Friday, October 23, 2020

UNAWEZA KUMPENDA MTU SIKU YA KWANZA KUKUTANA NAYE?

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NDUGU wasomaji, karibuni sana katika safu hii ya uhusiano wa kimapenzi ambayo hutoka kila Jumanne na Jumamosi.

Awali ya yote, nitoe shukrani zangu za dhati kwa wote ambao wamekuwa wakichangia mada zangu na kwamba nimefarijika sana kwa jinsi wasomaji wa BINGWA walivyozipokea zikionekana kuwagusa mno.

Baada ya salamu hizo, twende katika mada ya leo inayosomeka: ‘Unaweza kumpenda mtu siku ya kwanza kukutana naye?’

Neno nakupenda huwa ni rahisi sana kulitamka, lakini ni vigumu mno kuamini iwapo anayelitamka anamaanisha, yaani ni kweli anampenda kutoka moyoni anayemtamkia maneno hayo.

Kiuhalisia, wapo wanaochanganya maneno mawili, kupenda na kutamani. Kumpenda mtu ni tofauti kabisa na kupendwa.

Unaweza kukuta mvulana anakutana na msichana kwa mara ya kwanza na kumtamjia kuwa anampenda na msichana huyo kuamini kwamba anapendwa kweli.

Kwa hali ya kawaida, huwezi kukutana na mtu kwa mara ya kwanza na kumpeda. Huyo utakuwa umemtamani tu aidha kutokana na sura yake, rangi, uzuri, kimo, umbo, maisha, uzungumzaji, umaarufu, uvaaji, nywele na mambo mengine kama hayo.

Kumpenda mtu hutokea baada ya kumshiba kutoka moyoni. Kwamba umekaa naye kwa muda mrefu na muhusika kuuteka moyo wako kutokana na matendo yake dhidi yako au kwa wengine.

Mathalani, unaweza kuwa na urafiki na mtu kwa muda mrefu ukabaini anapenda sana watoto, kiasi cha kutamani awe mzazi mwenzio ukitegemea watoto wako kuonyeshwa upendo wa hali ya juu, lakini ikiwa ni baada ya nafsi yako kuridhishwa bila shaka kuwa muhusika hakuwa akiigiza ili kukuteka kirahisi.

Binafsi nimekuwa mzito kuamini kwamba unaweza kukutana na mtu siku ya kwanza na kumpenda japo wapo wanaoamini hivyo.

Ili uwe umempenda mtu, inashauriwa uwe karibu naye kwa zaidi ya miezi sita hadi miaka kiasi cha kufahamu kasoro zake, ubora wake na iwapo sifa na kasoro zake hizo vitaendana na vyako.

Lakini wapo wanaoamini unaweza kumpenda mtu siku ya kwanza kuonana naye iwapo utabaini ana sifa za mpenzi ambazo umekuwa ukizisaka kwa muda mrefu bila mafanikio.

Mtaalamu mmoja wa mambo ya mapenzi anasema: “Unahitaji kuanzia wiki mbili, miezi sita na hata mwaka mmoja kufahamu kama unampenda mtu fulani. Lakini ili uwe salama zaidi, unatakiwa kuchukua miezi mitatu hadi sita kumpenda mtu baada ya kumsoma vilivyo.”

Mtaalamu mwingine wa mambo ya mahusiano alisema: “Unaweza kumpenda mtu baada ya mwezi mmoja au hata miwili baada ya kuwa naye pamoja na kuona ana sifa unazozihitaji, huwezi kumpenda mtu bila kumsoma vya kutosha.”

Mtaalamu mwingine wa mapenzi, alisema: “Sidhani kama unaweza kumpenda mtu ndani ya sekunde, wiki, mwezi…. Ili uwe umempenda mtu kwa dhati kabisa, inachukua miaka baada ya kumsoma nje ndani na kuona ndiye chaguo lako hasa.”

Ndugu wasomaji, hebu nipe maoni yako juu ya mada hii; kwamba unaweza kumpenda mtu siku ya kwanza kukutana naye? Kwa maoni, tuwasiliane kwa namba ya simu hapo juu au anuani pepe michietz@yahoo.com.

Tukutane Jumamosi ambapo nitawaletea mada kali zaidi. Ahsanteni.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -