Tuesday, December 1, 2020

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU [110]

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

Ilipoishia jana

WAKIWA katika maongezi hayo, Shazayi alikuja pale akiwa mwenye furaha. Lakini alimkuta Roika akiwa na huzuni na mwenye woga mwingi. Rais Galim alipogeuka kumtazama binti yake, aliona amekosa furaha ya ghafla mara tu alipokuwa amemwona Roika akiwa na sura ya woga na huzuni kubwa.

SASA ENDELEA

Lakini Rais Galim alimuuliza mwanaye.

“Mama yako anaendeleaje?”

“ Mungu ni mkubwa amekula chakula vizuri,” alijibu Shazayi kwa furaha.

“Nakushukuru mwanangu kwa kumuokoa mke wangu. Naamini sasa atarudi kwenye uzima.”

“Pole sana muheshimiwa kwa kumuuguza mke wako kwa nguvu zote. Ingawa ulikosa matumaini,” aliongea Roika kwa tabasamu hafifu.

Roika alionekana kukosa furaha kutokana na yale maswali aliyokuwa akiulizwa na Rais Galim, kabla Shazayi kuja pale sebuleni. Maswali yale yalionekana kabisa kuwa yanaweza kubomoa uhusiano wake na Shazayi. Kwa kuwa hakuwa amelijua lengo la Rais Galim kumuuliza vile. Ukizingatia Roika ni mtu mweusi, yaani mwafrika, aliona kumuoa mwanamke wa kiarabu  ni ngumu, hivyo alihitaji nguvu ya ziada, japokuwa  alikuwa akiamini kuwa, penzi lake na Shazayi haliwezi kuvunjika kwa sababu, Mungu wa mbinguni ndiye aliyewakutanisha yeye na mwanamke huyo wa kipakistani. Moyoni alikuwa akimuomba Mungu kuwa amuingie Rais Galim ili asiweze kuukataa uhusiano wao.

Shazayi aliingiwa na wasiwasi baada ya kumuona Roika akiwa amekosa furaha, tofauti na alivyomuacha hapo mwanzo. Alipiga hatua hadi kwenye kochi alilokuwa amekaa Roika.

“Roika mbona umekosa furaha? usiogope hapa ni kama kwako uwe na amani,” aliongea Shazayi huku akiwa amemshika Roika mgongoni.

Rais Galim aliwatazama kwa sekunde kadhaa, kisha akasema.

“Tafadhari nakwenda chumbani.”

Aliposema hivyo, aliinuka na kuelekea chumbani akiwaacha na maswali fulani vichwani mwao. Mara tu Rais Galim alipofika chumbani, huku nyuma Roika alianza kutokwa na machozi. Shazayi alipatwa na mshangao mkubwa.

“Nini tena mpenzi mbona unalia?” aliuliza Shazayi huku akimshika Roika kichwani.

Kama mtoto mdogo Roika alijilaza kwenye kifua cha Shazayi, huku akilia.

“Tafadhari Shazayi, fanya yote ili mimi niwe na wewe. Mshawishi baba yako kwa kila kitu ili akubali nikuoe. Endapo nitakukosa, sitaiona thamani ya maisha. Kumbuka nilimuahidi mama yangu kuwa nitakupekea akakuone. Leo sitaki kuivunja ahadi,” aliongea Roika akilia sana.

Hakika Shazayi alisikia maumivu makubwa sana moyoni, hakujua ni kwa nini Roika alikuwa amezungumza yale. Hakujua baba yake alikuwa amemwambia nini Roika. Upesi alimkubatia Roika kichwani na kumsihi asilie.

“Usilie Kipenzi changu, kila kitu kitakuwa sawa, hata kama baba yangu atapinga uhusiano wetu, lakini kumbuka kuwa Mungu ndiye aliyetuunganisha, nitammueleza jinsi ambavyo siwezi kuishi bila wewe, sawa mpenzi wala usijali.”

Shazayi alimfuta Roika machozi na kumbusu kwenye paji lake la uso. Baadae Roika alijitoa kifuani kwa Shazayi, mahali anapopenda kulala siku zote. Punde tu Rais Galim, alirudi pale sebuleni. Naye alishtuka kuwaona wakiwa na huzuni iliyojificha. Alipiga hatua na kwenda kukaa kwenye kiti. Aliwatazama kwa sekunde kadhaa za ukimya na kisha akamuuliza binti yake.

“Mwanangu, Mr Roika amenieleza kila kitu kilichopelekea wewe kupotea na kuhusishwa kuwa unashikiliwa na Swaba. Je yote aliyonieleza ni sahihi?”

Shazayi alikawia kujibu swali hilo, alimtazama Roika na kisha alimgeukia baba yake.

“Ndio baba ni sahihi,” alijibu Shazayi kwa uwoga.

Rais Galim alikaa kimya kwa muda kidogo na kisha akawaambia.

“Msiogope najua mnahofia kuwa mimi ninaweza kuvunja mapenzi yenu. Kamwe siwezi kufanya hivyo.”

Aliposema hivyo, wote walishtuka kwa mshtuko wa furaha. Hakika walikuwa na hamu ya kusikia kile atachokiendelea kukisema Rais Galim.

“Kwa sababu nimegundua kuwa, mwanangu ulifanya mengi kwa ajili  Mr Roika na  Mr Roika ulifanya mengi kwa ajili ya mwanangu. Endapo nitaipinga ndoa yenu ni sawa na kumpinga Mungu aliyemuokoa mke wangu. Tabia zenu zinafanana kama ambavyo jarida la The Century Human lilivyosema. Naungana na Mungu kuibariki ndoa yenu.”

Kama mtu aliyechanganyikiwa, Shazayi alimrukia baba yake na kumkumbatia kwa nguvu. Roika alitabasamu huku akitokwa na machozi. Siri ya furaha aliyokuwa nayo, moyo wake ndio uliokuwa ukijua. Alijiona ni kama malaika. Aliinuka kwenye kochi na kwenda kumgusa miguu Rais Galim. Lakini Galim alikataa kuinamiwa, alimuinua Roika na kumwambia.

“Asante kwa kumleta binti yangu.”

Aliposema hivyo, alimbusu Shazayi kwenye paji la uso na kuwaambia jambo lililowashtua kidogo.

“Lakini mwanangu, licha ya mimi kusema hayo, jua sina nguvu ya kupinga  uamuzi wa mama yako atakao kuwa ameamu kuhusu nyinyi. Mke wangu naye anamaamuzi yake, hivyo nendeni mkamshawishi. Binafsi mimi nimeridhia mwanagu kuolewa na mwanaume shujaa kama Mr Roika.”

Rais Galim aliposema hivyo, aliwaacha pale sebureni na kuelelekea chumba chake cha habari. Huko aliwaita waandishi wote wa vyombo vyote vya habari.

Huku nyuma Roika na Shazayi walikumbatiana kwa furaha kubwa isiyoelezeka. Hakika Mungu alikuwa kando yao. Baadae Shazayi alimpeleka Roika chumbani kwa mama yake. Ilikuwa ni ajabu, kumkuta mama yake akiwa ameketi kitandani. Ilimaanisha kuwa mama yake alikuwa amepona ghafla. Shazayi alimkimbilia mama yake na kumkumbatia.

“Mama umepona?”

“Nimepona mwanangu. Natamani kwenda chumba cha Swala, kwani ni muda kidogo sijakwenda kusujudu,” aliongea Salma.

“Mama kabla ya hilo, nakuomba nikutambulishe mtu muhimu kwenye maisha yangu,” aliongea Shazayi huku akimshika mkono Roika.

Alimsogeza hadi pale kitandani kwa Salma.

Nini kitafuatia usikose Alhamisi    

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -