Saturday, January 16, 2021

UPENDO KUSHINDA UFAHAMU

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

Ilipoishia jana

“Nikubali kufanya hivi maana sina jinsi, Roika nisamehe na Mungu anisamehe pia. Nikimuua Roika mimi na kazi yangu tutakuwa salama. Siwezi kukubali kujipoteza mimi, wakati mama na mdogo wangu wananitegemea,” alijisemea Ramona wakati akipanda ngazi kuelekea ghorofa ya mwisho.

Ulinzi ulikuwa ni mkali tofauti na jana ndani ya jengo hilo la kikundi cha Swaba chenye ushirikiano na watu wa biashara za magendo. Wenye mtandao mkubwa duniani kote na makundi ya kigaidi na wa waasi mbalimbali.

SASA ENDELEA…

Watu wote mle ndani walikuwa wakimsubiri malkia wao aweze kuwaelezea ukaribu wake na mtu aliyelivamia jengo lao. Tayari kiongozi wa kikundi cha kigaidi, Zahil Bin Shaq pamoja na viongozi wengine wa biashara na kikundi cha Swaba, walikuwepo chumba cha mkutano. Watu wengine waliokuwa hawajafahamishwa juu ya Ramona kumfahamu mtu aliyeingia kwenye jengo lao, walishawakuwa wamejulishwa kabla Ramona hajafika.

Ramona aliingia ndani ya chumba cha mkutano, ambapo alivutiwa kiti na kukaa. Wote mle ndani walimsalimia kwa kuinamisha vichwa chini. Naye aliwaitikia kwa kuinamisha kichwa chini akionekana mwenye hofu kubwa.

Baada ya kukaa, wapiganaji wa kikundi cha Swaba walimleta Roika mbele ya mkutano akiwa anavuja damu. Ilionyesha alikuwa amepigwa sana. Moyo wa Ramona ulimuuma kupita kiasi. Maumivu aliyoyahisi yalikuwa yameuzidi uwezo wake wa kuyahimiri. Aliumia sana kumuona Roika wake katika hali ile. Lakini kwa kuwa alikuwa amekuja na lengo la kumuua, aliingiwa na roho ya ujasiri, akaitupa mbali  huruma ya mapenzi, huruma iliyokuwa inaonyesha kuwa ingeweza kumvunja moyo muda wowote, asiweze kutekeleza mauaji ili aweze kujiokoa yeye mwenyewe pamoja na kazi yake.

Roika aliinua macho na kumtazama Ramona kwa huruma asijue Ramona anafikiria nini juu yake.

Kiongozi Zahil Bin Shaq aliwaamuru wajumbe wote wakae kwenye viti baada ya kusalimiana. Baada ya wote kukaa kiongozi huyo alisema.

“Toka jana tulikuwa na mashaka na mtu huyu aliyekuwa ameingia kwenye jengo letu. Hajui kama ni kweli alikuwa akimfuatilia mdogo wake kama alivyotuambia. Lakini, tulihisi kuwa anafahamiana na madam  Ramona na tulipomuuliza madam akasema hamfahamu. Sasa ili kujua ni  kweli hamfahamu tulimuomba ampige risasi.”

Aliposema hivyo watu wote mle ndani walitikisa vichwa. Roika alizidi kupatwa na hofu ingawa alishakuwa amejihesabia kifo. Alijiuliza hivi ni kweli Ramona anaweza kumuua, jibu alilokuwa nalo lilikuwa ni hapana. Alichokuwa anakiogopa yeye ni kujitambulisha kuwa yeye ni mtu wa umoja wa mataifa akihofia kuuawa mbele ya kamera. Kwani watu wa umoja wa mataifa wanapaswa kutunza siri za umoja huo hata kama watakuwa wameshikwa na watu hatari.

Kiongozi Zahil aliendelea kuongea.

“Tunafanya hivi ili kujenga uaminifu miongoni mwetu. Maana kazi yetu ni ya tahadhari na umakini mkubwa.”

Aliposema hivyo alimgeukia Ramona na kumwambia.

“Madam Ramona, tunakuamini wewe ni mtu makini na ni mwanamke usiyeogopa kitu chochote. Tunaamini utatuthibitishia kuwa humfahamu mtu huyu.”

Ramona aliposikia hivyo alikitikisa kichwa chake akikubali kwa ujasiri hafifu.

Baada ya dakika mbili, mpiganaji wa kikundi cha Swaba alimletea Ramona bastola. Ramona aliipokea kwa ujasiri. lakini mapigo ya moyo wake yalianza kumwenda mbio za fujo. Aliinuka pale kwenye kiti na kusogea hadi pale Roika alipokuwa amepigishwa magoti. Wakati huo watu wote mle ndani walikuwa kimya wakimsubiri Ramona afanye maamuzi ili kuwaondolea wasiwasi.

Ramona alimtazama Roika kama vile hamjui. Alijikaza vilivyo asionyeshe hata chembe itakayojulisha kuwa  alikuwa akimfahamu mtu huyo. Lakini moyo wake uliokuwa unampenda Roika ndio uliokuwa unalalamikia, juu ya uamuzi anaotaka kuuchukua. Wakati huo moyo wa Roika ulizidi kumpenda Ramona ingawa Ramona alikuwa amekusudia kumuua. Tayari Roika alishakuwa ameyakabidhi maisha yake kwa Mungu akiomba Mungu ampokee kule aendako. Maana alijua kuwa kwa vyovyote vile Ramona hataweza kumuacha hai kwa kuwa atahitaji kuulinda uaminifu wake dhidi ya watu wake na kujilinda yeye mwenyewe.

Taratibu Ramona aliinua bastola akaielekeza kwenye kifua cha Roika. Akaikoki bastola yake vizuri tayari kwa kumuuondoa mtu ampendaye hapa duniani. Kwa huruma isiyo ya kawaida Roika alizidi kuhesabu pumzi yake ya kuendelea kuishi hapa duniani. Alimtazama Ramona kwa macho yaliyojaa fumbo la kimapenzi na woga wa hali ya juu. Moyo wake ukaridhia kuuawa na mwanamke ampendaye.

Nini kitafuata? Usikose kesho        

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -