Monday, November 30, 2020

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU [106]

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

Ilipoishia Jumanne

 DEREVA wa taksi hiyo aliwapeleka hoteli iliyokuwa karibu na barabara ya kwenda mji wa Masjid, ambako huko kuna ikulu ya Rais. Baada ya dakika 15, Roika na Shazayi walikuwa wamefika hotelini hapo, ambapo walichukua chumba cha ghorofa ya pili.

Shazayi alimkumbatia Roika na kulia sana kwenye kifua chake. Roika alimfuta machozi na kumbusu.

SASA ENDELEA

Nguvu ya mapenzi ilikuwa kubwa kwa wawili hao. Roika aliamini bila Shazayi hawezi kuishi na Shazayi aliamini bila Roika hawezi kuishi. Siku hiyo Shazayi alivaa vizuri, hakika alipendeza na kuonekana si mwanamke wa kawaida. Roika naye alivaa suti nyeusi zilizomfanya kuonekana mwanamume wa tofauti. Kwani muda wa kwenda ikulu ya Rais Galim Halim ulikuwa umefika.

Yakiwa yamebaki masaa 12  ili Swaba wafike hatua ya kumchinja mtoto wa Rais, vyombo mbalimbali vya habari duniani kote, vilikuwa makini kusubiria taarifa hiyo ili viweze kuuhabarisha ulimwengu. Na wakati huo huo vilikuwa makini pia kusubiria kauli ya Rais wa Pakistani kutoka ikulu ya juu alichoamua kuhusu mwanaye. Amani ilikuwa imetoweka kwa raia wa Pakistani, watu wanaompenda Shazayi.

Pindi Roika na Shazayi walipokuwa wakijiandaa kutoka hotelini, walisikia habari iliyokuwa ikirushwa kupitia televisheni ya taifa kwenye runinga iliyokuwa pale hotelini. Shazayi alichanganyikiwa kwani hakuwa akijua kama wamechelewa kiasi kile.

“Roika mpenzi tusipowahi, baba yangu anaweza kuwapa Swaba kile wanachokitaka. Kwani hawezi kuniacha niuawe, hivyo atawapa wakitakacho bila kujua kuwa mimi siko mikononi mwao.”

“Ni kweli mpenzi, lakini kwa nini usimpigie simu baba yako kumwambia kuwa uko sehemu fulani? nashangaa hatukuwa na wazo hilo.”

“Kwa kawaida baba na mama, huwa wanabadilisha namba za simu zao kila baada ya miezi minne. Yaani namba mpya. Hii ni kutokana na usalama wa ikulu. Na wakati mimi natoka nyumbani kwenda kukutafuta wewe, tayari baba na mama walishakuwa wamebadilisha namba zao za simu. Nilikuwa nazo kwenye simu ambayo niliiacha nyumbani na sikuwa nimezikalili kichwani,” aliongea Shazayi.

“Kwa nini usipige simu ya ofisini kwake?”

“Baba Alisha nikanya kuwa ninapokuwa na shida nisitumie simu ya mezani ya ikulu kwani ni hatari. Kwa sababu kuna watu wabaya wako ikulu ambao sisi hatuwajui. Kwa kipindi hichi ndio hatari zaidi labda nibahatishe yeye akiwa ofisini, Roika mpenzi fanya hima twende, baba akikuona ni vizuri zaidi kwa usalama wa mapenzi yetu.”

“Sawa tuondoke,’ aliongea Roika na kumkumbatia Shazayi.”

Walishuka kutoka gholofani hadi chini. Walimkuta dereva taksi akiwasubiri, kwenye eneo la maegesho ya magari. Hakuna mtu yoyote aliyewajua.

“Tupeleke masjid,” aliongea Roika.

Dereva aliwasha gari na kutoka nje ya viunga vya hoteli hiyo. Baada ya dakika 20, gari lilianza kuingia kwenye mji huo mdogo, uliokuwa na ulinzi kila mahali. Wanaoishi mji huo walikuwa ni matajiri na viongozi mbalimbali wa serikali. Walipofika eneo lenye ulinzi zaidi, ambalo ndio mwanzo wa kuingia barabara ya ikulu, polisi walilisimamisha gari lao.

“Bila shaka mnakwenda ikulu?” aliuliza afisa wa polisi.

“Ndio,” alijibu Shazayi.

“Tunahitaji kuwakagua.”

Askari aliposema hivyo, Shazayi alimtazama Roika na kisha akamgeukia tena askari. Taratibu aliiivua nikabu na kuionesha sura yake ili kujitambulisha. Askari huyo alipatwa na mshtuko mkubwa baada ya kuomuona mtoto wa Rais aambaye anajua kuwa anashikiliwa na kikosi cha kigaidi cha Swaba.

“Madam ni wewe?”

“Bila shaka, niruhusu nipite,” alijibu Shazayi.

Upesi alimpigia Shazayi saluti na kuliruhusu gari kupita. Baada ya kupita askari huyo aliwapiga simu askari wa kitengo kikuu cha ulinzi wa ikulu. Taarifa zilisambaa kwa muda mfupi kwenye maeneo yote ya ikulu. Taarifa hiyo ilifika haraka hadi kwa mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama kuwa mtoto wa Rais anaingia ikulu. Mkuu huyo wa majeshi aliagiza vikosi maalum, kujongea ikulu.

Rais Galim akiwa chumbani, akiwa pamoja na mke wake aliyekuwa kwenye hali mbaya, kutokana na taarifa za binti yake kuwa mikononi mwa Swaba, alikuwa akimbembeleza mke wake kula chakula kwani ni siku ya pili, alikuwa hajapata chakula cha kutosha. Huzuni ilikuwa imetanda kwa wawili hao wapendanao.

“Mke wangu naomba ule unafikiri bila kula utaweza kuishi?” aliongea Rais Galim kwa huzuni huku akiwa amekishika kijiko cha supu.

“Namtaka mwanangu,” alijibu mke wake kwa tabu huku akitokwa na machozi.

“Usijali leo ninakwenda kuwapa Swaba kile wanachokitaka nafikiri jioni wanatamuachia mwanetu.”

“Ukifanya hivyo, nitakula chakula,” alijibu mke wake.

Wakiwa kwenye maongezi hayo, maongezi yaliotawaliwa  huzuni, mudumu wa ikulu aliwagongea mlango. Rais Galim alikwenda kufungua.

“Mheshimiwa kuna taarifa kutoka idara ya ulinzi,” aliongea muhudumu huyo.

“Taarifa gani?” aliuliza Galim.

“Madam Shazayi anakuja ikulu.”

Rais Galim alishtuka, macho yalimtoka vilivyo.

“Unawazimu?” aliuliza Galim.

“Ni kweli mheshimiwa, hii nitaarifa niliyopewa na sajenti Mahamud, hata hivyo simu ya ofisini kwako inaita.”

Upesi Galim alikimbia kuelekea ofisini kwake, ofisi iliyokuwa umbali wa hatu 20 ndani ya ikulu. Alikuta simu ya mezani ikiita, kabla hajaipokea,  simu yake ya mkononi nayo ilianza kuita, huku ujumbe mfupi wa maneno ukiingia kwa fujo.

Aliipokea simu yake ya mkononi.

“Mheshimiwa madam Shazayi, binti yako yuko geti kuu anaingia Ikulu,” aliongea kamisina wa idara ya ulinzi.

Rais Galim alionekana kuchanganyikiwa, bado hakuwa na nguvu ya kuamini taarifa za mwanaye kuja ikulu.

Nini kitafuatia usikose kesho

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -