Tuesday, November 24, 2020

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU [115]

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

Ilipoishia Jumatatu

AKIWA kama mfanyakazi wa UN alikuwa amemuacha Shazayi Ikulu na kuongozana na jeshi hilo.

SASA ENDELEA

Jeshi la ulinzi la Pakistani, liliuzunguka mtaa mzima wa Ramat na miji ya karibu. Roika aliomba askari kumi, atakaoongozana nao kuingia kwenye jumba hilo, jumba lenye gholofa nne.

Askari kumi waliongozana na Roika wakiwa makini kutazama huku na kule. Wakiwa wanalikaribia jengo hilo, walimuona mzee mmoja akipita eneo hilo, akielekea msikitini. Mzee huyo alisimama na kuwatazama.

“Hawapo hapa muda mrefu walishahama,” aliongea mzee huyo akiwa na taa yake mkononi.

“Wamehama?” Roika aliuliza kwa mshangao.

“Ndio wamehama masaa kadhaa yaliopita hivyo ndani ya jengo hili hakuna mtu yeyote.”

Lakini ili kujiridhisha, Roika na askari hao, walianza kuingia kwenye kila chumba kuanzia gholofa ya kwanza hadi ya mwisho wakikagua kwa tahadhari kubwa. Ni kweli jumba lote lilikuwa halina mtu mali chache sana zilikuwa zimeachwa. Wakiwa wanajigawa kwenye vyumba vya juu, Roika pekee yake aliingia kwenye chumba kimoja kilichokuwa na chumba kidogo ndani yake. Alishtuka baada ya kumuona mtu mmoja akiwa amelala kitandani, aliiweka bastola yake vizuri na kupiga hatua kumsogelea mtu huyo, ambaye aligundua kuwa ni mwanamke. Alianza kuhisi kuwa huenda mtu huyo ni marehemu.

Kitendo cha kumgeuza mtu huyo, Roika alipatwa na mshtuko mkubwa. Moyo wake ulimpiga kwa maumivu makali, alipepesuka na kudondoka chini. Alibaki ametoa macho, asiamini kabisa kuwa yule anayemuona pale kitandani ni Ramona. Alihema mithili mbwa aliyekimbia maili nyingi.

“Ramona!” aliongea Roika akiwa ametoa macho kupita kiasi.

Akiwa katika kushangaa huko, askari wengine walikuwa wakisikika wakija kwenye chumba hicho. Bila kujali kuwa Ramona alikuwa amekufa au mzima, upesi alimshusha kitandani. Alilisogeza kabati liliokuwa karibu, akalidondosha juu ya kitanda. Alipanda juu ya kabati na kukifungua kimlango kidogo cha kuingia darini, kisha alishuka na kumbeba Ramona ambapo alimuingiza darini. Upesi alikifunga na kulitoa kabati juu ya kitanda. Alipomaliza kazi hiyo, alikaa chini huku akihema hovyo, kwani alikuwa amechoka sana.

Punde askari waliingia kwenye chumba hicho na kumkuta Roika akikagua kagua  droo za kabati.

“Mr Roika kuna jipya lolote ndani ya chumba hichi?” askari mmoja aliuliza.

“Hakuna lolote, tuondoke tu hawa watu wameshakimbia,” alijibu Roika.

Askari wote walitoka ndani ya chumba hicho wakiwa na Roika, ambapo walishuka chini na kumtaarifu kamanda wa jeshi kuwa, Swaba wamekwisha ondoka. Baadhi ya wananchi walisema kuwa, Swaba walielekea njia ya kusini. Jeshi lote lilielekeza nguvu kuelekea kule.

Mtaa wa Ramat ukaachwa bila mwanajeshi yoyote. Roika alipewa gari la peke yake kwa ajili ya kurudi ikulu. Alipofika barabara ya Alamayana, aligeuza kurudi mtaa wa Ramat kwa kasi, kwenda kumchukua Ramona ambaye hakujua kama alikuwa amekufa au ni mzima. Alimtoa darini na kumlaza kitandani. Alimtazama sana, bila kujizuia alijikuta anamwaga machozi mengi kama mtoto. Alishtuka baada ya kuona Ramona anapumua, moja kwa moja alijua kuwa alikuwa ni mzima. Upesi alimbeba na kutokana naye nje ya jengo hilo, ambapo alimpakia kwenye gari na kuondoka naye. Hakujua kilichomkuta mrembo huyo, ambaye kwa kiasi fulani  alikuwa bado akimpenda kwenye moyo wake.

Alimpeleka hadi hotelini kwake, walinzi wa hoteli walipomuuliza, aliwajibu kuwa, Ramona alikuwa amelewa. Moja kwa moja alimpeleka chumbani kwake na kumlaza kitandani kisha aliandika ujumbe mrefu kwenye karatasi na kuuacha mezani. Kwa kuwa ilitakiwa kesho asafiri, hakuwa na muda wa kukaa karibu na Ramona, alirudi upesi ikulu ambapo alimkuta Shazayi akiwa na furaha kwa kuwa kesho alijua kuwa atasafiri na yeye kuelekea Tanzania.

“Mpenzi umerudi salama,” aliongea Shazayi.

“Ndio namshukuru Mungu. Hata hivyo tumekuta Swaba wamekwisha kimbia mtaa ule, hivyo nimeliacha jeshi likielekea kusini mwa Ramat.”

“Sawa naomba ukapumzike, si unajua kesho tunasafiri?”

“Ni kweli mpenzi, basi usiku mwema.”

Roika alimbusu Shazayi na kila mmoja alielekea chumbani kwake kulala. Saa 11:00 alfajiri, msafara wa magari ya jeshi na polisi, ulikuwa njiani ukiwapeleka Roika na Shazayi uwanja wa ndege wa Islamabad. Rais Galim alikuwa amependa mwanaye akapumzike nchini Tanzania pamoja na mchumba wake. Lakini Shazayi alikuwa na hamu sana ya kumuona mtu aliyemuongezea damu mama wa mume wake mtarajiwa.

Uwanja wa ndege wa Islamabad ulikuwa na ulinzi mkali kuliko siku zote, ndege pekee ya Roika na Shazayi ilifanyiwa ukaguzi mara nyingi zaidi. Muda mfupi baadae, walipanda ndege na safari ya kuelekea Tanzania ilianza.

Kesho yake, walifika uwanja wa Julius Nyerere nchini Tanzania, saa mbili asubuhi. Umati mkubwa wa watanzania, ukiongozwa na Rais Jakaya Kikwete, uliwapokea uwanjani hapo. Baada ya kufika ikulu, waliongea mengi na Rais na kufanya sherehe kubwa.

Saa tisa alasiri, Roika na Shazayi walimuaga Rais Kikwete na mke wake na kuondoka ikulu ambapo walielekea nyumbani kwa mama yake na Roika.

Walipofika nyumbani, wakiwa nje ya nyumba Roika alimwambia Shazayi.

“Nataka mama akuone kwanza wewe. Tangulia ukamuone.”

Shazayi alitabasamu, aligeuka na kupiga hatua kuingia getini.

Mama Roika akiwa jikoni, akiwa anaimbaimba huku akipika, alishtuka kusikia sauti nyororo ya mwanamke ikimuita, alipogeuka, alipatwa na mshangao baada ya kumuona mwanamke mzuri wa kipakistani akitabasamu huku akitokwa na machozi.

MOHAMED WORDS

Biyanah mwanamke tajiri alikuwa hospitalini ikiwa ni siku ya tano tokea alipopigwa risasi na Ramona. Taarifa ya kwamba Roika alikuwa anakwenda kumuoa mtoto wa Rais, ilikuwa imemfanya kuugua ugonjwa wa akili.

Nashukuru kwa kuwa pamoja na mimi hadi sasa tunapofikia MWISHO wa hadithi hii, Mungu akubariki.

Usikose hadithi yangu nyingine inayoitwa NIMEBAKI MWENYEWE.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -