namna hii.

Unaweza kuwa mmojawapo. Pia huenda kila unapofanya hivi mwenzako hujikuta akiwa katika hali ya wasiwasi na kukuomba sana msamaha. Kwa hili huenda ukawa unafurahi na kuona unamuweza sana mwenzako. Pia huenda huwa unatumia nafasi hii katika kuomba ama kuhitaji kitu kwa maana katika namna hii mwezako huenda huwa katika wasiwasi wa kukupoteza na hujikuta akifanya tu kukuridhisha. Huwa unafurahi eeeeh?

Ila umeshawahi kujiuliza hali hiyo itaendelea mpaka lini? Unafikiri pale mwenzako anapokuwa na wasiwasi mpaka ikafikia hatua ya kukufanyia mambo au kukufanyia vitu nje ya utaratibu wake wa kawaida huwa anafurahia?

Ila mwenzako hawezi kufurahia hali hii. Kila mmoja anayefanyiwa hivyo hulazimika kufanya yote anayotakiwa kumfanyia mwenzake ili afurahi huku moyo wake ukiwa unaumia.

Huumia na kuona kama hana thamani wala umuhimu stahiki kwa mhusika. Katika hali hii akili yake huwa inatafuta suluhisho na njia ya kudhibiti hali hii. Unajua njia ya kwanza huwa ipi?

Huanza kupunguza ukaribu na wewe kwa kuamini huenda ukaribu wenu wa mara kwa mara ndiyo huwa chanzo cha ugomvi ambao kimsingi huwa haupo ila huamua tu kukasirika kwa mambo yako mwenyewe.

Kwa kufanya hivi kama mlikuwa mna mazoea ya kukutana mara kwa mara atajikuta akiwa na upweke kwa kuwa kakatisha ghafla kuonana kwenu kwa sababu ya kuhofia kukukwaza.

Hapa ndipo huanza kutafuta mbinu ya kukupunguza katika akili yake ili asiwe anaumizwa na mawazo mengi juu yako. Kama akifanikiwa katika hili, tambua hata moyoni mwake pia utakuwa hauna hadhi uliyokuwa nayo zamani. Unajua kwanini?

Kwa sababu kitendo chake cha kukupunguza katika akili yake kitaenda sambamba na kukuona si mtu wa kumpa furaha muda mwingi kwa maana muda mwingi mkiwa pamoja huwa unakasirika.

Ndiyo hapa utakapoanza kulalamika kikweli kweli huku mwenzako akishindwa kukuthamni kama ilivyokuwa mwanzo kwa maana hauna thamani kama uliyokuwa nayo hapo mwanzo.

Kuna raha sana kuwa na furaha unapokuwa na mwenza wako. Kwa maana hali hiyo humfanya ajione kwako ana umuhimu kiasi gani mpaka unajihisi raha kuwa naye karibu.

Ndiyo, kukasirika kupo ila kukasirika kwa makusudi ni ujinga. Utaona ni kitendo kidogo ila jua ndicho kitakachokuja kuharibu raha na amani ya mahusiano yako. Kwa leo itoshee hapa.

ramadhanimasenga@yahoo.com 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -